LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Nimekuwa nikifatilia page zake kwa muda sasa na nimejilidhisha kuwa nyingi ni uongo na zinaandikwa kwa mihemko na sio weledi

Mwanakijiji aiba kifaru aisee bro anatulisha matango poli kila siku kuhusu hili jambo dunia imeona kila kitu habari ambayo hutaipata kwingine kitenge atakupa video ya mtoto wa kipalestina akibishana na mwanajeshi wa izrael Leo anatuaminisha kuwa ya Leo kwa warusi najiuluza maslahi yake ni ipi kwenye vita hii

Bro simuelewi kwa kweli
 
Mkuu,huyu hana malezi bora,huwezi kuwa na akili timamamu kwa kutukana na kukejeli kila mtu kisa mnatofautiana ki mtazamo, inatia shaka sana kama kweli alipata malezi bora utotoni. The best way ni kumu ignore tu,watu wana frustration za maisha na mahali pekee pa kutolea stress zao ni hapa,
 
Reactions: Tsh
Yaan nchi moja wafe watu mil 24??
 
Hadi kufikia jioni naamini dakika 90 za mpambano zitakuwa zimeisha na hazitaongezwa dakika 30 wala penalt hatuendi. Putin atamaliza mapema sana mchezo huu. Tit for tat=Vita ni Vita Mura
ha ha ha we jamaa unanifurahisha sana Mkuu, huna stress hata kidogo,muda wote wewe ni full burudani.
 
Russia anasaidiwa na kanchi kadogo?

Ni aibu ya karne!
 
Ni kweli. Kuliko kuparuana nae bora ukamuacha.
 
Hadi kufikia jioni naamini dakika 90 za mpambano zitakuwa zimeisha na hazitaongezwa dakika 30 wala penalt hatuendi. Putin atamaliza mapema sana mchezo huu. Tit for tat=Vita ni Vita Mura
CNN wanasema walidhani ile convoy ni kama KM 4 urefu ila satelite image inaonesha ni zaidi ya 40KM plus hii ni punch kama ni boxing basi mtu anapigwa knockout. Mimi binafsi sina sababu ya kumpenda Russia ila nachochukia hawa jamaa wakianza kampeni zao za media wasichokitaka wao utasema mwisho wa dunia ila haya yangeweza kutokea huku kwetu na uhakika wangetoa maneno tu na kupotezea hawa thamini kabisa watu wengine ila ya kwao wanataka kila mtu aongelee kitu kizuri pekee katika hili hata kelele za Corona wamesahau ghafla na ugonjwa umesahaulika. Hawa jamaa hatari sana nimefurahi tu nchi za Africa kimyaa good wapambane na hali zao.
 
Kuna mchezaji alisukuma paka kwa mguu tu basi utasema karusha bomu la nuclear haikubaliki, afukuzwe, afungwe maneno mpaka unashangaa kwani paka kafa? wao paka kusukumwa ni habari kubwa kuliko mwafrica kufa sasa utakuta huku kwetu mtu I stand for Ukraine.
 
CNN wanasema walidhani ile convoy ni kama KM 4 urefu ila satelite image inaonesha ni zaidi ya 40KM plus hii ni punch kama ni boxing basi mtu anapigwa knockout. Mimi binafsi sina sababu ...
Sasa nchi za Africa zitaongea nini? Katika hili hakuna haja ya kuwa na kiherehere cha kuchagua upande mapema. Unakaa unatazama kwa mbali. 😀
 
Yule paka alipigwa bana. Umeangalia video zote? Kuna moja alitandikwa kofi nyingine buti halafu kuna moja nafikiri ndo unayoisemea ya kumsukuma kwa mguu.
 
Kumbe korona ukishighulika nayo na yenyewe inajishughulisha ila ukiipotezea basi nayo inakupotezea. Kuna siri kubwa sana inaendelea duniani, rotation ya vita magonjwa ni ya kuchungwa sana hapa duniani. Walipoona vita hakuna wakaja na Corona na sasa corona inafifia wamekuja na vita,. Bado nawaza baada ya vita ni kile kirusi kipya cha HIV?
 
Katika hari ya kushangaza dunia Putin amesikika akitangaza kuivamia Ukraine na kusema yeyote atakaye jipendekeza atazaa nae, hivi hiki kibuli ni kweli anacho au biti.

Karibuni maana sielewi.
 
Sasa nchi za Africa zitaongea nini? Katika hili hakuna haja ya kuwa na kiherehere cha kuchagua upande mapema. Unakaa unatazama kwa mbali. 😀
Nimependa hii kuwapotezea tu
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…