Ukifikiria kama hivi basi utaingia kwenye matatizo kama yaliyomkuta Ukraine. Russia haitaji uwe mshirika wake. Anachohitaji ni usalama wa nchi yake; lielewe dhumuni na mantiki ya Russia. Na hakuna anayepinga kama Russia naye kijeshi ni mkubwa kama huyu mkubwa aliye na ushawishi.
Nimejaribu kuirejea historia lengo ni kupata kujua endapo ukiwa kwenye nafasi kama ya Ukraine uishi vipi! Historia inatufunza kwa Cuba baada ya kumkaribisha Soviet aweke makombora yake. Cuba ni pua na mdomo na US. US kwake ikawa ni tishio. Alichokifanya aliwapiga vikwazo Cuba. Haikutosha akajaribu kufanya mapinduzi ila yakashindwa.
Huyu ni mwenye nguvu ya kijeshi na ushawishi alitumia nyenzo zake. Mwenye nguvu ya kijeshi peke yake unafikiri atatumia nguvu ipi?
Kingine umezungimzia vikwazo kwa Mrusi tambua ya kwamba havitomuathiri peke yake. Kwa namna moja na nyengine vita athiri na wengine kwa sababu: Russia ndiyo nchi ya 3 duniani (kama sijakosea) inayozalisha mafuta kwa wingi baada ya mashariki ya kati. Russia naye ni mzalishaji mkubwa wa ngano duniani. Russia ni miongini mwa nchi zinazozalisha gesi kwa wingi duniani.
India, Misri, China n.k zinategemea ngano ya kutoka Russia. Misri inatumia takribani $ billion kadhaa kununua ngano Russia. Bara la ulaya wanategemea gesi kutoka Russia kwa % kubwa. Kuna nchi nyengine zinategemea kwa 100% gesi ya Russia zipo Ulaya na huku wanataka kumtoa kwenye mfumo wa SWIFT hayo malipo mtayafanya kwa njia gani? Ukraine yenyewe inategemea gesi ya Russia.
UK anatumia sana anga ya Russia kwenda New Zealand, Australia n.k Russia naye kampiga vikwazo vya kutotumia anga yake. Ina maana UK ata-change route ambayo itakuwa ni ndefu sana (hapa gharama za mafuta zitaongezeka) itasababisha gharama kwa mteja kuwa juu sana.
Hivyo haya masuala ni mapana. Russia wataathirika ila Russia hatoathirika peke yake. Unampiga vikwazo huku unategemea gesi kutoka kwake naye akiongeza gharama za mauzo ya gesi mtafanyaje?
Nafikiri kwa kiasi fulani tumeelewana?