Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nijuavyo Mimi Russia haiwezi kuondoa majeshi huko Ukraine. Eneo la mashariki la Ukraine Sasa ni la warusi..
Nafikiri usahihi ni linashikiliwa na warusi na si la warusi.
 
Hizi nchi zote za Africa mashariki ziko pamoja na US kwa kujua ama kwa kutokujua... Kwa kutaka ama kwa kutokutaka.

Watu Wana base karibia kila nchi unaanzaje kuwakataa[emoji16], huyo mkenya ndio usiseme kila siku anasaidiwa kwenye vita huko
Inawauma sana hawa wanao ichukia amerika lakini nchi yao ni mshirika wake mkubwa.
 
Napata shida sana kukuelewa kiswahili unachotumia kitofauti sana.

Zaidi ya ugumu wa kuelewa lugha unayotumia sijaona cha maana ulichoandika kujibu post yangu.

Alafu juu unadai wafini wameona hawapo salama (baada ya ukr invasion) alafu chini unasema hwaogopi jeshi la urusi. Sasa kama hawaogi wanakimbilia/lazimisha kujiunga NATO ili nini!? Umeona upupu unaoongea ulivyo!?
Mwanzoni hawakuwa wanataka kujiunga NATO, baada ya Ukr kuvamiwa na wao wakaona hawako salama wakataka kujiunga NATO lakini hapo hapo hawaogopi[emoji1787] unachekesha! Au ndio lugha inasumbua!?
Nimetoa taarifa tu kuhusu habari kutoka Finland.
a) idadi ya wananchi wanaopenda kujiunga na NATO imeongezeka kutoka 20% mwezi wa pili hadi 70% sasa. Je, wewe ungeeleza mabadiliko hayo vipi?
b) Wanasiasa wa Finland wanasema hawaogopi jeshi la Urusi.
Mimi ninaichukua kwamba, wakiona udhaifu wa jeshi la Putin jinsi ulivyoonekana huko Ukraine, wanaamini hawatashindwa. Ila wanajua vita ingeleta uharibifu mwingi. Hivyo wanaimarisha ulinzi kwa kujiunga na NATO.
Je, wewe ungeeleza maoni yao vipi?
 
Uswizi yaamua kutofautiana na Marekani+NATO, yaziachia mali za Russia ilizozizuia kutokana na mzozo wa Ukraine...Serikali ya Uswizi imesema haiwezi kushikilia mali za Russia kibubusa, wakati hakuna sababu zozote za msingi za kufanya hivyo.

Taasisi ya kimarekani yalalamikia msimamo huo wa serikali ya Uswizi na kuiita Uswizi kuwa muwezeshaji mkubwa wa harakati za Putin. Serikali ya Uswizi imekemea upotoshaji huo, na Rais wa Uswizi ameitaka serikali ya Marekani kurekebisha huo upotoshaji alipozungumza na waziri wa mambo ya nje wa Marekani

View attachment 2222496 View attachment 2222497
Swiss Wana akili,wanajua huo ndio ulikua unaenda kua mwisho wa wao kua offshore tax heaven.
 
33F95C9E-66F2-4737-AD0E-D7F3F4975F0D.jpeg


Picha inasema mengi sana hii na inafikirisha sana

Tujikwamue

Britanicca
 
Ni vema sana Kabisa mwananchi anaonekana ana fursa kujikomboa ila anataka nyingine 😂
 
94% unaikataa 68% unaikubali una akili sawa sawa wewe? Aliyekwambia matumizi ya Oil Finland ni 68% nani?
Punguza jazba. Angalia mwenzako Galip #39,643 aliandika nini:
"Finland Gas ni 94 yote anatoa Russia, Oil 68 yote atoa Russia."
hapo anarudia yaleyale niliyotaja mimi. Unalalamika nini??

majadiliano yalianza nikimjibu Galip #39,627 alipoandika:
"Finland huyu anapokea 94% ya Oil and Gas kutoka Russia" - ambayo si kweli; 94% zinahusu gesi pekee. Kwa mafuta ni kiwango kidogo zaidi (bado kubwa)

Nilichosema ni: gesi si muhimu vile nchini Finland, maana ni asilimia 5-7 ya mahitaji ya nishati pekee. Kama ungejielimisha, ungejua pia wanaitumia katika sekta gani. Kwa sehemu hiyo ya nishati yao, si vigumu kupata mbadala.
Hadi sasa tishio la Urusi ilikuwa kukata gesi ya Finland. Hapo Finland yenyewe inaona si tatizo.
Kama Urusi ingetisha kukata pia mafuta wiki hii, mambo yangekuwa tofauti.
Ila hii hawakusema.
Kwa namna yoyote, wakifanya hivyo (gesi au mafuta), wanavunja mikataba. Hatua kama hii italeta matatizo mengine.
 
Akiri za kiambiwa changanya na zako
Twenty European natural gas buyers have opened accounts with Gazprombank so they can pay in rubles, a person close to Kremlin-controlled energy giant Gazprom told Bloomberg.
We are calmly waiting for them to face Legal action.
IMG_20220513_124312_347.jpg
EU Leaders wapo kama wadada wa kiswahili, leo anakutukana we sio size yake kesho anakutumia txt "baby uko wapi", "nitumie Vocha mpenzi", So stupid indeed
 
Back
Top Bottom