Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Toa sudan ni weusi kama mkaa
 
Mkuu ni vigumu kidogo kuamini habari hii. Hadi sasa Urusi imeshindwa kudhibiti anga juu ya Ukraine. Yaani wanatumia ndege zao mpakani tu penginepo wanarusha makombora kutoka mbali. Kwa njia hii walishindwa kutawala anga na hivyo tunaona utalii wa kisiasa wa maraisi wa Ulaya kutembelea Kyiv mara kwa mara. Ambayo isingewezekana kama Urusi ingetawala anga.

Sasa tunatakiwa kuamini kwamba inaweza kudhibiti anga juu ya nchi ya NATO?` Wafanye nini? Kuangusha ndege juu ya Lithuania?
 
Key statements by NATO Secretary General Jens Stoltenberg:

The price of Russia's victory in Ukraine for NATO will be higher than providing support to Kiev for a long time.;

The NATO summit in Madrid will adopt a new strategic concept, which will call Russia the "most significant and direct threat to the security" of the alliance;

*NATO is in constant contact with Lithuania on the situation around Kaliningrad, believes that it "only applies EU sanctions."
 
Mzee unalinganisha Ukraine na Lithuania!?
1. Lithuania ni ndogo sana.
2. Lithuania ipo njiani mwa Russia kuelekea kwenye jimbo lake.
3. Ukraine ni kuuuuuuubwa ukilingamisha na Lithuania.
4. Sijakuelea unaposema ni ngumu. Tayari S-400 nimeonekana Belarus zikielekea mpakani mwa Lithuania na Belarus.
 
Sawa, zielekee tu. Baada ya kufika zifanye nini? - Pamoja na hayo: je Belarus itakubali kushambulia nchi nyingine kutoka ardhi yake? Hasi sasa mtawala wake hakutuma wanajeshi Ukraine . . .
 
Social Revolutionaries submitted to the State Duma a draft law on simplified acquisition of Russian citizenship for citizens of Latvia, Lithuania and Estonia
Cha kwanza asante sanaa kwa kufanya huu uzi uwe hai nakuappriciate endelea kufanya ufanyacho.

Aiseeee Russia wanakusanya majimbo yao mmamaaee haaa
Mi napenda undava wao sanaa,hiki kizazi kilichopo madarakani ni cream ya binadamu kifupi sina cha kuongeza.
 
Sawa, zielekee tu. Baada ya kufika zifanye nini? - Pamoja na hayo: je Belarus itakubali kushambulia nchi nyingine kutoka ardhi yake? Hasi sasa mtawala wake hakutuma wanajeshi Ukraine . . .
Yaani we jamaa sijui tujadili. Au sijui nifanye nini tu. Nashindwa kukujibu. Maana unaonekana hata Geopolitics hujui.
Belarus na Russia ni kama chanda na pete. Lao ni moja.

Pili tunaongelea Air Defense system. Hiyo S-400 ni air defense system. Maana yake anga la Lithuania litakuwa chini ya uangalizi wa Russia.

Hivi unaujua mgogoro uliopo kati ya Lithuania na Russia!?
Tuanze kwaza hapo.
 
Sio east Africa tu... Kipindi flani Uganda ilikuwa juu kabisa kwenye ubora jeshi la anga Africa nyuma ya Algeria
 
Sawa, zielekee tu. Baada ya kufika zifanye nini? - Pamoja na hayo: je Belarus itakubali kushambulia nchi nyingine kutoka ardhi yake? Hasi sasa mtawala wake hakutuma wanajeshi Ukraine . . .
Your browser is not able to display this video.


⚔️⚔️⚔️S-400 was spotted in Belarus with a V marker⚔️⚔️⚔️
 
Sawa tu, Mkuu! Nimekuuliza roketi hizo za S-400 zifanye nini baada ya kufika Belarus karibu na Lithuania? Nimeelewa kwamba wangeweza kuangusha ndege juu ya Lithuania. Ila siamini kwamba wataifanya. Maana kurusha roketi ndani ya nchi ya NATO ni sawa na kushambulia NATO. Kwa hiyo naona Warudi wanataka kutishatisha tu kidogo ila hawawezi kufanya kitu. Au machoni pako wangefanya nini?
 
Unadhani Russia anaogopa NATO. Mpaka sasa hivi huko Ukraine anapigana na NATO lakini wamefanya nini mzee!?

Hivi unaichukulia Russia kama Kenya siyo. Hapo imepelekwa Air Defense System. Hivi unajua maana yake!?

Kwanza nimekuuliza swali unajua mgogoro wa Lithuania na Russia!?
 
Swadakta mdau, anyway ngoja niseme kitu kingine na leo...

Ukirejea kwenye history ya darasani, inasema waarab waliingia Afrika karne ya 7, mabeberu haya yakaja Afrika karne ya 18, baada ya mapinduzi ya viwanda.

Wakati wanakuja Afrika walikuja na ujio wa Dini, Missionary activities... Hapa kwa mtu mwenye akili kuna jambo au mambo ya kujiuliza na kuyatafutia majibu.

Kama lengo la beberu lilikuwa ni kutawala, swali ikawaje au alifikiria nini kuleta ujio wa dini kama mwanzo wa kuweka utawala wake. Jibu la haraka haraka litakuwa "Divide and Rule", Ingawa ukipanua wigo wa mawazo ni zaidi ya hilo.

Kuna weakness flan tupo nayo sie watu weusi, hatuna kitu inaitwa "kiasi" katika mambo yetu. Kila kitu huwa tunafanya "kupitiliza"... Yah I mean tuna "extremism" ya hali ya juu.

Tukipenda basi tunapenda kupindukia, na tukichukia tunachukia kupindukia. Hatuna kiasi katika upendo au chuki. Huu ni udhaifu mmoja mbaaaya sana... tena mbaya mno.

Udhaifu huo uko hivi, unapopenda au kuchukia kupita kiasi unaondoa normal decisive power uliyonayo. So unafanya na kuamua kwa mahaba endapo umependa au kwa chuki kama hujapenda... Always unakuwa nje ya uhalisia. Hii ni kwa mujibu wa saikolojia.

Kwa kulijua hilo, ikawa ndio mission yao ya kwanza Afrika, I think that's why wakaitwa Missionaries... Ha ha yani wazee wa Mishe mishe 😂 (kidding), their key Job ikawa ni kujaza upendo kuhusu wao kwenye nyoyo za watu weusi.

Na kwasababu mtu mweusi hana kiasi, akauvaa ule upendo utosini hadi kwenye unyayo, so ile decisive power ikafa. Then ikawa kila kitu sawa, yani sawa sawaaa.

Naam mababu zetu wakachumbiwa namna hiyo.

Tuendelee...

Ni kama leo, upate pesa... Kesho uzikose useme huzitaki tena huo ni uongo. Baada ya watu weusi kupewa "Uhuru" wao. Hawakuishia hapo, bado ile kiu ya utawala ipo, na itaendelea kuwepo unless itokee siku tuamke kwenye huu usingizi tuliolala ulojaa wingi wa ndoto nyevu.

Uki-refer kwenye hii Raman, utaona miaka ya nyuma hapo wengi tukiwa hatujazaliwa, Power ya Dunia ilikuwa wapi. Wakina nani walijipa mamlaka ya kutawala kila pembe duniani.


Tusijisahau nyie, Madaraka matam, na kiu ya madaraka huwa haikatiki. Bado wana ham na wanafanya juhudi ya kila hali kuendelea kuyamiliki madaraka hayo!

Huezi kumtawala kijinga mtu mwenye akili timam, lazima umpumbaze mithili ya msukule ili aweze kutawalika. Na hiki ndicho walichofanikiwa kwa kiasi kikubwa through mind controlling tool maarufu kama Media.

Kulieleza hili maelezo yangu yatajikita afrika tu.

Ili ukoloni wa nyuma ya pazia uendelee kuwepo wanahitaji kuwe na wapumbafu wengi zaidi Afrika. Wakijaa makatwente wengi mithili ya MK254 na kundi lake kila Order itakayotoka itapokelewa kwa mikono miwili.

Na kwasababu sie watu weusi hatuna kiasi, show ikaanza kwa kuletewa tamaduni ambazo si za kwetu, hii ni kubadilishwa asili yetu na kupewa asili ya kigeni. Ambayo ni Tattoo ya Utumwa.

Wakaikamata na kuicontrol mifumo yetu ya elim. Yote tunacopy kutoka kwao, na tunacopy old fashioned system ambayo ukiileta kwenye hii dunia iliyochangamka inakuwa Useless.

Zikaboreshwa starehe, Media zao zikaplay part kubwa kwenye hili. Leo hii kizazi chetu cha 1990+ kinataman kua kam Jay Z na Beyonce. Kile bata kwa wingi kama Lil Wiz. Ila sio kesho au keshokutwa kitafanya nini..

Ukirejea tena the fact kua sie huwa ni wazee wa kupindukia. Leo African tunaongoza kwa kupenda starehe kuliko Bara lolote duniani.

So wakati tuko busy kuwaza Pombe na ufuska, wao wako busy kuimarisha Control yao dhidi yetu.

Africa tunachaguliwa wa kumpenda na wa kumchukia, hatuna "taste" yetu. Shubir ikiitwa Asali tunaitikia, na Sukari ikiitwa mwarobaini tunaitikia, Bado hapa napo katika mapenzi na chuki hatuna Chujio.

Wameinajisi mashariki ya kati kwa kuwaita Magaidi, wao wako hapo wanachimba mafuta wanapeleka kwao. Sometimes wanatuuzia na sie huku. Lakini ukichunguza kelele za Ugaidi zimeanza kipindi kipi? Zimeanza US alivyojipenyeza hapo Mashariki ya kati.

Kwa kua sie tumepandikizwa chuki, hatuna mahusiano na hizo nchi ya kueleweka. Nitoe mfano wa UAE, ni Nchi hiyo ina waarab wa asili kama 11% ya population nzima.

Wengine waliobaki zaidi ya 88% ni wageni, wengi wakiwa kutoka mataifa hayo hayo yanayowaita magaidi huku Africa tukipeleka wafanyakazi wa ndani tu hawa dada zetu.

Na sio UAE pekee, Qatar, Kuwait, Jordan n.k kumejaa expats wengi kuliko raia, sasa kama nchi za kigaidi wanaenda kulundikana huko kutafuta nini? Hilo nalo hatushtuki?

Sio hivyo tu, below ni list of countries with highest technology kwa ujumla... Hii list haijatolewa na Mchina wala Mrusi, imetolewa na jarida la USNews na wenzie.


Kwenye top 10, utaziona Russia na China. Ila hizi nchi zinachafuliwa na hao hao ambao pia wamejazana kwenye hizo nchi na kufanya nao biashara.

Weusi desturi yetu ni kuchukia kupindukia au kupenda kupindukia, wakisema China ama Russia mbaya basi tunajitenga nao mazima. Ila wao wanafanya biashara na hizo nchi kwa kiasi kiiiiiikubwa sana.

China kama mfano wa kuigwa, hajafika hapo leo alipofika bahati mbaya, wana kitu hii inaitwa "Yin Yang", ni Philosophical Concept ambayo inaelezea how obviously opposite au contrary forces may actually be complementary, interconnected, and interdependent in the natural world, and how they may give rise to each other as they interrelate to one another.


Damn! Hiyo picha najua sio ngeni kwenu, We need to know how tunaweza ku'control chuki na mahaba ili kurejesha decisive power yetu iliyopotea. Tunatakiwa tuweze kua in charge ya kile kinachoingia kwenye milango yetu ya faham, macho na masikio ili Ubongo utoe maamuzi yenye tija.

Ikirudi itatuwezesha rasm kujua aliye mzuri kwetu ni nani na aliye mbaya kwetu ni nani bila chuki wala mahaba ya kupitiliza.

Inabidi ifike hatua walau tuamke tushtuke tujiongeze na tuamue.

Hili gazeti so poa, ila nawakumbusha tu kiroho safi. Katika nchi zinazoongoza kwa kua na rasilimali nyingi duniani ni hizi.


Out of hizi top 10
1. Canada na Australia zipo chini ya Familia moja ya Malkia Elizabeth. Je Hujiulizi how na kwanini familia hii iendelee kumiliki kiasi hicho bila bughdha?

2. Ukitoa hizo nchi 2, Canada na Australia ukaongeza na Saudia kibaraka wa US... Waliobaki wote wana ugonvi dhidi ya US, sio kwamba wao waanzisha Ugonvi dhidi ya US, bali US amekua akisaka Control kwenye nchi hizo kwa mwamvuli wa Ugashocracy a.k.a Democracy.

My people hivi mnafikiri ni usalama wa dunia ndio unapambaniwa? Laa hasha!

Of course jibu ni sio, bali kinachopambaniwa ni World total Control, maarufu kama NWO.

I may be the youngest of oll here, ila nikiwatizama baadhi hasa pro-west mnadhihirisha kabisa kua Umri ni number tu. Kwamba hata Punguani huwa anazeeka.

Aseee Nimeongea mengi babeki ila mkiniona chizi baridi... endeleeni kulala mie mbu wamening'ata sana usingizi umekata!
 

Aiseee hivi akili yako ipo sawa?? Unaifuatilia hii operation toka inaanza au umevamia uzi??
 
Aiseee hivi akili yako ipo sawa?? Unaifuatilia hii operation toka inaanza au umevamia uzi??
Mkuu nafuatilia habari tu. Najitahidi kuangalia habari kutoka kila upande bila ubaguzi. Lithuania inatekeleza sasa maazimio ya Umoja wa Ulaya kutoruhusu bidhaa kadhaa za Urusi kwenye eneo lake. Hivyo hazipitii tena kwenye reli inayopita katika Lithuania hadi Kaliningrad.
Naona kwamba Urusi imetisha mara kadhaa hatua kali (na kuonyesha picha za roketi zinazoenda hapa na pale) dhidi ya nchi zinazotuma silaha Ukraine. Nisipokosei hadi sasa hakuna kilichofuata.
Kwa hiyo nimekuuliza: roketi hizo zenye muziki mbaya zifanye nini zikifika karibu na Lithuania na eneo la NATO???
 
Mzee nadhani huelewi hata kinachoendelea huko NATO vs Russia.
Russia aliwaambia wakituma silaha inayoweza kufika ndani ya Russia ataweza kulipua ilikotoka. Ni kuulize silaha gani na ya nchi gani imetumwa yenye uwezo wa kupiga ndani ya Russia!?

Jibu swali usinichoshe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…