Yeah ni kweli wala jsmaa hana kosa.Tukikumbuka mwanzo Russia alihitaji yale majimbo na Ukraine kutokujiunga Nato.
Lakini deep inside Aligundua mambo yaliyokuwa yanaendelea ndani ya Ukraine Mengi yakihatarisha usalama wa nchi yake, Ikiwemo kuwepo kwa vinu vya Nuclear.
Utagundua huu mgogoro Putin wala haitaji Negotiations, Negotiations zipo kwajili ya Kuwagelesha Mataifa mengine asionekane rude.
Brother Pumzika Pata kawaha kidogo, Nitalipia snacksMarekani hasingiziwi ndilo taifa lililoongoza uvamizi wa nchi nyingi duniani...Marekani ni taifa la kinyama kabisa...ni taifa la kishetani...USA imevamia zaidi ya nchi 15 duniani na kuwaondoa viongozi...Panama, Irak, Chile, Haiti, Libya, Serbia na nchi nyingine kadhaa duniani...hata Syria Kama siyo Russia saa hizi Assad ingekuwa ni historia...Mimi nimesoma historia na politics za USA na nchi nyingine ambazo ni Industrial States duniani..na nimefika Marekani...kwa wasiojua watu wa asili wa Marekani ni Wahindi Wekundu...lakini waliuawa kwa mamilioni ...More than 20 million Red Indians died...ni genocide ya Aina yake...Wahindi Wekundu waliobaki huko Marekani hivi Sasa wanaishi kwenye maeneo yaliyotengwa Kama wanyama kwenye zoo...Wamarekani kwa Sasa huwa hawataki kabisa kuzungumzia issue ya Red Indians kwani kwao ni fedheha...USA Ina jela ya kutisha ya Guantamano iliyoko Cuba...democracy???!!! Stupid...suala la Ukraine walioharibu ni USA na mashoga zake wa ulaya...stupid guys...wanajacili Uhuru wa kutoa maoni lakini wao wenyewe ni washenzi na ambao wanafungia vyombo vyote vya habari vinavyotoa taarifa tofauti na za kwao kuhusu Ukraine.....
Sasa wamekutana na Putin ambaye amejiandaa for almost 20 years ili kuwaangamiza Wamarekani na vibaraka wait...wakileta za kuleta Putin anafyatua nuclear...kutakuwa hakuna mshindi katika Vita hivyo...kwani dunia nzima itateketea...Wamarekani hawataki hilo...wamekuwa outsmarted..Russia ndiyo inayoongoza kwa silaha za nyuklia duniani....makombora mengine ya nyuklia ya Russia yakirushwa tu hewani hujjigawa katika vipande zaidi ya 20 huku Kila kimoja kikiwa na uwezo wa kuua mamilioni ya watu...stupid Americans ..
Mabomu hukosea pia kwa kutua uko sahihi.Mabomu hayana macho ya kuchagua huyu raia huyu bedui
Sawa brother,kwa kuanzia lete takwimu zako zikisaport madai yako.Kwa kuanzia😂😂😂mkuu imenichekesha Ulaya inamuhitaji Urusi kuliko Urusi inavyohitaji ulaya?Bro kabla ya kuongea fanya tathmini kwanza.Putin vikwazo alivyowekewa sio vya kitoto.Embu jibu hoja kwa facts na sio mihemko
Wayahudi ndio akinaniMrusi kachokoza nyuki kumbe Raisi wa Ukraine ni myahudi ,wayahudi wa Ukraine wasema lengo la Putin ni kufuta wayahudi walioko Ukraine na kumwondoa Raisi wao myahudi
Nimesikiliza CNN jamii ya wayahudi wa Ukraine wanasema Putin ni Hitler wa pili
Kapiga mabomu hadi.memorial yao Ukraine ambako eneo hilo la Ukraine Hitler aliua wayahudi mamilioni kwa lengo la kuwafutilia mbali
Sasa Putin kaanza kuwalenga wao na majengo yao wanayoishi
WayahudiWayahudi ndio akinani
Hii moderators iwekeni separate jukwaa la siasa msichanganye iwe separate kama tangazo la serikali
Ngoja mazungu ya Western Country yapigwe na baridi mpaka wagande Russia haita pump gas kwenda huko
Umeongea mengi kuona kama unaelewa sana kumbe bado uwela wako wa medani uko chini, kama hujui vita ni sanaa sio kama unavyofikilia wewe, kuna vitu vingi vinatokea kwenye vita ambavyo vinahusisha uwezo wa makamanda wa vikosi ambavyo viko front, najua wengi humu ni civilian hawaijui vita in its technical sense, in fact urusi amezudiwa mbinu za medani na mabeberu ambayo yanampa backup Ukraine, cha kwanza alitumia military showoff kuwa intimidate wa ukraine na pili kitendo kufanya drilling mpakani kili wa alert ukraine na washirika wake kujiandaa kivita. Inaonekana wazi kabisa mpango wao wa uvamizi ulivuja ndio maana beberu mkuu USA aliwaomba raia wake kuondoka Ukraine alijua nini kitatokea. Kwa mwenye uwezo wa kutumia common sense Niko tayari kukoselewa mabeberu yamemzidi Putin mbinu, vikosi vyake vimeshindwa kabisa ku advance richa ya kutumia powerful fire support lakini group assualt hawapenyi kila wakisogea wanabondwaNimekuwa mfuatiliaji wa maoni ya watu mbalimbali juu ya huu mgogoro wa Ukraine na Urusi acha nami niandike kile ambacho naamini kwenye huu mgogoro.
Mapema kabisa Urusi ilipoanza mazoezi ya pamoja na Belarus, Washington ilionya kuwepo kwa uvamizi nchini Ukraine kutoka Urusi. Baadaye yakifanyika mazungumzo na ikaonekana Urusi amerudisha majeshi yake ila kauli ya siku zote ya Urusi alikuwa akisema "HATAKI VITA" shinikizo la kuchochea uvamizi lilikuwa linaendelea kutoka Magharibi na si Ukraine kwa maana Marekani alikuwa na taarifa juu ya kile ambacho Urusi inapanga juu ya Ukraine.
Putin anatangaza kuyatambua majimbo yaliyojitenga na kusema atapeleka majeshi kulinda raia na hatimaye anafanya hivyo na haishii kwenye majimbo tu aliyoyalenga anataka kung'oa serikali yote ya Ukraine na kupandikiza pandikizi lake pale. Majeshi ya Urusi yanaanza kusambaa kwenye maeneo mbalimbali ya nchi ya Ukraine. Upinzani umekuwa mkubwa sana kutwaa mji mkuu Kiev. Japo kwa wengi wanazungumza hili suala kishabiki sana kuliko kiuhalisia.
Ngome pekee ambayo imeonekana kuwa na nguvu nchini Ukraine ni kutwaa mji wa Kiev ambao ni makao makuu ya serikali na shughuli mbalimbali. Isingekuwa rahisi kwa Urusi kuchukua Kiev kama jinsi ambavyo Wamarekani wa Songwe na Warusi wa Ilula wanavyodhani. Baada ya uvamizi Zelensky alitangaza kuwapa silaha raia walinda nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi na tumeendelea kuona idadi kubwa ya raia wakichukua silaha kwa ajili ya mapambano. Ukraine ni taifa lenye watu takribani milioni 42 na mji wa Kiev una watu wapatao milioni 2.7 (tuseme milioni 3)
Urusi iliandaa idadi ya wanajeshi wapatao laki moja na nusu hadi laki 2 kwa ajili ya operesheni/uvamizi huo. Idadi ya wanajeshi ambao Urusi ilipeleka Ukraine ni sawa kabisa na idadi ya wanajeshi wa Ukraine. Urusi ina wanajeshi wapatao laki 9. Nimeona media nyingi zinaandika kuwa asilimia 75 ya jeshi lipo Ukraine kitu ambacho wanashindwa kufafanua kuwa ni asilimia 75 ya wanajeshi walioandaliwa kwa ajili ya uvamizi/operesheni.
Urusi inapata shida kuuteka mji wa Kiev kutoka na aina ya mashambulizi waliyochagua au kile ambacho wameamua kufanya. Mji wenye raia milioni 3 usingekuwa mgumu kuwa mikononi mwa Urusi kama ingeamua kufanya MAUAJI ya halaiki ili kuhakikisha mji upo mikononi mwao hata kwa masaa 2 ama 5. Inawezekana na mataifa yote yanajua hivyo inawezekana Kiev kuwa chini ya Urusi kwa muda mfupi zaidi ya mbinu hii waliyotumia ya kupiga maeneo muhimu huku wakitaka raia kuondoka ili wapambane na majeshi ya Ukraine.
Kiev ingekuwa unakaliwa na wanajeshi pekee yake ni imani yangu kuwa hadi sasa Urusi ingekuwa imeteka mji huo na kuwa chini yake. Wengi tunaongea kushabiki na kushindwa kung'amua kwanini Urusi umeshindwa kuchukua mji huo hadi sasa. Jibu ni kuwa haitaki kuua raia na ingekuwa inataka kufanya hivyo idadi ya vifo ingekuwa mbaya sana huko Ukraine.
Siyo Marekani wala NATO wote wanajua uwezo wa kijeshi wa Urusi na hata wao wanajua Urusi hajatumia hata asilimia 40 ya uwezo wake wa kijeshi dhidi ya Ukraine ila kwa sababu ngozi za Waafrika ni nyeusi nasi tumemezwa na ushabiki tumeamua kugawana fimbo na kila mmoja anamchapa mwenzake kishabiki na si kiuhalisia.
Macron mapema leo ametoa pongezi kwa jeshi la Ukraine ila akakiri haoni kama watahimili nguvu za jeshi la Urusi siku za karibuni. Ni wazi wote wanajuana na wala Macron hajawaambia kinafiki anajua nini ambacho Urusi anacho. Laiti kama uwezo wake wa mashumbulizi ungekuwa umefika mwisho leo ungeziona nchi zenye nguvu kijeshi zikiibuka Ukraine moja kwa moja kuipiga Urusi ila wanajua Urusi ni nani na wameamua kumheshimu katika maamuzi yake ila wamebaki kupiga kelele na vikwazo.
Kwahiyo tunapolizungumza hili suala tusilichukulie kama malumbano ya Simba na Yanga maana haziumii nyasi huko Ukraine wanaumia watu hata kama ni wanajeshi wana familia zao. Hakuna familia inayotaka kuona inaletewa ndugu yao akiwa kwenye jeneza akiitwa shujaa.
Vladimir ameendelea kusisitiza na kusema nia yake kwa Urusi lazima itimie hata kama watafanya mazungumzo, yaani ni kuwa Urusi ili irudi nyuma ni lazima matakwa yake yasikilizwe jambo ambalo hakuna mtu au nchi itaenda mbele kuzuia uvamizi wa Urusi pale Ukraine, wataipa kichwa Ukraine ila hawataumia raia wa Ujerumani wala Canada bali wanatumia raia wa Ukraine na jeshi la Ukraine.
Urusi itafanya kile inacholenga juu ya Ukraine hata kama atamaliza mission akiwa kachoka kiuchumi ila lazima afanye na lazima atimize kile ambacho anaamini juu ya mgogoro huu. Huu si uvamizi wa kwanza kuonwa ukifanywa duniani na hata si mara ya kwanza kwa Urusi kufanya uvamizi wa aina hii. US ni kinara wa vamizi za aina hii ila hakuna siku kaonekana mbaya tumejaa unafiki wa kuikosoa Urusi na kuona ni taifa dhalimu na lenye ushetani ila tuition ya somo hili Urusi imelichukua kutoka kwa US na punde Uchina nayo itajifunza na Taiwan itatwaliwa.
Kwahiyo kama US alifanya dhidi ya wengine akaona ni sawa asinyenyuke kukemea masomo ambayo yeye mwenyewe ndiye mwalimu wake. Urusi atapoteza uchumi wake na kila aina huduma kutoka Ulaya na maeneo mengine duniani ila ili Urusi iwe na ukomavu wa leo na kesho NI LAZIMA AICHUKUE UKRAINE IWE ISIWE. ndicho ambacho Putin kamwambia Macron.
#MbaoZaMawe
Wanahitaji utulivu wa Hali ya juu sanaaaaaa. ...Nilifurahi sana Chancellor wa Ujerumani alipoanza kutoa vitisho ,Mr. Putin akaweka tayari vikosi vyake tayari baada ya hapo hatusikia chokochoko wala kelele yoyote. Mjerumani ndio hata asiongee ataponza wenzake Urusi ana machungu naye sana.
Eti ki nchi kama Lativia ambacho kina ukubwa wa wilaya moja ya ukraine inaivimbishia Urusi. Huo umoja unadanganyana sana, bora wanaona hawawezi kuingia front wawe neutral tu
Nimeheshimu mawazo yako kama ulivyoheshimu mawazo yangu.Umeongea mengi kuona kama unaelewa sana kumbe bado uwela wako wa medani uko chini, kama hujui vita ni sanaa sio kama unavyofikilia wewe, kuna vitu vingi vinatokea kwenye vita ambavyo vinahusisha uwezo wa makamanda wa vikosi ambavyo viko front, najua wengi humu ni civilian hawaijui vita in its technical sense, in fact urusi amezudiwa mbinu za medani na mabeberu ambayo yanampa backup Ukraine, cha kwanza alitumia military showoff kuwa intimidate wa ukraine na pili kitendo kufanya drilling mpakani kili wa alert ukraine na washirika wake kujiandaa kivita. Inaonekana wazi kabisa mpango wao wa uvamizi ulivuja ndio maana beberu mkuu USA aliwaomba raia wake kuondoka Ukraine alijua nini kitatokea. Kwa mwenye uwezo wa kutumia common sense Niko tayari kukoselewa mabeberu yamemzidi Putin mbinu, vikosi vyake vimeshindwa kabisa ku advance richa ya kutumia powerful fire support lakini group assualt hawapenyi kila wakisogea wanabondwa
Chezea Putin weweNato member wakiwa mkutanoni wanaulizana ni nani atamfunga paka kengele hadi saiv hakuna aliyenyoosha mkono. Tuliona marekani akinyoosha tukamwangalia akasema mie hapana najinyoosha tu viungo.
Source of water