Nadhani propaganda imekukamata na unakuja hapa nakuamini kabisa hizo story. Vita unashinda lakini lazima hasara upate ni kawaida tu. Kumbuka Russia waliwasaidia Europe kuwatoa Hitler hao England na France walikuwa maji shingoni na zawadi yake kuchukuwa East Germany nadhani kasome history.
Karudi kwenye historia yako. Watu kama nyie mnakera sana, yani unadai nisome historia na wewe uliyeisoma unapotosha. Wapi ambapo Russia au USSR aliikomboa England (ambayo sio hiyo, unamaanisha Great Britain or United Kingdom kama umejumuisha Northern Ireland). Hakuna mwanahistoria hata awe anapata zero darasani ataiita GB au UK eti England, huu sio mpira wa FIFA.
At least ukiniambia USA au British waliikomboa Europe nakusikiliza. The British empire na commonwealth zilitangaza vita mwaka 1939 pale Hitler alipoivamia Poland. Hitler hakuwa ametangaza kuivamia Britain mpaka alipovamiwa nao. Hitler alikuwa anashawishiana na Britain iungane na Ujerumani ili baadae aigeuke. Britain siku zote wako next level kwenye matumizi ya akili wao ndio walifanya declaration of war dhidi ya Nazi Germany na wakaiambia.
On the other hand, USSR chini ya Stalin Ilikuwa na mkataba na Ujerumani ulioitwa Molotov-Ribbentrop Pact wa mwaka 1939. Vyacheslav Molotov huyu huyu wa Molotov cocktails alikuwa Foreign Minister wa USSR. Hiyo non-aggression pact ilisema wasiingizane vitani. Germany ikapiga Poland KWA KUSHIRIKIANA na USSR, USSR walidai eti wanaisaidia hii Ukraine na Belarus eti walikuwa wanaonewa na Poland. USSR iliua maofisa wa Poland maelfu wa kijeshi kwenye Katyn masacre ambapo maofisa wa kijeshi na wanausalama 22,000 waliuwawa na USSR.
Britain ikatangaza vita dhidi ya Germany. Germany ikapiga France kwa kuwa Britain iko karibu nao basi watatumia Ufaransa watume ndege zao na meli kuvamia Uingereza.
Ufaransa ikaanguka kwa haraka hata mwezi haikukaa, walikuwa na maofisa wajinga sana hasa ndio tatizo. Uingereza ikawa yenyewe tu hapo Ujerumani ina Italy kwa Mussolin. Mwaka 1941 Hitler akaona Uingereza haijajipanga sana na haiwezekani ijipange akaamua aivamie USSR kwa haraka, hapo ni baada ya USSR kuonesha udhaifu ilipovamia Finland wabishi sana hawa. USSR iliamini mkataba ule na ikashtukizwa. Marekani kutokana na Pearl Harbor attack ndio akatoa supplies na nguvu dhidi ya Ujerumani.
Nimezunguka sana kukwambia hivi: Russia/USSR hakuisaidia Europe, alijitetea mwenyewe maana mwanzo tu alikuwa ashakubaliana na Ujerumani. Kama Hitler angesikiliza majenerali wake asingevamia two fronts at the same time na Russia isingepigana kukomboa Ulaya. USSR asingepigana na Ujerumani angepotezwa, walifikia hatua ya kubakiza 20km kuifikia Moscow, walipigana battles kama Stalingrad na Kursk mamilioni ya vifo yakatokea.
Na hatua ya mwisho kulikuwa na scramble nani afike Berlin wa kwanza aitwae nchi. Washindi waligawana nusu ya Ujerumani kisa hawakuwa wanaaminiana hata pale Yalta conference. USSR iliitaka Kaliningrad enclave kwa sababu hizi hizi za kushtukiana. Wote walikuwa washajipanga kwa possibility ya kuendelea na vita nyingine baada ya Ujerumani.