Kwa mujibu wa bwana Putin mwenyewe. (Ma)Lengo kuu la military operation yake hapo Ukraine ni;-
1. Demilitarization of Ukraine
2. Denazification of Ukraine
3. Russian speaking Ukrainians in Donbass
Haya aliyasema kwa kinywa chake mwenyewe siku anatangaza kuanza kwa operesheni hiyo ya kijeshi.
Kuhusu Ukraine kujiunga NATO na swala la mipaka naweza kusema ili uelewe inabidi ujue ishu sio kupakana kimipaka kati ya NATO na Urusi (yaani sio kwamba Urusi anaogopa kupakana kimipaka na NATO). Juzi (wakati Finland na Sweden zimetangaza kujiunga na NATO) Putin amesema hawaoni tatizo nchi hizo kujiunga na umoja huo kwa sababu hawana territorial issues nazo wala disputes zozote na hivyo hawaoni shida sana nchi hizo kujiunga na NATO. Na pia akaongeza kuwa hizo nchi zitakubaliwa kujiunga na NATO ila hazitakubaliwa endapo zikitaka kudeploy silaha za NATO kwenye nchi zao na endapo zitafanya hivyo Moscow itarespond.
Msikilize mwenyewe putin "We do not have such problems with Sweden and Finland, which, unfortunately, we have with Ukraine. We have no territorial issues… no disputes…"
"Only they should plainly and clearly realize that there were no threats before, now, if military contingents and infrastructure are deployed there, we will have to respond in a mirror manner and create the same threats to the territories from which threats are created to us,"
Hoja kwamba Urusi kwa kuanzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya nchi jirani ili kuzuia nchi hiyo isijuinge na NATO ilisemwa na katibu mkuu wa NATO bwana Stoltenberg ili kuonesha kwamba lengo la Urusi kutaka kuzuia kusogelewa zaidi na NATO halijafikiwa na badala yake ndio kazidi kuzungukwa zaidi kwa nchi jirani nyingine kujiunga na NATO. Putin alijibu hoja hii kwa kusema Ukraine kujiunga na NATO ni tofauti na Finland au Sweden kujiunga na NATO au nchi nyingine. Hata hao NATO wenyewe wanaelewa;
"These are completely different things. They understand this perfectly, and they just throw this thesis into public opinion to show that Russia did not achieve the desired outcomes," alisema Putin
Kutokana na hayo yote naweza kufupisha malengo ya Urusi ni kuikomboa donbass na kulinda raia wake walioko huko na kutengeneza mazingira yatakayohakikisha usalama wao ikiwemo kuizuiq Ukraine kujiunga NATO. Ni kwa bahati mbaya sisi inakuwa vigumu kuelewa ni vipi Ukraine kujiunga NATO kuwe ni hatari kwa Urusi na sio kwa nchi nyingine zilizopakana na Urusi. Wao Urusi wanajua ni kwa vipi ndio maana hawataki na NATO wanajua ni kwa vipi ndio maana walikuwa wanalazimisha sana Ukraine ijiunga na si nchi hizo nyinginezo.