Special thread: Wapenda vinywaji visivyo na kilevi (non alcoholic) na changamoto wanazokutana nazo wakikaa na walevi

Special thread: Wapenda vinywaji visivyo na kilevi (non alcoholic) na changamoto wanazokutana nazo wakikaa na walevi

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Habari wadau,

Mimi ni si mnywaji wa vinywaji vyenye kilevi ni mnywaji wa vinywaji visivyo na kilevi kama juice, soda, bavaria, nk. Najua wapo wenzangu ambao nao ni wapenzi wa vinywaji hivyo.

Nikiwa kama mnywaji wa vinywaji visivyo na vilevi hua nakutana na changamoto sana wakati nikitoka na marafiki, wengine hunilazimisha ninywe, wengine hunicheka.

Mara waseme nawajazia nzi kwenye meza zao, mara sasa utaweza kukaa kweli mpaka usiku, utaboereka, onja basi kidogo.

Ajabu ni kuwa napenda sana kucheza muziki, muonekano wangu mimi ni mcheshi,yani ukiniona nacheza utasema huyu kanywa, sioni aibu.

Haya twende kwenye hoja;

Ni kero gani ambayo unakutana nayo wewe usiyekunywa.
Na ni kwa namna gani unaondokana nayo.

Karibuni
 
Kuna siku nimekaa na jamaa bar, wao wanakunywa pombe zao, Mimi nikaagiza maji, kuna jamaa wa meza nyingine alitoka wash room akapita mezani kwetu akauliza "huyu jamaa anafuga mamba tumboni, mbona anakunywa maji ? "
 
Mm sinywi kilevi chochote hua natumia Maziwa tu.. mara ya kwanza nilikua nakunywa doda lkn 4/10/2017 nilikunywa fanta orange tumbo likauma nikapigwa Dripu 4 Now ni maziwa Tu..

Pombe si nzuri, mm sina changamoto yoyote maana rafiki zangu wote ni waimba kwaya nami pia..
 
Back
Top Bottom