LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
The Russian army occupied the city of Vasilyevka in the Zaporozhye region

Jana nimesoma analysis fulani nikaja na conclusion kwamba Ukraine imepewa Su-25 na Mig-29 za NATO lakini ni sawa na kusema zitakuwa na matokeo madogo. Haziendani na za Ukraine.

Kwanza hazina Identification of Friend or Foe (IFF) au labda waliziweka haraka na kufunga systems mpya. Ukraine ina jeshi tofauti na Poland au Moldova, hawawezi kuwa na IFF sawa. Hizo MANPADS wanazopewa hovyo zinaenda kutumika dhidi ya ndege zinazofanana, wote Ru na Ukr wana Su-25 na Mig-29. Ndege kadhaa za Ukraine zishapotea kwa friendly fire.
Pia hazina level moja ya modifications, zitachanganya marubani ambao hawajazoea. Tukumbuke zimetengenezwa miaka 40 uko iliyopita na zinaletwa kutoka nchi tofauti. Systems zake kama za communication na jamming ni tofauti. Ni vigumu kumpa rubani ndege ukamuelekeza kwa siku chache au wiki ukampa afanye vizuri kwenye battle eti kisa ile airframe alikuwa anaitumia. Airframe haibadiliki ila systems ndio zitatoa guarantee ya ushindi.

Airbases za Ukraine upande wa mapigano ziko under surveillance ya Russia. Ikitokea ndege zinatua basi makombora ya Urusi yatadondoshwa hapo. Hii imefanya Ukraine wafiche ndege zao kwenye airstrips badala ya airbases. Uzuri ndege hizi ni za watu wasiojali zinaweza ruka hata kwenye kiwanja cha nyasi hasa hizi Mig-25. Taiwan wenyewe walifikia hatua ya kujenga highways zenye viwango vya rami ya airbase. Mfano sisi hapa tuchukue barabara ya Mbezi ikitokea vita iweze kutumika kutua na kurusha ndege vita.

Ukraine haina ground control radars za kutosha kufanya communication kwa attack jets zao. Huwezi tuma ndege angani kisa kuna adui umemuona la sivyo unajifanya ndege yako iwe soft target, ndege zenyewe hazijitoshelezi sio air superiority fighters zinategemea kuwa fed na ground radars. S-300 za Ukraine bado zinafanya kazi upande wa Magharibi na Kusini ndio maana ndege zao zinaruka uko ila kwingine Russia ana complete air dominance.

Electronic countermeasures za Russia zitasumbua ndege za Ukraine ambazo sio advanced kwenye sekta hiyo. Na ikizidiwa sana Russia ina option ya kuleta ndege nyingine advanced.
Kwenye hili tuseme EU wamefanya kitu inaitwa "let us do anything" kwanza ndege zenyewe zishafikia mwisho wa matumizi. Kuhusu anti tank missiles hizo ni game chager
 
The Italian Visa Application Center in Russia has announced that it has started accepting documents for tourist visas since March 1

Source: TASS
SmartSelect_20220301-220358_Gallery.jpg
 
kamdanganye shangazi yako wa buza distance ya kutoka urusi mpaka ukraine ni 4681km ni sawa na 2909miles kwa ndege yenye speed ya 560miles per hr ni masaa 5 na kitu usichokijua vita sio washirika wala propaganda vita ni vitu vikuu vitatu tu 1)uchumi 2)intelejensia na 3)teknolojia ukiwa vizuri kwenye haya maeneo ma3 hakuna kenge anayeweza kukugusa hapa duniani urusi hana kimoja tu hapo uchumi mzuri na urusi hana uchumi mzuri ukimlinganisha na mataifa makubwa km usa,france,uk,china etc na sio panya kama ukraine nchi inayozalisha mafuta inawezaje kukosa lita 50 za kuweka kwenye kifaru? ndege na makombora ya japan yanawezaje kutoboa mbele ya s-300 s-500 s-700
Are you serious unaamini hizi propaganda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nimesoma analysis fulani nikaja na conclusion kwamba Ukraine imepewa Su-25 na Mig-29 za NATO lakini ni sawa na kusema zitakuwa na matokeo madogo. Haziendani na za Ukraine.

Kwanza hazina Identification of Friend or Foe (IFF) au labda waliziweka haraka na kufunga systems mpya. Ukraine ina jeshi tofauti na Poland au Moldova, hawawezi kuwa na IFF sawa. Hizo MANPADS wanazopewa hovyo zinaenda kutumika dhidi ya ndege zinazofanana, wote Ru na Ukr wana Su-25 na Mig-29. Ndege kadhaa za Ukraine zishapotea kwa friendly fire.
Pia hazina level moja ya modifications, zitachanganya marubani ambao hawajazoea. Tukumbuke zimetengenezwa miaka 40 uko iliyopita na zinaletwa kutoka nchi tofauti. Systems zake kama za communication na jamming ni tofauti. Ni vigumu kumpa rubani ndege ukamuelekeza kwa siku chache au wiki ukampa afanye vizuri kwenye battle eti kisa ile airframe alikuwa anaitumia. Airframe haibadiliki ila systems ndio zitatoa guarantee ya ushindi.

Airbases za Ukraine upande wa mapigano ziko under surveillance ya Russia. Ikitokea ndege zinatua basi makombora ya Urusi yatadondoshwa hapo. Hii imefanya Ukraine wafiche ndege zao kwenye airstrips badala ya airbases. Uzuri ndege hizi ni za watu wasiojali zinaweza ruka hata kwenye kiwanja cha nyasi hasa hizi Mig-25. Taiwan wenyewe walifikia hatua ya kujenga highways zenye viwango vya rami ya airbase. Mfano sisi hapa tuchukue barabara ya Mbezi ikitokea vita iweze kutumika kutua na kurusha ndege vita.

Ukraine haina ground control radars za kutosha kufanya communication kwa attack jets zao. Huwezi tuma ndege angani kisa kuna adui umemuona la sivyo unajifanya ndege yako iwe soft target, ndege zenyewe hazijitoshelezi sio air superiority fighters zinategemea kuwa fed na ground radars. S-300 za Ukraine bado zinafanya kazi upande wa Magharibi na Kusini ndio maana ndege zao zinaruka uko ila kwingine Russia ana complete air dominance.

Electronic countermeasures za Russia zitasumbua ndege za Ukraine ambazo sio advanced kwenye sekta hiyo. Na ikizidiwa sana Russia ina option ya kuleta ndege nyingine advanced.
Kwenye hili tuseme EU wamefanya kitu inaitwa "let us do anything" kwanza ndege zenyewe zishafikia mwisho wa matumizi. Kuhusu anti tank missiles hizo ni game chager
Ni sawa unamuambia jiran yako akupe Chakula ule, anakupa bigijii utafune.

Ni mzaha wa Karne kutumia ndege zenye teknolojia ya kizamanu dhidi ya Russia ya Sasa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaifanyaje nchi iliyo huru na matakwa yake? ivi Tz ikianzisha uhusiano na oman nani atainua mdomo, China nani ataiunua mdomo, korea nk., nchi huru haziingiliwi siasa zake, Ukrain ni nchi huru tunapaswa kulaani mauaji ya kinyama kutoka russia kwa taifa dogo kivita kama Ukrain
Palestina je?
Anapoingiliwa na Israel kila Siku na kuua watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo Putin ajue western countries ndo wanarun dunia kiuchumi, kijeshi na ndo maana kiurusi hata top ten ya nchi zenye GDP kubwa hakipo, na bado atabanwa kende mpaka maji aite mma na muhogo aite mhoho. Mabepari achana nao ndo maana china waliona ni upumbavu kuendelea na sera za ujamaa maana hazilipi wakaingia kwenye ubepari mazima matokeo yake leo hii China yupo namba mbili kiuchumi. Na china kwenye sakata hili haongei sana maana hataki kumuuzi sana US na wenzie maana anakumbuka kichapo cha kiuchumi alichopewa juzi kati ndo maana anaenda aste aste.
We boya unasifia watu ambao hawakupendi wanakuona nyani
 
Tunatamani dunia isio na mapigano ya aina yoyote, lakini kwa sababu ya maslahi binafsi ya taifa hili na lile ndipo kunapotokea mambo kama haya.

Siku moja amani ya jumla itapatikana.
 
Nadhani propaganda imekukamata na unakuja hapa nakuamini kabisa hizo story. Vita unashinda lakini lazima hasara upate ni kawaida tu. Kumbuka Russia waliwasaidia Europe kuwatoa Hitler hao England na France walikuwa maji shingoni na zawadi yake kuchukuwa East Germany nadhani kasome history.
Karudi kwenye historia yako. Watu kama nyie mnakera sana, yani unadai nisome historia na wewe uliyeisoma unapotosha. Wapi ambapo Russia au USSR aliikomboa England (ambayo sio hiyo, unamaanisha Great Britain or United Kingdom kama umejumuisha Northern Ireland). Hakuna mwanahistoria hata awe anapata zero darasani ataiita GB au UK eti England, huu sio mpira wa FIFA.

At least ukiniambia USA au British waliikomboa Europe nakusikiliza. The British empire na commonwealth zilitangaza vita mwaka 1939 pale Hitler alipoivamia Poland. Hitler hakuwa ametangaza kuivamia Britain mpaka alipovamiwa nao. Hitler alikuwa anashawishiana na Britain iungane na Ujerumani ili baadae aigeuke. Britain siku zote wako next level kwenye matumizi ya akili wao ndio walifanya declaration of war dhidi ya Nazi Germany na wakaiambia.

On the other hand, USSR chini ya Stalin Ilikuwa na mkataba na Ujerumani ulioitwa Molotov-Ribbentrop Pact wa mwaka 1939. Vyacheslav Molotov huyu huyu wa Molotov cocktails alikuwa Foreign Minister wa USSR. Hiyo non-aggression pact ilisema wasiingizane vitani. Germany ikapiga Poland KWA KUSHIRIKIANA na USSR, USSR walidai eti wanaisaidia hii Ukraine na Belarus eti walikuwa wanaonewa na Poland. USSR iliua maofisa wa Poland maelfu wa kijeshi kwenye Katyn masacre ambapo maofisa wa kijeshi na wanausalama 22,000 waliuwawa na USSR.
Britain ikatangaza vita dhidi ya Germany. Germany ikapiga France kwa kuwa Britain iko karibu nao basi watatumia Ufaransa watume ndege zao na meli kuvamia Uingereza.

Ufaransa ikaanguka kwa haraka hata mwezi haikukaa, walikuwa na maofisa wajinga sana hasa ndio tatizo. Uingereza ikawa yenyewe tu hapo Ujerumani ina Italy kwa Mussolin. Mwaka 1941 Hitler akaona Uingereza haijajipanga sana na haiwezekani ijipange akaamua aivamie USSR kwa haraka, hapo ni baada ya USSR kuonesha udhaifu ilipovamia Finland wabishi sana hawa. USSR iliamini mkataba ule na ikashtukizwa. Marekani kutokana na Pearl Harbor attack ndio akatoa supplies na nguvu dhidi ya Ujerumani.

Nimezunguka sana kukwambia hivi: Russia/USSR hakuisaidia Europe, alijitetea mwenyewe maana mwanzo tu alikuwa ashakubaliana na Ujerumani. Kama Hitler angesikiliza majenerali wake asingevamia two fronts at the same time na Russia isingepigana kukomboa Ulaya. USSR asingepigana na Ujerumani angepotezwa, walifikia hatua ya kubakiza 20km kuifikia Moscow, walipigana battles kama Stalingrad na Kursk mamilioni ya vifo yakatokea.

Na hatua ya mwisho kulikuwa na scramble nani afike Berlin wa kwanza aitwae nchi. Washindi waligawana nusu ya Ujerumani kisa hawakuwa wanaaminiana hata pale Yalta conference. USSR iliitaka Kaliningrad enclave kwa sababu hizi hizi za kushtukiana. Wote walikuwa washajipanga kwa possibility ya kuendelea na vita nyingine baada ya Ujerumani.
 
Leo huko Uk kumeiva kuna wachezaji wa Ukraine Man city, Westham na Everton wametoa matusi makali juu ya wachezaji wa Russia ambao hawana lolote juu ya haya inabidi wakae kimya, ila watu huko huko UK wamewatolea uvivu waache kelele too much kama wanataka waende kwao kupigania nchi yao. Nadhani EPL wamejiingiza katika shimo la siasa hata FIFA mambo ya michezo ya nini siasa hata nchi ya Kenya wawafungulie tu maana siasa zinakubaliwa rasmi.
 
Assault on Mariupol
SHAMBULIO HUKO MARIUPOL
 
Back
Top Bottom