Ukweli ni kwamba,Urusi Ina nguvu zisizo za kawaida.
Kama utakubali ama utakataa lakini ukweli usiopongika ni kwamba Urusi inapigana na NATO Sasa hivi.
Hata NATO nao wameshachoka na wameishiwa pumzi.
Katika NATO amebaki USA peke yake ndie anaeisaidia Ukraine kwa Kila kitu,kuanzia pesa,silaha,mbinu za vita na taarifa za Kijasusi na ushauri.
Tulishuhudia nchi Wanachama wa NATO walianza kwa mbwembwe kuisaidia Ukraine,kama akina Poland,UK,Canada na wengineo,lkn mwisho wa siku kabakia Marekani TU ndie anaetoa misaada ya fedha na silaha Kila kukicha.wengine wote wamekata moto.
Nina msemo wangu,Nina sema hivi,kwa kawaida ukiona mtu anaongeza kitu Fulani ujue alichokua nacho au alichokua akitumia,hakimtoshi au hakijamtosha.
Kwa mfano mtu akila chakula ,asiposhiba maana yake hajashiba au hajatosheka.
Kama ana nguo moja akienda kuongeza nyingine,ujue hiyo moja haijakidhi haha yake ya kumiliki nguo,
Ukiona mtu anakunywa maji,akiongeza chupa moja nyingine ujue Ile chupa ya kwanza haijakata kiu yake.
Sasa Iko hivi,Marekani toka siku ya kwanza alikua akitoa misaada ya silaha na fedha kwa Ukraine,Urusi wakazimaliza zote.Marekani wakaongeza nyingine,Urusi wakazila kama moto ulao,
Marekani wakaongeza Tena natena,Urusi wakaendelea kuzila TU.
Kwa Hali ya kawaida n Hali halisi kama silaha anazotoa ama alizotoa Marekani kama zingesaidia siku za kwanza TU,basi asingefoa Tena,maana yake zingekua zimeweza kufanya kile alichokua anakitaka.
Hapa ndipo nakuja kuamini kua kumbe Urusi sio nchi ya mchezo.
Niwendawazimu TU,asiejua kuwa Urusi inakabiliana na NATO, na kinara wa NATO USA akiwa ndio mtoa silaha mkubwa.
Ukiona Marekani inaongeza kutoa silaha kwa Ukraine,ujue zile za kwanza hazijagua dafu.sasa sio USA peke yake,Bali wapo na akina UK,France,German,Poland,Canada, Denmark, Australia,na utitiri wa vi nchi vimepeleka Silaha huko,lkn Urusi anazila.
Achilia mbali silaha,Kuna michango ya fedha,Ujasusi na hata askari wa nchi kamili na hata askari wa kukodiwa "mercenaries" kutoka Dunia nzima,lkn Hawa wote Urusi anawala.
Jamani vita ni gharama,hebu fikiria Urusi anapigana lkn kawekewa vikwazo vyote,hatukatai na wala wao hawakatai kuwa vikwazo vinawakwaza lkn mwamba anatoa dozi kama hayuko kwenye vikwazo.
Jamani eeeh tutake tusitake,tukubali tukatae Urusi anapigana na NATO na kiranja wao USA lkn Urusi Yuko peke yake na bado kawayumbisha vibaya sana.
Hii sio mara ya kwanza kwa Urusi kupigana na mataifa yenye Nguvu Sana hapa duniani.
Huko Afghanistan, Mujahedeen walikua wakisaidiwa na USA,UK,na NATO wote,China,Pakistan,Saudi Arabia,na utitiri wa vi nchi.
Urusi aliwamudu wote kwa miaka kumi na aliamua kutoka baada ya kuja na sera ya Mageuzi ya kiuchumi na kisiasa yaani Perestroika na Glasnost.
Mrusi hakushindwa Afghanistan kama USA alivyoshindwa Vietnam.