Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mzee kuhusu mambo ya technology ya Russia nadhani USA wanaweza kuliongelea vizuri hilo jambo ngoja nikurudishe miaka ya nyuma kidogo nikupe mfano halisi.

April 10, 2014 US navy destroyer USS Donald Cook (DDG-75) iliingia kwenye black sea near Russia's territorial water.

Hii USS Donald Cook haikua ya "kitoto" ilikua ni 4th generation guided missile destroyer ambapo ilikua inabeba Tomahawk cruise missile zilizokua na range upto 2,500 kms na uwezo wa kubeba nuclear explosives. Mzigo huu ulikua na uwezo wa kubeba 56 tomahawk missiles in standard mode na 96 in attack mode pia ilikua inabeba zaidi ya 50 anti-aircraft missiles. Bila kusahau hiyo destroyer ilikua equipped na recent Aegis combat system pamoja na rada kubwa 4.

Ndipo ilipokutana na Russian jet Sukhoi-24, ndege vita hii ya Russia ilikua unarmed yani haikua na makombora kama ndege vita zinavyowekewa makombora ila Russia waliweka the most complex electronic warfare device inaenda kwa jina la khibiny.

Wakati Russian Su-24 ilipokua inaikaribia USS Donald Cook, ile eletronic device yake ika disable all the radars, control circuit, systems, information transmission na mambo mengine mengi tu yakawa hayafanyi kazi tena kwenye ile USS Donald Cook. Yani kiufupi ile modern Aegis system ikazimwa na electronic warfare device ya Russian jet kama unavyozima TV yako na remote control.

Russian jet ikacheza cheza pale kwa dakika kama 90 then ikarudi zake ilipotoka mda wote huo crew iliyokuwepo kwenye destroyer USS Donald cook walipanic sana, walikua demoralized na baadae baadhi ya vyanzo vya habari vikasema among ile crew nzima, 27 waliomba kuwa "relieved from active service"

Sasa ndio ujiulize Russia walikua wanajiamini vipi mpaka wapeleke Su-24 bila missile wala bomu lolote, waliweka tu electronic warfare device na wakaamini inatosha alafu wakaipeleka kwenye US navy destroyer iliyokua na most recent, modern combat system? Technology yao sio mchezo kiufupi Su-24 ilikua kama inafanya "simulated attack"

Ukisikia Biden anasema hataki direct confrontation na Russia anaelewa Russia ikoje nje ya propaganda za media yani anaijua Russia halisi.

Leo hii wewe unasema Russia haina technology wakati technology ya kisasa iliyoaminiwa na USA ilizimwa na electronic device ya Russia kama TV.






 

Attachments

  • 20220806_153236.png
    70.3 KB · Views: 25
Xi JinMandonga ametufelisha sana BRICS, ilibidi akaze amlipue huyo bibi halafu tuone US atafanya nini! Angelianzisha tungemualika kiduku ili akinukishe wakati wao wanashambulia China. Urusi nae angewasha tambo lake "Satan"
China hana huo ubavu. Uchumi wake sahivi unapumulia mashine. Russia ndo anahenyeshwa huko Ukraine.

BRICS wanategemea haohao G7 kutatua matatizo yao.

South Africa kama Tz tu, umeme tu sahivi unampiga chenga. Hayo ya vita atayawezea wapi?

Hakuna nchi ya Brics yenye uchumi wa kudumu kwenye vita kwa 90 days mfululizo.
 
Hii vita inamuumiza zaidi Russia kuliko Ukraine.

Rasilimali anazotumia Russia ni kubwa kuliko mategemeo yake.
Naamini Russia alijipanga zaidi na hii operation kuliko tunavyofikiria, alijipanga kijeshi na kiuchumi pia. Baada ya kuanza operation nchi za magharibi zilikimbilia vikwazo zikiamini kumuwekea Russia vikwazo kutamuadabisha na ataondoa jeshi ukraine. Nini kimetokea?

Vikwazo havikufanya kazi waliyoitarajia, nchi nyingi za ulaya kwa sasa hali za za uchumi ni tofauti na kabla hawajaweka vikwazo.

Angalia hata thamani ta hela ya Urusi mwezi march alafu angalia na august hii naamini Putin anacheza kete zake kwa akili sana.

Tuliaminishwa na western media kwamba uchumi wa Russia ni wa "kuunga unga" hivyo hawataweza kustahimili vita kwa mda mrefu ila kwa sasa tumeshuhudia tofauti.

Tukumbuke Russia ni mojawapo ya nchi zenye taasisi imara sana ya kijasusi haiwezi kufanya mambo kwa kukurupuka kama tunavyoaminishwa na media


 

Vijana wa 2000s hawawezi kuielewa Russia mkuu unatwanga maji kwenye kinu.
 
Mkuu una ongea mambo makubwa sna. Vijana wa Mihemko hawawezi kuelewa. Ni ushabiki tu.
 
Yule jamaa mchambuzi matata wa US tawi la JF kuna siku aliipigia sana chapuo huu mfumo wa Aegis. Aliweka maneno meeeeeeengi akidai dunia nzima hakuna wa kuugusa.

Ama kweli akiba ya maneno haiozi, Hivyo kuiweka sio dhambi...

Hili jukwaa huwa linanipa sana burdan 😂😂😂
 
Nalikumbuka Hili tukio asee 2016 hiyo bila shaka

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 

Nalikumbuka Hili tukio asee 2016 hiyo bila shaka

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
nakumbuka vizuri sana hilo tukio pia liliongelewa sana marekani nilikuwa ndio nimeingia nikiwa mgeni mgeni na all the main news channels were broadcasting and castigating their government
wacha niongezee na video hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…