Ungeanza kwanza kujiuliza kwa nini Ukraine itake kujiunga NATO kabla ya kuanza kuuliza kama baada ya miaka 30 itajiunga.
Hakuna promises yoyote iliyoweka kwamba NATO isingesogea kutoka West Germany, hizo ni porojo tu.Katika NATO- Russia founding Act ya 1997 Russia iliridhia kila nchi huru kujiamulia mustakbali wake ikiwa ni pamoja na kujiunga na alliances ambazo inaona zina manufaa kwake.
Russia ilikuwa inasapoti uasi mashariki mwa Ukraine, iliichukua Crimea, inasapoti uasi katika majimbo kadhaa ya Georgia halafu juu ya hayo bado inataka written guarantee ya Ukraine kutojiunga NATO!!! Sasa Ukraine ingebaki na leverage gani kwa adui anayetishia sovereignty na existence yake kama taifa ??!
Halafu unafahamu Written guarantee ya US kuhusu NATO ni suala la Congress sio la Rais? Hiyo ishu ingefika Congress ya US isingepata hata robo ya kura za Republicans tu.
Hivi ni kwa Nini Russia au China akisema kwamba hili swala x y z linahathili national security yake inakuwa sio sawa kusema, sio kweli, wanaongea uongo, wanataka kuleta Vita etc.
Lakini hapo hapo US akisema kwamba wapo concern na swala flani kwa kuwa linahatarisha usalama wao, linakuwa Ni swala la kweli, US anaongea ukweli, lazima asikilizwe, lazima aachwe afanyalo ili kujilinda.
Kwa Nini nasema hivi...?
Chukulia mfano wa juzi hapa, China ameingia mikataba ya Ulinzi na Solomon Islands (US amekuwa concern na inahatarisha usalama wake)
China kutoa mikopo kwa Africa (US amekuwa concern na Africans wanaingia kwenye debt trap)
Iraq alishambuliwa na nchi kuharibia kwa reasons ambazo Ni fake (US alikuwa concern na WMD, ambazo hazikuwepo)
Iran na North Korea kuwa nuclear na weapons (US amekuwa concern na anafanya kila awezalo ili kuhakikisha hawapata hiyo chance ya kuwa na hizo silaha)
Kosovo kujitenga na Serbia, US anaona Ni sawa kabisa, lakini Crimea kujitenga na Ukraine, US amekuwa concern na ameweka vikwazo.
Okay, mifano hipo mingi Sana.
Kwa Nini nimejaribu kukupa hiyo mifano, Ni kwa sababu Kuna double standards sana na Kama kweli wewe hupo reasonable, lazima utaiona tu.
Je, kuna tofauti gani Kati ya Cuba Crisis na hii ishu ya Ukraine? Au ishu ya Taiwan ya US kupeleka vifaa vyake mpakani mwa China
Tujaribu kujadili kwa reasonableness,