Ujerumani inawauzia Israel aina fulani ya diesel electric submarines zenye AIP system zile Dolphin class. Hizo subs hazikaribiwi na poor subs za Russia zile Kilo class. Hiyo Israel ndio mwalimu wa Russia kwenye drones. Israel huyo ndio bingwa wa kuharibu na kukwepa air defence system za Urusi. Maeneo yote ambayo silaha za Mrusi na zinakutana na za Muisraeli silaha za Urusi zifiche tu. Tumeziona vizuri Nagorno Karabhak. Sasa Israel haijawahi nunua silaha mbovu au kwa mtu mjinga asiyejua.
Ujerumani imetoa Gepard anti aircraft gun system kwa Ukraine. Hizo Gepard ilishaacha kuzitumia ikisema ni za zamani wala sio hadhi yake. Cha ajabu bado zinalitishia jeshi la Russia na Ukraine iliziomba.
Ujerumani imetoa Pz2000 ambayo ni the best howitzer waliyopokea Ukraine. Ogopa sana Ukraine wakipokea silaha kwa msaada kisha wakachangishana harambee kununua idadi nyingine ya silaha hiyo. Pz2000 ni bora kuliko French Caesar, Swedish Archer na yoyote aliyo nayo Marekani.
Imetoa silaha nyingi ndogo kama DM22 directional anti tank mines zenye uwezo wa kushangaza. Panzerfaust 3 ATGM ambazo ni nyepesi kuliko Javelin. Kuna mines nyingine, na silaha nyingi.
Rheinmetall kampuni ya Ujerumani ndio ilijenga Mulino, kituo kipya cha mafunzo ya jeshi cha Urusi. Hakuna yeyote pale Russia angejenga kituo kama hicho, Urusi walikuwa na vituo vya kizee ambavyo havina hata simulation capabilities.
Bado Rheinmetall inatengeneza silaha za uwezo mkubwa kama Leopard MBT.
Kulinganisha jeshi la Ukraine dhidi ya Ujerumani ni mchana na usiku. Ujerumani haiwezi tumia silaha yeyote made in Ukraine, ni silaha duni sana kwao. Vilevile haiwezi tumia silaha nyingi ambazo ziko deployed na Ukraine. Ukraine ina Su-27 na Mig-29 ambazo ni 3rd gen jets za miaka ya 70 uko wakati Ujerumani ina 4th gen Eurofighter Typhoon ambazo ndege ya kwanza imetengenezwa 2003.
Ukraine haina navy wakati Germany ina wargships na subs. East Germany ilikuwa na silaha ambazo ilizigawa kwa former Soviet block members miaka ya 80 na 90 uko. Mfano BMP-1 ilizipa modifications kubwa ikazipeleka Sweden kisha Czech Republic.
View attachment 2330591 Vita hii Ukraine ikaziomba na Wajerumani wakatoa ruhusa hizo junks ziende Ukraine. Wao hawawezi tumia kazi mbovu vile katafute IFV na APC wanazotumia na wanazodevelop.
Kuhusu morali ya kupigana na mwamko, hilo kajifunze kwanini Nazi Germany ilipozimavia Poland, France na USSR kwanini Britain na US zilikuja kuwasaidia. Huwezi linganisha Ujerumani na Ukraine. Huijui Ujerumani kwa kuwa haipigi kelele kama Russia. Unaamini kwenye kelele kuliko ukimya