LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Kwanza kbs napenda kutanguliza salam kwa wana JF wenzangu hapa jukwaani, pili naomba mods msiuunganishe huu uzi na uzi wowote unaohusiana na mambo ya Ukraine maana kila mtu ana uwasilishaji wake wa taarifa hapa jukwaani, so kuuchukua uzi wa mtu ambae kila siku anatumia data zake, muda wake, fikra zake na energy yake kuchangia comment mbali mbali au kuandika thread mbali mbali afu kwenda kuunganisha na uzi wa mtu mungine bila taarifa au sababu za msingi ni kuingilia uhuru wa watu kutoa maoni yao hapa jukwaani. Kwahiyo mwisho wa siku mtajenga hofu na uoga kwa wateja wenu, maana mtu atajua akileta uzi hapa kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusu yanayojiri huko duniani mods watauchukua huo uzi wake na kuupeleka sehem wanayojua wao bila idhini yake ili kupoteza maana ya kile alichoandika hapa jukwaani. So nina imani mods mtazingatia ushauri wang huu niliowapa. Tuje kwenye mada husika. Ndugu zangu kitendo cha raisi wa Russia kuomba poo ya mazungumzo ya kumaliza mapigano kati ya jeshi lake linalosifika kuwa na nguvu zaidi duniani baada ya lile la Marekani, kimewashangaza wengi waliokuwa wakimuunga mkono mbabe huyo na jeshi lake. Wakati akijiandaa na uvamizi, wengi wa wapambe wake walitegemea uvamizi wake ungechukua usiku mmoja tu kumaliza kile alichoita safisha safisha ya viongozi vibaraka wa magharibi. Sasa anashangaa pamoja na ukubwa wa jeshi lake, wingi wa silaha zake, na ukubwa wa nchi yake ameshindwa kutwaa hata miji mitatu tu mikubwa, badala yake yeye ndo amekuwa akirudishwa nyuma na kunyang'anywa mji wa pili kwa ukubwa ambapo hapo awali jeshi lake ndo lilikuwa linaumiliki. Bila shaka Putin ashasoma alama za nyakati baada ya kunusa ule mtego wa Marekani ambao waliutega kwa lengo la kupata sababu ya kuingia kijeshi kuiadhibu Russia kupitia katika ardhi ya Ukraine. Ikumbukwe Marekani na genge lake la NATO walisema hawawezi kuingia vitani kuisadia Ukraine kwani sio mwanachama wao kamili wa NATO. Ila nyuma ya pazia Marekani alikuwa anapanga mpango wa kurushwa kombora moja tu la Russia nchini Poland ambae ni mwanachama wa NATO ili watemi hao wa dunia waweze sasa kuingia kazini live bila kujificha kwa kisingizio kuwa Russia ndio ilianza uchokozi wa kumshambulia mwanachama mwenzao wa NATO (Poland) Silaha kubwa kubwa zimekuwa zikitumwa Ukraine usiku na mchana kwa kisingizio cha kuipa msaada wa silaha Ukraine, kumbe wakubwa hawa wanaziandaa kwa ajili ya kwenda kuzitumia wenyewe hapo baadae baada ya mipango kukamilika. Mimi na wewe hatujui hilo kombora lingerushwaje rushwaje ili mission yao ikamilike kuingia mzigoni. Wangesubiri kombora la Russia likosee njia na kuangukia kwa mwanachama wao? au wale wale askari wa Ukraine wangetafuta njia ya kupata kombora la Russia na kulivugumiza nchi yoyote mwanachama kinyemela ili msala umuangukie Putin? Pongeza kwa Putin kwa kuliona hili mapema na kuwahi kuomba poo before mambo hayajaharibika, maana Mmarekani na genge lake sio watu wazuri hata kidogo. Kweli unaweza kujikakamua kupambana nao lkn mwisho wa siku wewe ndo utaanguka miguu juu. Mungu aepushe mbali vitaa hii, ili dunia iwe sehemu salama ya kuishi kwa amani.
Aliyesoma hii nyaraka isiyo na kiuno, kichwa, kofia wala koma naomba anieleweshe huyu mwameleki anasema nini
 
SmartSelect_20220228-201639_Chrome.jpg
 
Russia imesema kwa muda mrefu haitaki kuona Ukraine yatumiwa kuwa kichaka cha NATO na Marekani.

Kumbuka mafahali wawili huwezi kuwaweka zizi moja.

Russia hataki Marekani asogee karibu kupitia mgongo wa Ukraine.

Ukraine ingeruhusiwa kuingia NATO basi ingepewa Air defence systems za kuzuia mashambulizi ya Russia na Russia ingekuwa haina uwezo wa kuzishambulia nchi zote majirani na ingevamiwa.

Ndo maana Russia ikaiwahi Crimea na sasa yaitaka Ukraine.

Poland, Latvia na Romania ndio majirani pakee ambao Russia hana shida nao kwa upande wao magharibi na kusini magharibi.

Estonia ambako vipo vikosi vya majeshi ya UK na wengine nao Russia hana shida nao.

Russia haitaki kuona NATO na Marekani upande wa mashariki na kusini mashariki hadi bahari nyeusi.
Una uhakika Russia hana mgogoro na Poland?

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Uzi wa kijinga hauna mantiki yeyote. Eti putin kaomba poo kwa kipi. Hakuna hata risasi moja iliyorushwa kwenda Russia. Yaan huko mjini Moscow business as usual, watu wanaendelea na maisha kama kawaida. Wakati huku Ukraine either ukimbie nchi au ujifiche kwenye handaki kama panya.
Sasa putin aombe poo kwa kipi?

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
 
Nawaza tu russia akianza tumie zile bombs zake za nyuklia za ICBM(InterContinental Ballastic-range Missile) asije chochea WWIII...pia ikumbukwe ana best AIR-DEFENCE systems hapo tunazungumzia S200, S300, S400, S500 na S700...hapo ndipo alipo vizuri russia.
Nani kakwambia ICBM ni Neuc Bomb ?

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nina mashaka sana na Russia kuhusu ukweli wa Silaha zake. Ninaona kama Fix hivi. Hii vita ikiendelea halafu NATO waingie unawezakuta hizo silaha alizoaminisha dunia huenda sio za kihiiiivyo. Hata nuclear unawezakuta zipo lakini low grade. Na akicheza hao NATO/USA wanaweza kum surprise wakazipiga hapohapo Russia.

Kuna uwezekano NATO wameshajua uwezo halisi wa RUSSIA na kugundua mbona ANAPIGIKA KIRAHISI TU.
Silaha za nyuklia za Urusi zina uwezo, nikisoma testing za Soviet Union miaka ile kabla hatuna uhuru kwenye Semipalatinsk test site na baadae kisiwa cha Amchitka unaona hawa watu hadi leo usiwachezee. Walifanya tests zaidi ya 700 kwa ujumla, hawatest warheads tena wana uhakika sana na kazi zao.

Ground nuclear weapons zinaweza haribiwa kabla ya kurushwa hasa hizo zilizopo kwenye silos. Satellites huwa zinazunguka muda wote, umakini porini ambako unaona nguzo za umeme zinaenda ila hakuna makazi na zinaishia sehemu fulani. Pia zinachunguzwa reli na barabara zinazoishia porini. Na kabla ya kufyatua kombora kwenye silo kuna logistics activities zinakuwepo. Kwahiyo inawezekana kuharibu silo kabla haijafyatua kombora. Ndio kazi ya bunker buster

Kwa kuzingatia hili ndio maana Russia ana mobile nuclear missiles kama Topol-M na RS-24 Yars ambalo na leo kafyatua kwenye mazoezi. Hizi zinaendeshwa kwenye malori satellite ikizikuta hapa, nusu saa baadae ziko kwingine. Marekani haina mobile nuclear weapons kwa kuwa doctrine zao hazioni ni vipi Urusi itavuka airspace yao. Marekani hawaamini sana kama Russia anaweza ingia anga lao kizembe ndio maana hawana layeled air defence. Wanazo MIM Patriot na range yake sio kubwa haifiki 200km na short range systems kadhaa. Russia ana long range tatu: S-300, S-400, S-500 inakuja, medium range S-350E na hizi Buk zinazopigwa hovyo na drones hapo Ukraine. Short range ni kina Pantsir na wengine. Hizi zinawekwa kwenye layer kuanzia range kubwa mpaka ndogo.

Kwenye maji uko ndiko silaha za nyuklia zinatisha zaidi. Wote wana submarines zinabeba makombora mengi na hazionekani kiurahisi. Ila kiujumla hizi ni deterrence, ile mnataka kufyatua nyuklia ila mnafikiria hata nyie mtapigwa haijalishi Urusi au Marekani itateketea ila nuclear subs zao ziko baharini. Mnaona au basi tuache.

Russia ana silaha. Ukimvamia kwake ndio anakufundisha adabu
 

Hatareee!...UKWELI NI KUWA MAZUNGUMZO YAMEFELI KWA MAANA MASHARTI ALIYOWEKA PUTIN NI MAZITO PAKIWEMO NA KUSTEP DOWN KWA RAIS HUYU ALIYOPO WA UKRAIN...Hivyo njia pekee ya kujiokoa kwa huyo bwana zelenskyy ni kutuma barua ya kuomba kujiunga na EU tu ili awape legitmacy kamili nchi washirika waje kumsaidia hayo mapigano kwakuwa atakuw ni mwanachama mwenzao!
 
Back
Top Bottom