Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mkuu mbona umeandika kama unakimbizwa, nimeuliza nisababu zipi zinazo sababisha Biden asikubalike na wamerekani namna hiyo(kwa mjibu wa data za utafiti huo)

Sasa wewe hujataja hata sababu moja badala yake umeishia kurukaruka kama mgonjwa wa tumbo la kuhala.

Jibu swali acha Ramli zisizo kuwa na maana.
 
I second you .... Sky Eclat sikumbuki nimepingana naye kati lipi.... Ila Kuna vitu anavipiga low-profile... Mtu Mmoja anajielewa sana ... Katika jinsia za Ke.... Kongole kwake
Yuko vizuri dada yetu.
Siku zote Yuko upande wa haki.
Sky Eclat hajaharibiwa na propaganda za Hollywood movies na waimbaji kama akina Beyonce.yeye anasimamia haki tu.
 
Ha ha dah, basi sawa mdau. Nikipata wasaa nitafanya hivyo.
 
Safi sana maelezo murua kabisa yaliyoambatana na ujumbe ule ule kwa lugha ya picha, yani hata wadau wa kuelewa kwa kutazama picha naamini wamakuelewa vizuri.

Tuendelee na moyo huu huu wa kujitoa kwajili ya waliyo tayari kujifunza na kuelewa mkuu kama sisi tulivyo tayari kujifunza na kuelewa kwa tusivyovifahamu kutoka kwa wanavyo vifahamu.
 
Mi nakuambia utapingwa TU.
We subiri.
 
Tuendelee na moyo huu huu wa kujitoa kwajili ya waliyo tayari kujifunza na kuelewa mkuu kama sisi tulivyo tayari kujifunza na kuelewa kwa tusivyovifahamu kutoka kwa wanavyo vifahamu.
Umenena kweli mdau, hio ndio sifa kuu ya mtu mwelevu. Tunafaham yale tunayoyajua sio kila kitu na kila wakati tupo huru kujifunza lipya hata kama linakinzana na kile ambacho tumekwisha jua habari yake.

Ukweli ndio una matter, na kuna njia za kuutambua ukweli kwenye "lundo" la taarifa. Na maadam vigezo vya taarifa kuitwa ukweli viko assured. We aren't dumb to deny the Truth.

Pa1 sana mdau wa Nguvu!
 
Hap Ukraine alipiga bomu mochwari kwa kuwa urusi aliviacha hivi vifaru vitupu kwa kuwa vilikuwa immobile

Haijalishi chochote mtakacho jiliwaza nacho, ila Kyev iligoma kukamatika, mliangukia pua, Zelensky mliyempa masaa 24 aachie ngazi au aikimbie nchi, leo hii bado ndiye rais.
 
Sana, Sky Eclat na ngaboru kama mmoja wapo ni mkeo, Hata zile nguvu za kusema ngoja nikajadiliane na mama flan hivi na vile unakua nazo!

Kwasababu unaamini wakifunguwa vinywa kuna kitu unakipata πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Yes ni kweli,
Ngaboru sikua namfahamu kabla,ukweli nimemfahamu kwenye thread hii,kwanza nilikua najua ni me,lkni kumbe ni ke,Hadi pale alipomuelewesha mdau mmoja ama wewe au mwingine kuwa yeye ni ke.
Lkini nilishaukubali mziki wake mapema sana,nilishaaga sana kua ngaboru ni ke,maana nondo,na uelewa wake uko juu sana.
Ila huyu Sky Eclat yeye nadhani tunafahamiana,Huwa tunapambana wote dhidi ya uonevu fulanifulani kwenye jukwaa la siasa.Yuko vizuri mno.
Hebu Sasa niambie Yu wapi moendwa wetu Joanna?
Au hata Victorie?
Nilijribu sana kumuelewesha Joanna kua Putin sio mtu mbaya na Urusi ni taifa la kiungwana sana ,Kuna mdau humu akaniambia huyo unatumia na kupoteza nguvu zako Bure TU.
Nulimwelewesha jinsi NATO na USA walivyo wabinafsi hawataki Russia karibu na USA lakini wao kutwa kuisogelea urusi.na Urusi ameisigi NATO mda mrefu sana isiendelee kujitanua kuelekea east lknwakampuuza mwamba wa Moscow.
Akachora mstari mwekundu,wakivuka a TU.,wamevuka na Sasa analala nao sambamba.
Joanna na wenzake hawakuelewa lkn Sky hii mambo naona anaijua au amaeilewa haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…