Kwanza kwenye kujadili suala la huu mgogoro ninachokiona wengi wana involve emotions, ukishahusisha hisia lazma utatoka out of control na kuanza kutukana watu, kujibishana kwa kejeli, hasira na mengine mengi.
Chukulia hii kama muvi tu sisi ambao tuko nje ya vita tuwe watazamaji, toa mtazamo wako juu ya vita inayoendelea bila kumkejeli/kumtusi mwenye mtazamo tofauti na wako. Kusema unamuona mjinga mtu anayemsapoti Russia?? Wewe mwenye mtazamo tofauti ndio mwerevu??
Ukweli wa Russia kumvamia ukraine wanaujua wenyewe hao Russia na Ukraine na hayo mataifa makubwa pia wanaujua ukweli. Kuna sababu tunazozijua na tusizozijua kwa nini Russia kavamia ukraine, Putin hajaamka tu alfajiri akaamuru majeshi yake yaivamie Ukraine kuna vingi sisi washabikia vita hatuvijui ila wenyewe wanavijua.
Athari nyingi ni sababu ya vikwazo ambavyo Russia imewekewa, umeshajiuliza kwa nini Israel na Palestina kwenye mpambano wao, UN walitaka wakae mezani waongee na kumaliza vita bila kuiwekea kikwazo chochote Israel? Kwa nini mfumo huo huo usingetumika kwenye mgogoro huu? Kwa nini hawakushinikiza Russia na Ukraine wamalize mgogoro wao kwa mazungumzo ila wakakimbilia kushinikiza kwa kuweka vikwazo na mwanzoni walikia wanaisaidia Ukraine silaha?