LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Haya mazungumzo ni mwanya wa mmoja wao kujizatiti zaidi ... russia baada ya mazungumzo hata yakifail itabidi angalie namna zaidi ya kuendeleza majadiliano kuliko kuendela kuzichapa...
Nae anaendelea kujaza majeshi na vifaa 👇

Screenshot_20220228-210034.png
 
Mkuu no officia recognized source on the impact of their talks...hiyo kuna jamaa mmoja mfaransa nilion tu insta kacomment hivyo kwamba inasemekan moja ya maafikiano aliyowek mezan bwana mkubwa putin ni kustep down kwa rais zelenskyy...hivyo kwa hali iliyopo yawezekana ndo ivyo na ata icho kikao cha pili huenda kisizae matunda na ndio maana ata rais wa ukrain ameamua kusign na kutuma barua EU kuomba uwanachama kamili maana kwa sasahivi ukrain ni partner wa EU na sio member.

Kukiwa na taarif ya source kamili nitaweka kiongoz!!!
Unadhani EU wanaweza kukubali na kuangia vita na Russia kwa sababu ya Ukraine?
 
Kaka ...

By 02 March 2022..

Rais wa Ukraine atakuwa amekimbia na Ukrane itakuwa imechukuliwa na Urusi...
Hata Putin binafsi alikuwa anatamani iwe hivyo, lakini kwa bahati mbaya mambo yamekwenda ndivyo sivyo akaamua kunyoosha mikono juu.
 
Nakumbuka Gavana wa BoT wakati wa Nyerere mzee Mtei alikuwa akimkatalia Mwalimu mambo mengi kutokana na athari zinazoweza kujitokeza mbeleni lakini wanasiasa wa wakati ule wakamuona Mtei kama mtu mkorofi.

Leo Putin baada ya kubanwa mbavu amemuita faraghani gavana wa Benki kuu wayajenge.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimeona makamanda wachache sana akina Yoda na Jitegemee ndio wanaunga mkono udhalimu unaofanywa na Russia lakini walio wengi wako upande wa Ukraine na washirika wake.

Na kuhusu Lumumba wao wakati wote husimama na wale wanaoonewa yaani upande wa haki.

Hakika, Maendeleo hayana vyama!
Mimi Niko urusi Jo, Kwa kuwa TU hawawapendi wasiojulikana was ulaya na Amerika kwa kivuli Cha nato, unanisemeaje bwana🤔
 
Kwanza kbs napenda kutanguliza salam kwa wana JF wenzangu hapa jukwaani, pili naomba mods msiuunganishe huu uzi na uzi wowote unaohusiana na mambo ya Ukraine maana kila mtu ana uwasilishaji wake wa taarifa hapa jukwaani, so kuuchukua uzi wa mtu ambae kila siku anatumia data zake, muda wake, fikra zake na energy yake kuchangia comment mbali mbali au kuandika thread mbali mbali afu kwenda kuunganisha na uzi wa mtu mungine bila taarifa au sababu za msingi ni kuingilia uhuru wa watu kutoa maoni yao hapa jukwaani. Kwahiyo mwisho wa siku mtajenga hofu na uoga kwa wateja wenu, maana mtu atajua akileta uzi hapa kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusu yanayojiri huko duniani mods watauchukua huo uzi wake na kuupeleka sehem wanayojua wao bila idhini yake ili kupoteza maana ya kile alichoandika hapa jukwaani. So nina imani mods mtazingatia ushauri wang huu niliowapa. Tuje kwenye mada husika. Ndugu zangu kitendo cha raisi wa Russia kuomba poo ya mazungumzo ya kumaliza mapigano kati ya jeshi lake linalosifika kuwa na nguvu zaidi duniani baada ya lile la Marekani, kimewashangaza wengi waliokuwa wakimuunga mkono mbabe huyo na jeshi lake. Wakati akijiandaa na uvamizi, wengi wa wapambe wake walitegemea uvamizi wake ungechukua usiku mmoja tu kumaliza kile alichoita safisha safisha ya viongozi vibaraka wa magharibi. Sasa anashangaa pamoja na ukubwa wa jeshi lake, wingi wa silaha zake, na ukubwa wa nchi yake ameshindwa kutwaa hata miji mitatu tu mikubwa, badala yake yeye ndo amekuwa akirudishwa nyuma na kunyang'anywa mji wa pili kwa ukubwa ambapo hapo awali jeshi lake ndo lilikuwa linaumiliki. Bila shaka Putin ashasoma alama za nyakati baada ya kunusa ule mtego wa Marekani ambao waliutega kwa lengo la kupata sababu ya kuingia kijeshi kuiadhibu Russia kupitia katika ardhi ya Ukraine. Ikumbukwe Marekani na genge lake la NATO walisema hawawezi kuingia vitani kuisadia Ukraine kwani sio mwanachama wao kamili wa NATO. Ila nyuma ya pazia Marekani alikuwa anapanga mpango wa kurushwa kombora moja tu la Russia nchini Poland ambae ni mwanachama wa NATO ili watemi hao wa dunia waweze sasa kuingia kazini live bila kujificha kwa kisingizio kuwa Russia ndio ilianza uchokozi wa kumshambulia mwanachama mwenzao wa NATO (Poland) Silaha kubwa kubwa zimekuwa zikitumwa Ukraine usiku na mchana kwa kisingizio cha kuipa msaada wa silaha Ukraine, kumbe wakubwa hawa wanaziandaa kwa ajili ya kwenda kuzitumia wenyewe hapo baadae baada ya mipango kukamilika. Mimi na wewe hatujui hilo kombora lingerushwaje rushwaje ili mission yao ikamilike kuingia mzigoni. Wangesubiri kombora la Russia likosee njia na kuangukia kwa mwanachama wao? au wale wale askari wa Ukraine wangetafuta njia ya kupata kombora la Russia na kulivugumiza nchi yoyote mwanachama kinyemela ili msala umuangukie Putin? Pongeza kwa Putin kwa kuliona hili mapema na kuwahi kuomba poo before mambo hayajaharibika, maana Mmarekani na genge lake sio watu wazuri hata kidogo. Kweli unaweza kujikakamua kupambana nao lkn mwisho wa siku wewe ndo utaanguka miguu juu. Mungu aepushe mbali vitaa hii, ili dunia iwe sehemu salama ya kuishi kwa amani.

Huu utopolo wote ni paragraph 1 peke yake?
 
MR BEN mambo ya Ukraine ni mbali sana na yamekuzidi kimo sana, pambana na ya bongo kwanza
Nimeona makamanda wachache sana akina Yoda na Jitegemee ndio wanaunga mkono udhalimu unaofanywa na Russia lakini walio wengi wako upande wa Ukraine na washirika wake.

Na kuhusu Lumumba wao wakati wote husimama na wale wanaoonewa yaani upande wa haki.

Hakika, Maendeleo hayana vyama!
 
Wizara ya Nishati imesema kutokana na kupanda kwa bei za mafuta katika Soko la Dunia kunakosababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine, mwenendo wa bei za mafuta nchini umeathirika kwa bei hizo kuendelea kupanda.

Tozo ya Tsh 100 kwa lita kufutwa.

Uzuri mafuta yakipanda ipasavyo, Warusi weusi, Wamarekani wa Tanganyika na wengine wote tunakuwa kitu kimoja kuisoma namba na jina letu la Waathirika wa vita kutoka nchi masikini.
Wizara badla ya kuchukua long-term plan wanadili na short të ambayo Bado haina maana Kwa Sababu Bei zitabaki palepale au zitaongezeka kidgo... Moja ya hatua ni at least aweze kuagiza mafuta ya kutosha hTa ya miezi siita hadi Tisa....badla ya kudill na mia mia
 
Kiukweli sijasoma mpaka mwisho!Nilikuwa naruka Hadi mistari 4 Ili tu nipate picha Kwa ujumla!
WanaJF tujifunze kuandika Kwa namna itakayomvutia msomaji kuendelea kusoma mstari Kwa mstari!Nilichobaini ni kuwa haya maelezo yote yangeweza kuwa ndani ya aya mbili Tena kila Aya isichukue hata mistari 6!
Nikirejea kwenye topic,ni mtizamo wangu kuwa mleta mada hana uhakika na anachokizungumza,kaokoteza habari na kaweka maoni yake zaidi kuliko uhalisia!
 
A
Watanzania bwana kwa kujifanya wajuaji hatujambo!

Kila Mbongo ni Mchambuzi siku hizi. Kuanzia Siasa, Mpira, Kubet, Mapenzi, saikolojia, familia, kila kitu tuu wataalamu!
Acha kuwabana watu wasitoe maoni yao,hivi hujui kwamba kutoa maoni ni haki ya kikatiba?
 
Wizara badla ya kuchukua long-term plan wanadili na short të ambayo Bado haina maana Kwa Sababu Bei zitabaki palepale au zitaongezeka kidgo... Moja ya hatua ni at least aweze kuagiza mafuta ya kutosha hTa ya miezi siita hadi Tisa....badla ya kudill na mia mia
Bajeti boss
 
Uzi wa kijinga hauna mantiki yeyote. Eti putin kaomba poo kwa kipi. Hakuna hata risasi moja iliyorushwa kwenda Russia. Yaan huko mjini Moscow business as usual, watu wanaendelea na maisha kama kawaida. Wakati huku Ukraine either ukimbie nchi au ujifiche kwenye handaki kama panya.
Sasa putin aombe poo kwa kipi?

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
Soma vizuri mkuu, nimekwambia kanusa plan ya Mmarekani na genge lake la NATO. Ikitokea kwa bahati mbaya au kwa kupanga kombora lake moja likaangukia Poland au Lithuania ambao ni wanachama halisi wa NATO, basi Putin na nchi yake watakuwa wakimbizi wa kisiasa huko China. Maana hatoweza kuhimili balaa la hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom