Kwa hiyo intelligence ya urusi imelala kiasi Cha nchi kufanyiwa hujuma mara kwa mara?[emoji848]
Siwasemi vibaya lakini baadhi yenu uelewa wenu wa mambo ni dismal kabisa, am sorry kulitamka hilo - kuna mambo mengi tunayafahamu lakini huwa hatuyasemi for some reasons - kuna baadhi ya members ambao ni knowlageable kweli kwenye mambo fulani lakini badala ya kuwasikiliza na kujifunza kitu nyinyi mnawabeza beza tuu bila ya kuleta maoni mbadala yenye tija, hilo la kwanza.
La pili, sasa turudi kwenye mada - unaibeza Urusi kufanyiwa hujuma mara kwa mara as if haina itellijensia ya kutosha - oh, is it? Sasa nikuhoji hivi ilikuwaje taifa linalo jinasibu kuwa na intelijensia ya kufa mtu linazidiwa akili/kete na vijana karibu kumi kutoka Saudi Arabia na Misri wanapita kwenye airports zinazolindwa 24x7 na high tech survaillance systems wanapanda ndege za abiria tatu tofauti kwa muda tofauti, wanaziteka zikiwa angani wanaingia kwenye cockpit wanawafunga kamba marubani na wao kukalia kiti cha rubani na kugeuza ndege kwenda kuzibamiza kwenye critical targets walizo panga kuzishambulia tangu hawali, namely: NY trade center, Pentagon pamoja na Ikulu ya Merikani, malengo yao yalifanikiwa hisipo kuwa kuishambulia Ikulu ambayo kwa bahati nzuri abiria waliwawahi watekaji kwa kupigana nao kabla ndege haijafika anga la Ikulu, katika purukushani ndege ika anguka ghafla kabla haijafikia target.
Wewe unawabeza Warusi, hivi ilikuwaje tena Taifa la Amerika linalo jivunia ulinzi mkali wa: (anga, majini na nchi kavu, intelijensia za Kimungu Mungu, ground breaking silaha, jeshi imara - ilikuwaje vijana wa kiarabu wakafanikiwa kuzunguka na ndege za abiria kwa masaa huku abiria walipiga simu kuwaeleza ndugu na jamaa zao kinacho endelea ndani ya ndege ,lakini waongoza ndege aridhini hawajui wala kuona kwenye rada zao wapi zinaelekea, kumbe vijana wa kiarabu walizima transponder za ndege, je, air defense system zilifanya nini baada ya ndege ya kwanza kubamizwa kwenye jengo, baada ya dakika kadhaa ndege nyingine ikabamizwa kwenye wing lingine la jengo majengo hayo tasa - mbona USAF ilishindwa kidhibiti ndege ya pili, Cha aibu zaidi na kushambuliwa kwa makao makuu wa wizara ya ulinzi ya Merikani, nani ange amini kwamba makao makuu ya jeshi la Kimungu Mungu lingeweza kushambuliwa kirahisi kivile, one of the Pentagon wing ilishambuliwa na wafanya kazi wa Wizara kupoteza maisha,je,ili ni jambo la kawaida kweli - yaani moyo wa Taifa la Merikani linashambuliwa kirahisi!! Ikulu iliponea chupu chupu, bahati nzuri Rais Bush Jr hakuwepo Ikulu alikuwa amekwenda kuitembelea shule ya chekechea kwenye jimbo fulani nimelisahau jina, niliona alipo pewa taarifa na mlizi wake wakati huo Bush alikuwa ameshikilia kitabu anamsomea mtoto wa chekechea kitu fulani, alipo pewa taarifa alionekana kutishika sana wakambimniza sijui kwenda kumficha wapi? Makamu wake Mr.Dick Chenny naye nasikia alikimbizwa kwenda kufichwa kwenye mahandaki sijui ya wapi akifuatana na Waziri wa mambo ya nje Condelliza Rice, tukio hilo lilitingisha to the very foundation of US Administration.
Bottom line is: Mnapo wazodoa zodoa warusi kuhusu masuala ya kiitelijisia na ulizi wa Taifa lao kumbukeni vijana wa Kiarabu walivyo wazidi kete vyombo vya usalama vya Merikani - likumbukeni sana hilo na sio mnaiishia kumsema vibaya sema Putin mkasahau kilicho wahi kuwakumba Wamerikani their u
impregnable air defense systems,intelligence agencies notwithstanding.