Special thread: Wapenda vinywaji visivyo na kilevi (non alcoholic) na changamoto wanazokutana nazo wakikaa na walevi

Special thread: Wapenda vinywaji visivyo na kilevi (non alcoholic) na changamoto wanazokutana nazo wakikaa na walevi

Mimi sinywi kinywaji chenye kilevi ila kampani yangu kubwa wanapiga masanga, ila sikutani na hizo changamoto wanaheshimu kile nafanya akiwa mgeni kwangu atanishangaa sababu ya muonekano wangu, ni mjanja mjanja hawez amini kama situmii pombe ila maswahiba zangu wanaelewa na nikikosekana katika mitoko yetu huwa wanalalamika hapanogi kabisa.
Nimependa hii
 
Kuna siku nilikaa na walevi, wao wakaagiza vyao mi nikaagiza maji makubwa, nilishambuliwa sana, mmoja wao aliniuliza "hivi unafuga samaki, mbona unaagiza maji lita nzima?"
[emoji23] [emoji23] [emoji23] umenifurahisha sana agiza maji mengine nakuja kilipia
 
Kuna siku nilikaa na walevi, wao wakaagiza vyao mi nikaagiza maji makubwa, nilishambuliwa sana, mmoja wao aliniuliza "hivi unafuga samaki, mbona unaagiza maji lita nzima?"
Ahhaahahahahha
 
Mm sinywi kilevi chochote hua natumia Maziwa tu.. mara ya kwanza nilikua nakunywa doda lkn 4/10/2017 nilikunywa fanta orange tumbo likauma nikapigwa Dripu 4 Now ni maziwa Tu..

Pombe si nzuri, mm sina changamoto yoyote maana rafiki zangu wote ni waimba kwaya nami pia..
aiseeee kumbe tusiotumia vilevi tuko wengi kiasi
 
Back
Top Bottom