Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ushahidi kutoka Urusi uko wapi??
Migambo wa Donetsk wanatumia aina hii ya makombora ya Tochka-U. Ukraine wanayo pia. Kipande cha kombora kilichokutwa kilikuwa na maandishi ya Kirusi (si Kiukraine) "za detami" - yaani "kwa ajili ya watoto" wetu.
Mkuu kuanzia sasa kama hauwezi kujibu hoja zangu acha kuwa unajibu coment zangu, kwa sababu umenikera maana kazi yako kueneza propaganda na kurukia coment za watu lakini ukibanwa kwa hoja una kimbia hau jibu.

Eti ilikuwa na maandishi ya kirusi na si ya kiukraine sasa makombora si yali tengenezewa nchini Urusi kiukraine kitoke wapi tena?

Aina hii ya makombora Urusi iliacha kuyatumia tangu mwaka 2019 na Ukraine inayo mengi mno iliyarithi kutoka Usoviet na imekuwa ikiya tumia dhidi ya wanao taka kujitenga hata kabla vita haijaanza.

Aidha hilo shambulizi wamelifanya kwa bahati mbaya baada ya kukosea shabaha au wamelifanya makusudi ili kuendeleza vita vya kipropaganda dhidi ya Urusi ya kwamba Urusi inauwa raia.

Ukitaka kujua Ukraine imehusika angalia mwitikio wa vyombo vya habari habari hii haijapewa uzito ingekuwa Urusi kahusika hii ndio ingekuwa habari ya dunia nzima.
 
Maandishi kwenye Roketi ni ya mkono. MTU aliandika maneno Yale Kwa rangi. Wanamigambo ya Putin kutoka Donetsk wanatumia pia
 
J
Wewe unaongelea S-300 kwa mrussi aliyeitengeneza mwenyew? Kwanini msipeleke patriot zenu?
Jibu swali LA msingi mkuu!

Russia aliapa kuwa misafara ya siraha kutoka nje ya Ukraine ni shabaha halali kwake!
Then umishajibu utaendelea na maelezo hayo ya Russia kuiteneneza hivyo system

# (ingawa alisema atalipua siraha zozote kutoka nje na si kuwa zenye origin ya West)
 
Maandishi kwenye Roketi ni ya mkono. MTU aliandika maneno Yale Kwa rangi. Wanamigambo ya Putin kutoka Donetsk wanatumia pia
Kwa hiyo mkuu maandishi ya kirusi ndio ushahidi ya kwamba Urusi ana husika?

Kwa hiyo maandishi yangekuwa ya kiingereza tunge ituhumu wingereza sio?

Hata waukraine kirusi wana kijua sana tu kwa sababu wale ni jamii moja.

Ukiona vyombo vya habari havijaipa nguvu taarifa fulani kwenye huu mgogoro basi jua hiyo habari ni hasi kwa Ukraine.

Hilo shambulizi linge fanywa na Urusi ndio ingekuwa habari ya dunia hadi vikao vya umoja wa mataifa vingekuwa vimeitishwa.
 
Hii ODESA lazima ibakie RUSSIA
Waache wahangaike weee ila ODESA jamaa wanapita nayo
UKRAINE inatakiwa ibakie kama morogoro yaani
Mkuu kuwa makini..
Usije ukageuza maelezo baadae ,ukasema lengo lilikuwa tu kupunguza nguvu za kikeshi.
*Maana nakumbuka maelezo yako kuwa lengo LA operation siyo kumtoa Zelensky madarakani ,japokuwa Putini alitangaza hadharani kuwa moja ya malengo ni kuutoa utawala wa Nazi (na alishawahi zaidi ya Mara moja kuwaambia wanajeshi wa Ukraine wamtoe madarakani) ; but baadhi ya member humu wanakana hili kutokana na situation kwenda kinyume na matarajio.

#Nakukumbusha tu mkuu!
 
Aiseee ...........!!!!!!!!!!!
Wewe umedata.....
 
🤣🤣
Duh!
Naona sasa umepoteza chaneli,....zote zinaonyesha chengachenga 🤣🤣🤣😅
 
Kinachotokea Ukraine ni uhalisia ndugu,hisia zitafanya usione ukweli. Hii ni operation ambayo lazima iwe na matokeo, huenda usiyapende.
 
Ila nchi za magharibi na USA wanalaana kabisa. Tunaoumia ni sisi. Hata na raia wao. Viongozi wao hawana shida. Mkate mafuta ya kupikia gesi posho na sijuwi raha gani duniani wanapata.
Hivi mwajuwa mpaka leo USA wanafanya biashara zingine na Russia?!
Kuanzia Uranium, biological weapons na technology?!
 
Atakuambia yukraine haiko nato asa sijui iko afrika ....??
 
Now jukwaa linahamia kwenye bible [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]walianzia kwenye vita ya $ vs Ruble,wakarukia 'malengo ya Russia yametimia' hatujakaa sawa wakaja na 'Ukraine amekubali masharti yote ya Russia' ilivyoshindikana wakahamia 'Donmbass,Donesk zinakwenda na maji' na sasa wamefika hapa kutuelezea yaliyoko kwa Bible.Lakini upande wa pili silaha zinapelekwa wazi tu tena bila kificho,misafara ya magari inayopeleka vifaa inaonyeshwa,aliyetoa mkwara mbuzi wa yeyote atakaeisaidia Ukraine atakiona cha moto yuko anambwela tu hana cha kuwafanya hao NATO,sababu walishamuona ni mwepesi kama moto wa mabua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…