KABURI MOJA,CITY CENTER POSTA.
(KABURI LILOGOMA KUHAMISHWA)
Hili kabuli hili historia yake haijaandikwa sehemu yoyote
Ni kaburi la aliyekuwa SHARIFA (Kiongozi) wa kipindi Mtawala wa ZANZIBAR, Bwana MAJID BIN SAID ambaye ndiye aliyeanzisha Darra Salaam (Dar es Salaam).
Ni Kaburi la Sharifa ambaye alikuwa ndiyo mwenyeji wa eneo la Pwani ya Mzizima eneo la Posta makazi yake yalikuwa pale palipo na Old boma (Leo)
Old Boma ilikuwa ni nyumba rasmi ya Wageni wa Sultani Majid Bin Said jirani na Rotana Hotel (Leo),
Huyu Sharifa ndiye aliyempokea Sulutani MAJID BIN SAID aliyetawala ZANZIBAR Mwaka 1834 hadi 1870
Nakukumbusha wakati huo ukiwa Sulutani wa Zanzibar basi unatawala Pwani ya Mzizima (Dar es Salaam) ndiyo maana Sultani Majid bin Said alikuwa na makazi Zanzibar na Mzizima (Dar es Salaam)
Baba yake Sulutani MAJID BIN SAID akiwa Sulutani wa Zanzibar Bwana SAID BIN SULTANI ambaye alikuwa anatawala Pwani ya Mogadishu (SOMALIA) hadi Pwani ya Delagoa siku hizi ndiyo Maputo (Mozambique)
Huyu kiongozi alifariki mwaka 1862 na kaburi hilo linakaribia miaka 200 sasa.
Eneo hilo lilikuwa kwa ajili ya maziko ya Watu Mashuhuri,Viongozi wa Serikali ya Sultani na Viongozi wa dini wa miaka hiyo
Kama unavyojua Wazungu,Baada ya Ukoloni kuja na Wajerumani kusimika serikali yao rasmi walianza Kuipanga Dar es Salaam katika zone 3.
kabla Master plan yetu hii ya baada ya uhuru 1979 alipanga mji wa Dar es salaam kwa matabaka.
1.Wazungu zone ya Posta
2.Wahindi na Waarabu zone ya Mnazi mmoja
3.Watu weusi zone ka Kariakioo
Wakati huo Dar es Salaam inaishia Kariakoo tuh, Ukisogea mitaa ya Jangwani au Magomeni Kukutana na Simba ni Jambo la kawaida sana
Mtaa wa Samora wakati huo ukiitwa Barra Rasta yaani (Main Avenue).
Wajerumani waliubadilisha jina na kuuita Under de Acacien (Under the Acacia trees)
Na waingereza wakauita (Acacia Avenue) baada ya Vita ya pili ya Dunia.
Tulipopata uhuru tukauita Independence Avenue (baada ya 1961)
Na baada ya kifo cha Samora Michael 1986 mtaa uliitwa "SAMORA AVENUE"
kama kumbukumbu ya kumuenzi mpigania Uhuru huyo na Rais wa kwanza wa Msumbiji.
Katika kipindi chote hiki kaburi hili limeendelea kuwepo,Sababu Wajerumani walihamisha Makaburi Mengine lakini hili walilishindwa
Na Kila Rais aliyetawala wakati huo Serikali yake katika Kujenga miundombinu walijaribu kuhamisha kaburi hili
Awamu ya Mwl Nyerere miaka ya 1960 hadi 80 walijaribu zaidi ya mara 4 kulihamisha ikishindikana
Akaja Rais Ally Hassan Mwinyi serikali yake miaka ya 80 hadi 90 katika Kujenga miundombinu walijaribu kuliondoa pia ikashindikana
Akaja Rais Mkapa halikadharika walishindwa kuliondoa
Awamu ya Mwisho iliyojaribu kuliondoa hiki kaburi ilikuwa awamu ya Rais Jakaya Kikwete, na wenyewe walishindwa
Baada ya hapo hakuna taarifa yoyote tena kwa awamu ya Magufuli au hii ya Rais Samia kama na wao walijaribu au wana nia ya Kuliondoa.
NAMNA LINAVYOJILINDA
Mara kadhaa walipokuwa wanapeleka Kijiko (Excavator) au Bull dozer (Tingatinga) walikuwa wamefanikiwa kulitoboa
Lakini lilikuwa linatoa harufu kali mfano wa "SULPHUR" kutoka ndani ya Kaburi na Kufanya wanaolibomoa Kukohoa sana,Kukosa Pumzi na hata Kupoteza Fahamu
Ile harufu kali huenea eneo la Mzingo (DUARA) mpaka umbali wa mita 500 na harufu hudumu kwa ukali uleule kwa siku nyingi bila Kupungua madhara yake.
Serikali ilipokuwa inashindwa kulibomoa na kusababisha Kero hiyo ya harufu kali.
Mara zote walikuwa wanaenda Kigamboni Kuchukua Wazee wa Ukoo mmoja wenye asili ya Kiarabu
Ndiyo walikuwa wanarudi kwenye kaburi kufanya tambiko na kuliziba kwa kulijengea Juu ili harufu ile kali isiendelee kutoka kutokea ndani ya Kaburi.
HILI NDILO KABURI MOJA,POSTA.