Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

I'la wako Tayari kuwa vassal state ya US
 
Issue ya The Khazarian Mafia nimei-elezea sana hapa JF,sijui umei-miss vipi.Anyway kukusaidia fuata link hii👉Khazarian Mafia and its evil plan to infiltrate, tyrannize the whole World and eradicate all Abrahamic Religions and take over the World.
Nilichokuwa nimewakilisha ni summary tu.
 
Labda ungetoa na reference tuone namna Putin alivyosema "... watakiona cha moto" kwa ninavyojua mimi Putin alionya kwamba kujiunga NATO kwa nchi hizo kutakuwa na consequences na hasa kama wakiruhusu deployment ya silaha za NATO kwenye nchi zao. Na hili alilisema baada ya na wala sio kabla. Kama unareference ya putin kutoa onyo kabla tafadhali liweke hapa.

Wananchi wa urusi ndio wenye maisha mazuri zaidi kwa mujibu wa takwimu za kiuchumi nizijuazo.
 
JPM angecheka saana kwa dharau
 
Inamaana hao 160k wamepungua sana wanaongeza wengine duu waleteni[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

 
Endeleeni kupiga majengo ya shule na hospitali sisi tunapiga military base
 
Umeandika vzr na umeeleweka tofauti na wengi humu
Habari za vita wao wanaleta ushabiki wa Simba na Yanga
 
1.Hakuna silaha za NATO, kila nchi mwanachama wa NATO inatengeneza, kuuza au kununua silaha kibinafsi kama vile tu ambavyo Uturuki inanunua na kuuzia silaha Urusi. Finland ananunua na kuuza silaha kwa nchi nyingi tu ambazo ni wanachama wa NATO, hakuna hoja ya maana katika hili kwamba tatizo sio kupakana bali ni silaha.

2.Hakuna mgogoro wa mpaka kati ya Ukraine na Russia. Mipaka ya Ukraine iko wazi, hata Russia yenyewe haijwahi kudai Crimea au Donbas ni sehemu ya mipaka yake, walichokifanya ni uhuni wa kuchochea vurugu hayo maeneo yajitangaze huru yajiunge na Russia halafu wakatangaza wanafanya Peacekeeping mission

3.Hakuna raia wa Urusi Donbas, unaposema kuna raia wa Urusi Donbas ni sawa na Kenya kusema kuna raia wake Wamasai Arusha au Msumbiji kusema kuna raia wake Wamakonde Mtwara au Uganda kusema kuna raia wake Kagera au Burundi kusema kuna raia wake Kagera. Ni upuuzi mtupu.

4.NATO haijwahi kutaka au kulazimisha Ukraine ijiunge nayo, kusema hivyo ni kutokujua mchakato wa nchi kujiunga na NATO.Haikuwa na vigezo vingi sana, nchi ZOTE wanachama hazikuwahi kujadili wala kuridhia hilo suala, Olaf, Kansela wa Ujerumani alimuambia Putin hata kabla hii vita haijaanza Ukraine haiwezi kuwa mwanachama wa NATO hata kwa miaka 30 ijayo.

5.Kusema tu Putin na NATO ndio wanajua tatizo la Ukraine kujiunga na NATO ni utopolo.
 
Hakuna Silaha za NATO, kuna vikosi vya NATO ambavyo kila nchi mwanachama inakuja na sila zake vinapokuwa deployed. Kila nchi mwanachama wa NATO anazo silaha zake.
 
Huyu Dotworld alikuwa hatari sana kwa habari za Urusi. Sijui Yuko wapi huyu mwamba.
Huyu jamaa nimejaribu kuzitafuta hata nyuzi zake za zamani sizipati kabisa....Kuhusu masuala ya Urusi na USA tulikua tunapata shule mujarabu kabisa...buree, bila matusi bila karaha....kuna jamaa pia walikua wanashusha nondo za USA mpaka raha...

Sasa hivi watu wanaojiita mathink tank...wanapresent hisia zao tu..wanaandika huku machozi yanawalenga...mapenzi yamezidi..mbaya sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…