Special Thread: Ya kale ni dhahabu

Special Thread: Ya kale ni dhahabu

FB_IMG_1619855979220.jpg
 
RAY C

KUNA wakati unaweza kutamani kurudisha nyakati nyuma lakini siyo jambo rahisi. Kamwe huwezi kurudisha siku zilizopita. Lakini ni rahisi sana kuvuta kumbukumbu ya kilichotokea nyuma. Mwanamuzuki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amenikumbusha nyuma. Amenikumbusha kwenye enzi zake. Miaka ya katikati mwa 2000. Wakati akiwa Kiuno Bila Mfupa kwelikweli! Kipindi ambacho alikuwa ghali zaidi kwenye Bongo Fleva miongoni mwa wasanii wenzake wa kike. Wakati huo haikuwa rahisi kumuona mara kwa mara.

Nyakati hizo, Ray C alikuwa na foleni ya watangazaji wa vipindi vya Bongo Fleva waliotaka kufanya naye mahojiano. Shoo kila wikiendi, ndani na nje ya Bongo. Namzungumzia Ray C wa ‘Nimezama’. Achana na wimbo huo kuna pini nyingine inaitwa ‘Mahaba ya Dhati.’ Unakumbuka wakati huo?

Nyimbo nyingine alizopata kutesa nazo Ray C ni pamoja na Uko Wapi, Na Wewe Milele, Wanifuatia Nini, Mapenzi Matamu, Sogea Sogea na kibao cha miaka ya hivi karibuni cha Mama Ntilie alichoshirikishwa na wasanii Gelly wa Rymes akiwa na AT.

Ray C asiyekauka kwenye chati mbalimbali za wiki kwenye redio mbalimbali. Ilikuwa ukisikiliza Bamiza Top 20 (Magic FM) utamsikia, Ladha 10 za Bongo (Radio One) utamsikia au ukifuatilia Top 20 (Clouds FM) lazima umsikie. Vituo vyote hivyo na vingine vilivyokuwa vikitesa wakati huo, alikuwa katika chati za juu zaidi.

Ladha ya Ray haikuwa ya kitoto. Kifupi Ray C alikuwa juu, kiasi kwamba alikuwa akisumbuana vikali na wasanii wa kiume. Ray C alikuwa akipeta katikati ya Jide, Dataz, Zay B, Stara Thomas na wengineo. Ushindani ulikuwa wa hali ya juu. Ilikuwa ni kawaida kwake kusafiri hadi China kwa ajili ya kurekodi video ya wimbo wake mpya. Kipindi kile, msanii kusafiri hadi nje ya nchi, tena sehemu kama China ilikuwa siyo jambo dogo.

Lakini Ray wa sasa amebadilika. Amepitia mengi hapo katikati ambayo sipendi kuyakumbusha maana sasa ni Ray C mpya.

Vip kwa mtazamo wako umemisi nini toka kwa mrembo huyu.

1695052397727.jpg
 
Mapema Miaka ya 1980's ,Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani Michael Jackson Kushoto akiwa na Moja ya Wafalme wa Muziki wa Rock duniani "Freddie Mercury" Hapo Kulia....Je ni Nani huyu Freddie Mercury?

Mercury alizaliwa Tarehe 5 September Mwaka 1946 Stone Town Zanzibar akipewa jina la Farrokh Bulsara na Wazazi wenye Asili ya India,....Na Kabla ya Uhuru Wa Tanganyika na Zanzbar Freddie alisomeshwa Shule za Bweni Nchini Uingereza, hii ni Kabla ya Kurejea Zanzibar baada ya Kumaliza Sekondari na Kisha kukimbia Tena na kuelekea Middlesex Uingereza na Familia yake mwaka 1964 Wakikimbia Machafuko na Vurugu Wakati wa Mapinduzi kule Zanzibar, akahamia UK, akapewa Uraia wa Uingereza na Jina Jipya.

Baada ya kusomea Muziki kwa Miaka kadhaa Mercury alianza kuitikisa Dunia ya Burudani Miaka ya 1970, Akiwa na Band Queen Mercury alisifika Duniani kwa uandishi wake matata na Namna yake ya Ku-perform Katika Jukwaa na vibao vyake Vikali vilivyotamba Duniani huku alisifika kwa Kuandika vibao Kama vile "Killer Queen", "Bohemian Rhapsody", "Somebody to Love", "We Are the Champions", "Don't Stop Me Now" na "Crazy Little Thing Called Love".

Freddie Mercury ambaye alikuwa akijihusisha na Vitendo haramu Vya Ushoga aligundulika kuwa na Virusi vya Ukimwi (HIV-AIDS) mnamo Mwaka 1987 Lakini aliendelea kurekodi Muziki na albamu zake mpaka alipofikwa na Mauti 24 Nov 1992....na Mwaka huo huo 1992 baada ya Mauti yake liliandaliwa Concert kubwa la Rock Katika Uwanja wa Wembley kumkumbuka Gwiji huyo wa Waingereza....na Baada ya Mauti yake waliendelea kumkumbuka kwa Tuzo Mbali Mbali Kama vile Rock and Roll Hall of Fame (2001), Ivor Novello Award for Outstanding Song Collection from the British Academy of Songwriters, Composers, and Authors(2005), Songwriters Hall of Fame(2003), UK Music Hall of Fame (2004), ikitanguliwa na Ile ya 1990 akiwa hai (Brit Award for Outstanding Contribution to British Music).

1695239806501.jpg
 
Hussein Macheni, enzi za Uhai wake. Mwamba huyu ndiye alikuwa Mmiliki wa Baa maarufu ya Macheni eneo la Magomeni Mapipa. Hii ilikuwa zaidi ya baa kwani hakuna Burudani ambayo ilikosekana mahali hapo. Macheni alifariki tarehe 28 mwezi Mei mwaka 2016.

1695282645286.jpg
 
Mapema Miaka ya 1980's ,Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani Michael Jackson Kushoto akiwa na Moja ya Wafalme wa Muziki wa Rock duniani "Freddie Mercury" Hapo Kulia....Je ni Nani huyu Freddie Mercury?

Mercury alizaliwa Tarehe 5 September Mwaka 1946 Stone Town Zanzibar akipewa jina la Farrokh Bulsara na Wazazi wenye Asili ya India,....Na Kabla ya Uhuru Wa Tanganyika na Zanzbar Freddie alisomeshwa Shule za Bweni Nchini Uingereza, hii ni Kabla ya Kurejea Zanzibar baada ya Kumaliza Sekondari na Kisha kukimbia Tena na kuelekea Middlesex Uingereza na Familia yake mwaka 1964 Wakikimbia Machafuko na Vurugu Wakati wa Mapinduzi kule Zanzibar, akahamia UK, akapewa Uraia wa Uingereza na Jina Jipya.

Baada ya kusomea Muziki kwa Miaka kadhaa Mercury alianza kuitikisa Dunia ya Burudani Miaka ya 1970, Akiwa na Band Queen Mercury alisifika Duniani kwa uandishi wake matata na Namna yake ya Ku-perform Katika Jukwaa na vibao vyake Vikali vilivyotamba Duniani huku alisifika kwa Kuandika vibao Kama vile "Killer Queen", "Bohemian Rhapsody", "Somebody to Love", "We Are the Champions", "Don't Stop Me Now" na "Crazy Little Thing Called Love".

Freddie Mercury ambaye alikuwa akijihusisha na Vitendo haramu Vya Ushoga aligundulika kuwa na Virusi vya Ukimwi (HIV-AIDS) mnamo Mwaka 1987 Lakini aliendelea kurekodi Muziki na albamu zake mpaka alipofikwa na Mauti 24 Nov 1992....na Mwaka huo huo 1992 baada ya Mauti yake liliandaliwa Concert kubwa la Rock Katika Uwanja wa Wembley kumkumbuka Gwiji huyo wa Waingereza....na Baada ya Mauti yake waliendelea kumkumbuka kwa Tuzo Mbali Mbali Kama vile Rock and Roll Hall of Fame (2001), Ivor Novello Award for Outstanding Song Collection from the British Academy of Songwriters, Composers, and Authors(2005), Songwriters Hall of Fame(2003), UK Music Hall of Fame (2004), ikitanguliwa na Ile ya 1990 akiwa hai (Brit Award for Outstanding Contribution to British Music).

View attachment 2756381
Mpaka leo hii hakuna aliyeweza kuvunja rekod yake ya kukontrol watu kwenye show.
 
KABURI MOJA,CITY CENTER POSTA.

(KABURI LILOGOMA KUHAMISHWA)

Hili kabuli hili historia yake haijaandikwa sehemu yoyote

Ni kaburi la aliyekuwa SHARIFA (Kiongozi) wa kipindi Mtawala wa ZANZIBAR, Bwana MAJID BIN SAID ambaye ndiye aliyeanzisha Darra Salaam (Dar es Salaam).

Ni Kaburi la Sharifa ambaye alikuwa ndiyo mwenyeji wa eneo la Pwani ya Mzizima eneo la Posta makazi yake yalikuwa pale palipo na Old boma (Leo)

Old Boma ilikuwa ni nyumba rasmi ya Wageni wa Sultani Majid Bin Said jirani na Rotana Hotel (Leo),

Huyu Sharifa ndiye aliyempokea Sulutani MAJID BIN SAID aliyetawala ZANZIBAR Mwaka 1834 hadi 1870

Nakukumbusha wakati huo ukiwa Sulutani wa Zanzibar basi unatawala Pwani ya Mzizima (Dar es Salaam) ndiyo maana Sultani Majid bin Said alikuwa na makazi Zanzibar na Mzizima (Dar es Salaam)

Baba yake Sulutani MAJID BIN SAID akiwa Sulutani wa Zanzibar Bwana SAID BIN SULTANI ambaye alikuwa anatawala Pwani ya Mogadishu (SOMALIA) hadi Pwani ya Delagoa siku hizi ndiyo Maputo (Mozambique)

Huyu kiongozi alifariki mwaka 1862 na kaburi hilo linakaribia miaka 200 sasa.
Eneo hilo lilikuwa kwa ajili ya maziko ya Watu Mashuhuri,Viongozi wa Serikali ya Sultani na Viongozi wa dini wa miaka hiyo

Kama unavyojua Wazungu,Baada ya Ukoloni kuja na Wajerumani kusimika serikali yao rasmi walianza Kuipanga Dar es Salaam katika zone 3.

kabla Master plan yetu hii ya baada ya uhuru 1979 alipanga mji wa Dar es salaam kwa matabaka.

1.Wazungu zone ya Posta

2.Wahindi na Waarabu zone ya Mnazi mmoja

3.Watu weusi zone ka Kariakioo

Wakati huo Dar es Salaam inaishia Kariakoo tuh, Ukisogea mitaa ya Jangwani au Magomeni Kukutana na Simba ni Jambo la kawaida sana

Mtaa wa Samora wakati huo ukiitwa Barra Rasta yaani (Main Avenue).

Wajerumani waliubadilisha jina na kuuita Under de Acacien (Under the Acacia trees)

Na waingereza wakauita (Acacia Avenue) baada ya Vita ya pili ya Dunia.

Tulipopata uhuru tukauita Independence Avenue (baada ya 1961)

Na baada ya kifo cha Samora Michael 1986 mtaa uliitwa "SAMORA AVENUE"

kama kumbukumbu ya kumuenzi mpigania Uhuru huyo na Rais wa kwanza wa Msumbiji.

Katika kipindi chote hiki kaburi hili limeendelea kuwepo,Sababu Wajerumani walihamisha Makaburi Mengine lakini hili walilishindwa

Na Kila Rais aliyetawala wakati huo Serikali yake katika Kujenga miundombinu walijaribu kuhamisha kaburi hili

Awamu ya Mwl Nyerere miaka ya 1960 hadi 80 walijaribu zaidi ya mara 4 kulihamisha ikishindikana

Akaja Rais Ally Hassan Mwinyi serikali yake miaka ya 80 hadi 90 katika Kujenga miundombinu walijaribu kuliondoa pia ikashindikana

Akaja Rais Mkapa halikadharika walishindwa kuliondoa

Awamu ya Mwisho iliyojaribu kuliondoa hiki kaburi ilikuwa awamu ya Rais Jakaya Kikwete, na wenyewe walishindwa

Baada ya hapo hakuna taarifa yoyote tena kwa awamu ya Magufuli au hii ya Rais Samia kama na wao walijaribu au wana nia ya Kuliondoa.

NAMNA LINAVYOJILINDA

Mara kadhaa walipokuwa wanapeleka Kijiko (Excavator) au Bull dozer (Tingatinga) walikuwa wamefanikiwa kulitoboa

Lakini lilikuwa linatoa harufu kali mfano wa "SULPHUR" kutoka ndani ya Kaburi na Kufanya wanaolibomoa Kukohoa sana,Kukosa Pumzi na hata Kupoteza Fahamu

Ile harufu kali huenea eneo la Mzingo (DUARA) mpaka umbali wa mita 500 na harufu hudumu kwa ukali uleule kwa siku nyingi bila Kupungua madhara yake.

Serikali ilipokuwa inashindwa kulibomoa na kusababisha Kero hiyo ya harufu kali.

Mara zote walikuwa wanaenda Kigamboni Kuchukua Wazee wa Ukoo mmoja wenye asili ya Kiarabu

Ndiyo walikuwa wanarudi kwenye kaburi kufanya tambiko na kuliziba kwa kulijengea Juu ili harufu ile kali isiendelee kutoka kutokea ndani ya Kaburi.

HILI NDILO KABURI MOJA,POSTA.

1696589873029.jpg
 
Back
Top Bottom