Punguza jazba. Angalia mwenzako Galip
#39,643 aliandika nini:
"Finland Gas ni 94 yote anatoa Russia, Oil 68 yote atoa Russia."
hapo anarudia yaleyale niliyotaja mimi. Unalalamika nini??
majadiliano yalianza nikimjibu Galip
#39,627 alipoandika:
"Finland huyu anapokea 94% ya Oil and Gas kutoka Russia" - ambayo si kweli; 94% zinahusu gesi pekee. Kwa mafuta ni kiwango kidogo zaidi (bado kubwa)
Nilichosema ni: gesi si muhimu vile nchini Finland, maana ni asilimia 5-7 ya mahitaji ya nishati pekee. Kama ungejielimisha, ungejua pia wanaitumia katika sekta gani. Kwa sehemu hiyo ya nishati yao, si vigumu kupata mbadala.
Hadi sasa tishio la Urusi ilikuwa kukata gesi ya Finland. Hapo Finland yenyewe inaona si tatizo.
Kama Urusi ingetisha kukata pia mafuta wiki hii, mambo yangekuwa tofauti.
Ila hii hawakusema.
Kwa namna yoyote, wakifanya hivyo (gesi au mafuta), wanavunja mikataba. Hatua kama hii italeta matatizo mengine.