Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,233
Kuna watu wengi walikuwa wqnajiuliza kuhusu uwezo wa urusi na kutumia muda mrefu na Kwa gharama kubwa kuiendesha hii operation, kuna watu walisema kuwa operation hii imechukua muda sababu ni
1) Ni kutokana na ukubwa na uimara wa jeshi la Ukraine
2) Ni uwezo mdogo wa urusi kijeshi
3) Ni Kwa kuwa urusi anajali Sana raia Kwa hiyo hataki kuua watu wasio na hatia, ndiyo maana anaenda taratibu Kwa uhakika ili kupunguza madhara ya kivita
Lakini kwangu Mimi naweza nikachukua namba tatu, lakini Siyo Kwa uzito huo,
Sababu ninayoiona Mimi hii operation inaenda taratibu Kwa mkakati maalumu kutoka Moscow, kitendo cha operation hii kwenda taratibu ni Kwa sababu hii
Wakati Vita inaanza mrusi alikuwa mkali na aliwapiga bit nchi zote za ulaya kuwa wasijaribu kuingilia ugomvi huo na atakaye jaribu atakiona cha Moto, na katika kipindi hiki ndicho urusi ilikuwa inatishia kutumia nukes, na KOSA KUBWA ambalo EU,NATO na USA walifanya ni kuogopa na kukaa pembeni Kwanza wakimsoma mrusi, katika kipindi wanamsoma mrusi ndipo west wakaanza Kwa kujaribu kupeleka silaha Ukraine na walipolleka silaha urusi akaonyesha kama kazidiwa na kurudi nyuma na kuachana na Kyiv, kitendo hiki kiliwatia moyo Sana Ukraine, NATO na USA Kwa kudhania kumbe wanaweza kuimaliza urusi,
Ndipo USA na NATO pamoja na EU wakaungana Kwa kupeleka silaha nyingi Ukraine ili waweze kummaliza moja Kwa moja urusi, na ikiwezekana wakomboe Crimea huku wakiweka vikwazo vingi zaidi Kwa urusi ili ashindwe kuiendesha operation yake yake, unajua baada ya urusi kugundua kuwa west wameshanasa akifanya nini? 😄😄😄😄😄 Ndipo Putin alikwenda China na taarifa zikavuja kuwa urusi imeishiwa silaha na chakula, hapa west wakavimba kichwa wakiona Zama za urusi zinaenda kuisha,
Baada ya west kupeleka silaha nyingi na za kisasa ndiyo muda mzuri mrusi alikuwa ameua ndege wawili Kwa jiwe moja
1) Kwanza alipata kujua technology iliyotumika kwenye kutengeneza silaha zile akaangalia udhaifu wake na pia aliangalia ni Kwa jinsi gani anaweza kuzidhibiti zisilete madhara makubwa
2) Kupitia hili nchi kama Poland ilisafisha ghala lake la silaha lote na kupeleka Ukraine, Kwa namna moja ama nyingine mrusi alisababisha nchi nyingi za ulaya zipunguze hifadhi zao za silaha Kwa kutegemea Ukraine atashinda Vita
Kitu ambacho hawakuamini ni pale mrusi alipoziangamiza zote na nchi nyingi zimejikuta zimeishiwa silaha mpaka zinaomba msaada
Sasa mrusi baada ya kuona jamaa wamekiuka makubaliano akaja na mtego mpya
1) akaweka vikwazo Kwa nchi za EU kuwa wakitaka gas wanunue Kwa rubo, ulaya walivyo vilaza wakaingia kichwa kichwa kwenye mtego wakagoma kulipia gas Kwa rubo mrusi akakata gas, nchi nyingi ulaya wakajikuta wanatumia gas Yao ya akiba Kwa kuwa hawataki kulipia Kwa rubo lakini baada ya siku chache Ile gas ya akiba ikaisha wakakubali kulipia Kwa rubo lakini tayari wameingiza damage kwenye hifadhi ya gas, na mrusi Kwa kujua west wamemaliza gas Yao ya akiba, akaja na mtego wa pili akapunguza kiwango cha kupeleka gas ulaya hii ikasababisha gas wanayoipata ni Ile itakayowawezesha kuishi sasa hivi tu hakuna gas ya akiba
2) baada ya kuona tayari vile zile nchi ndogo ndogo zimenasa akaanza kudeal na nchi kubwa kama ujerumani ambayo ina hifadhi kubwa,
Akafunga bomba la kupeleka gas ujerumani Kwa kisingizio kuwa pangaboi lilipo Canada ndilo linahitajika ili kuweza kufungwa ili gas iende ujerumani, yakaingia mabishano Kati yao wenyewe west na kipindi hicho chote ujerumani alikuwa anatumia gas yake ya akiba mpaka wanakuja kupata muafaka na kufunga bomba mjerumani kashatia damage kwenye hifadhi yake ya gas, kibaya zaidi mrusi akaja na tangazo la kupunguza kiwango cha kupeleka gas ujerumani kutoka 100% hadi 60%, hii maana yake ujerumani atumie hiyo gas bila kuweka nyingine akiba ,
Baada ya kufanikiwa hilo mrusi kaja na njia mpya kila mwezi anafunga bomba Kwa ajili ya matengenezo kipindi hicho nchi za EU zinalazimika kutumi gas ya akiba, lengo kuu la urusi ni kuhakikisha ulaya nzima kipindi cha baridi hakuna nchi yenye akiba ya gas
Sasa ulaya ndiyo wanagundua sasa lengo la mrusi ndiyo maana zimezuka hoja za kuwasha vinu vya nuclear vilivyopo ulaya ili kupata nishati, kibaya zaidi hii mitambo ya nuclear imekaa muda mrefu bila kufanya kazi kwahiyo wanahitajika wataalamu ili kuweza kufufua hiyo mitambo kibaya zaidi hao wataalamu wanapatikana urusi,
Kitu kingine hiyo mitambo inahitaji kufungwa vipuri vipya, ambapo hivyo vipuri vinapatikana Russia
Pia wanahofu kutokana na mitambo hiyo kukataa Kwa muda mrefu bila kutumika kuna uwezekano wa baadhi ya maeneo kuwa yameliwa na kutu na ikatoka mionzi ikavuja,
Kitu kingine ni kuwa hata wakiwasha hiyo mitambo ili upate umeme unaohitaji itabidi wasubiri kama mwaka mmoja, kitu ambacho matatizo waliyokuwa nayo ulaya hayawapi nafasi ya kusubiri Kwa muda huo
Sasa faida ambayo mrusi kapata baada ya hii operation kuchelewa ni
1) kujua ulaya Wana silaha gani na zinauwezo gani, na wamejua ni namna gani wanaweza kuzizuia ili zisilete madhara makubwa
2) kupunguza hifadhi kubwa za silaha zilizopo kwenye mataifa ya ulaya
3) kupunguza uwezo wa NATO na EU kwenye nishati hii inasaidia mpaka sasa kuwa hawana uwezo wa kuzalisha silaha nyingi Kwa wakati mmoja kutokana na upungufu wa nishati WA kuendeshea viwanda vyao vya silaha
4) kupitia vikwazo ambavyo ulaya wamaiwekea urusi nchi nyingi za ulaya zimeyumba kiuchumi na hivyo kupunguza uwezo wao wa kuendesha Vita ya muda mrefu na mrusi
5) mpaka sasa hivi mmarekani kajua wazi kitendo Chao cha kusubiria kumsoma Putin anawaza nini juu ya Ukraine lilikuwa kosa kubwa maana kama sasa hivi vikitokea Vita basi MTU pekee atakayewajibika ni USA Kwa kuwa ameshajua EU na NATO wamekwisha choka yaani hawana uwezo wa kupigana Vita na taifa kubwa kama urusi, Kwa hiyo akiingia Ukraine yeye ndiye atakayeandamwa na akipigwa yeye maana yake ulaya nzima imeanguka
Kiufupi mpaka sasa mrusi yupo kwenye nafasi nzuri ya kupigana Vita hasa muda huu ambao baridi linaanza ulaya, naona kila dalili ulaya ikisambaratika bila urusi kuingia vitani, na ikisambaratika ulaya na marekani inatafata maana bidhaa za marekani zitapigwa ban nchi za Asia na kusababisha marekani akose soko la kuuza bidhaa, na kutokana na hali ya uchumi wananchi watafunga mikanda na hapo ndipo anguko la marekani lilipo
Barikiwa sana kwa maelezo yako yaliyo kwenda shule, once again thanks a lot - naona umesahu kidogo kuwakumbusha some members kwamba actually mpaka sasa Urusi inatumia asili mia 2% tu ya uwezo mkubwa wa nguvu ya jeshi la lake, wangapi wanajua ukweli huo??