LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Kiufupi Ukraine amisha lost kwa sababu zifuatazo,kwa kuwa yeye ndio kakubali mazungumzo so Odds zipo against yeye.akisema amukubalie Urusi madai Yale maana yake Urusi anaenda kuweka kambi ya jeshi hapo Ukraine na unakuwa mwisho wa USA na NATO-kitu ambacho USA na washirika wake kukibali itakuwa ngumu.
Vilevile,akisema asikubali kunakwenda kuibuka Vita kubwa-maana atapata back up ya NATO&USA-ndio maana Putin Jana alicheza movie ya kimaneno kabla ya Kikao chao cha Leo.

Ukraine kete IPO mkononi make,akubaliane na Urusi vita iishe na NATO wa ondoke forever,au akatae Nchi yake igeuke uwanja wa vita kati ya Urusi&USA.
Chaguo ni lake.

Kachagua vita
 
Nimepata taarifa kikao cha negotion kimeisha huko mpakani mwa Belarus kinachosubiliwa ni nini kilichojiri

View attachment 2134183
Angalia usije ukawa unafuatilia vita kupitia Instagram tena kuna wale wanaitwa Dizzim sijui nini ile account inayopost matako ya kina Nandy. Wale jamaa wananikera sana wanapotosha habari, zimekaa kiudaku
 
Hatareee!...UKWELI NI KUWA MAZUNGUMZO YAMEFELI KWA MAANA MASHARTI ALIYOWEKA PUTIN NI MAZITO PAKIWEMO NA KUSTEP DOWN KWA RAIS HUYU ALIYOPO WA UKRAIN...Hivyo njia pekee ya kujiokoa kwa huyo bwana zelenskyy ni kuandika barua ya kujiunga na EU tu ili awape legitmacy kamili nchi washirika waje kumsaidia hayo mapigano kwakuwa atakuw ni mwanachama mwenzao!
Okey.
Hii source ya habari ninayotazama wanasema terms za mazungumzo hazijawekwa wazi bado. Unaweza nipa Link ya source yako?
 
Silaha za nyuklia za Urusi zina uwezo, nikisoma testing za Soviet Union miaka ile kabla hatuna uhuru kwenye Semipalatinsk test site na baadae kisiwa cha Amchitka unaona hawa watu hadi leo usiwachezee. Walifanya tests zaidi ya 700 kwa ujumla, hawatest warheads tena wana uhakika sana na kazi zao.

Ground nuclear weapons zinaweza haribiwa kabla ya kurushwa hasa hizo zilizopo kwenye silos. Satellites huwa zinazunguka muda wote, umakini porini ambako unaona nguzo za umeme zinaenda ila hakuna makazi na zinaishia sehemu fulani. Pia zinachunguzwa reli na barabara zinazoishia porini. Na kabla ya kufyatua kombora kwenye silo kuna logistics activities zinakuwepo. Kwahiyo inawezekana kuharibu silo kabla haijafyatua kombora. Ndio kazi ya bunker buster

Kwa kuzingatia hili ndio maana Russia ana mobile nuclear missiles kama Topol-M na RS-24 Yars ambalo na leo kafyatua kwenye mazoezi. Hizi zinaendeshwa kwenye malori satellite ikizikuta hapa, nusu saa baadae ziko kwingine. Marekani haina mobile nuclear weapons kwa kuwa doctrine zao hazioni ni vipi Urusi itavuka airspace yao. Marekani hawaamini sana kama Russia anaweza ingia anga lao kizembe ndio maana hawana layeled air defence. Wanazo MIM Patriot na range yake sio kubwa haifiki 200km na short range systems kadhaa. Russia ana long range tatu: S-300, S-400, S-500 inakuja, medium range S-350E na hizi Buk zinazopigwa hovyo na drones hapo Ukraine. Short range ni kina Pantsir na wengine. Hizi zinawekwa kwenye layer kuanzia range kubwa mpaka ndogo.

Kwenye maji uko ndiko silaha za nyuklia zinatisha zaidi. Wote wana submarines zinabeba makombora mengi na hazionekani kiurahisi. Ila kiujumla hizi ni deterrence, ile mnataka kufyatua nyuklia ila mnafikiria hata nyie mtapigwa haijalishi Urusi au Marekani itateketea ila nuclear subs zao ziko baharini. Mnaona au basi tuache.

Russia ana silaha. Ukimvamia kwake ndio anakufundisha adabu
Hayo ma defense systems ni upuuzi usio kuwa na maana..

Hakuna cha kuzuia makombora hapo.
 
Hapa ni kama kijiwe cha kahawa...uongo uongo tu hakuna mwenye habari kamili...much know tu ndio wapo hapa...waombeeni amani maana hamjui kitu
 
Naaam karibu tena tumalizie ungwe ya pili na naona timu zinatoka vyumbani tayari kuanza,bado sijaona mabadiliko hadi sasa ila wachezaji wa timu ya Urusi wanaanza kupasha kwa wingi. Jukwaa la Ukraine lipo na watu wachache waliokaa sehemu moja na huku wengi wa mashabiki hao wakitoka nje ya uwanja.
Satan 2 tutaitumimia dakika za nyongeza inakwenda kumaliza ubishi wote.
 
Hapa ni kama kijiwe cha kahawa...uongo uongo tu hakuna mwenye habari kamili...much know tu ndio wapo hapa...waombeeni amani maana hamjui kitu
True kwa kiasi kikubwa. Ila kuna watu wapo wanaleta sources za uhakika. Kuwaombea amani ni Jambo la maana sana.
 
Mm nipo Ukraine hapa ila kiukweli mji upo kimyaaa ni mwendo wa kuvizia kuiba mikate ule

Screenshot_20220228_203335.jpg


20220228_203316.jpg


20220228_203311.jpg
 
Mazungumzo yalifanyika kwenye mpaka wa Belarus kati ya maafisa wa Urusi na Ukraine.

Ni mara ya kwanza wanakutana tangu Urusi kuvamia, lakini matumaini ya kufanikiwa si makubwa.

Kabla ya mazungumzo hayo, Ukraine ilisema inataka kusitishwa kwa mapigano na Urusi kujiondoa, huku Kremlin ikisema haitatangaza msimamo wake.

Wapatanishi wa Urusi wamezungumza kuhusu makubaliano ambayo yana maslahi ya pande zote mbili.

Ujumbe wa Ukraine unajumuisha Waziri wa Ulinzi Oleksiy Reznikov na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mykola Tochytskyi.

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Alexander Fomin na Balozi wa Urusi nchini Belarus Boris Gryzlov pia ni miongoni mwa waliopo.
 
Russia hawez lolote , kinachokufanya uonekane mbabe ,ni huge backup under fire , kitu ambacho Russia Hana ,na pia kuna different opinion among public , moja ya kitu kibaya mno kwenye vita , ametuaminisha ni mbabe yes tumekubal , but in reality huwez kurun show against European giants +US combined together , hao mnaosema washirika wake hawana chochote new cha kutoa hata wakijoin naye , kwanza hawana hela ,aiseee vita bila hela hamkna kitu , unaweza kujitutumua Kwa mwaka mmoja after that inakuwa ni disaster ...!!! Atakuwa ameishiwa kila kitu huku ukiwa umebanwa na vikwazo
Akili kubwa inajua hilo. Na mipango ilishawekwa na kuandaliwa 30yrs back.
Silaha za vita huandaliwa wakati wa Amani.
So Russia is prepared with .
 
Okey.
Hii source ya habari ninayotazama wanasema terms za mazungumzo hazijawekwa wazi bado. Unaweza nipa Link ya source yako?
Mkuu no officia recognized source on the impact of their talks...hiyo kuna jamaa mmoja mfaransa nilion tu insta kacomment hivyo kwamba inasemekan moja ya maafikiano aliyowek mezan bwana mkubwa putin ni kustep down kwa rais zelenskyy...hivyo kwa hali iliyopo yawezekana ndo ivyo na ata icho kikao cha pili huenda kisizae matunda na ndio maana ata rais wa ukrain ameamua kusign na kutuma barua EU kuomba uwanachama kamili maana kwa sasahivi ukrain ni partner wa EU na sio member.

Kukiwa na taarif ya source kamili nitaweka kiongoz!!!
 
Back
Top Bottom