Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kumbe wamekaribia mwisho. Igizo la "spesho opereshoni" - hakuna anyeamini. Askari - hawana wa kutosha.
Wanahitaji maelezo mazuri wakitaka kulazimisha wananchi kushiriki vitani na kuchunua wanaume kuwa wanajeshi (maana hadi sasa walitangaza kiynume).
Kumbe wanaanda kura bandia kuhusu Donabas na Kherson - watatangaza maeneo kuwa sehemu ya Urusi - watatangaza Urusi huo unashambuliwa - wameshapata sababu ya kulazimisha wanaume kuwa askari

Ila: Nani ataamini???
 
We'we dada, huwa nakuheshimu Sana ujue...wewe ni miongoni mwa wachache wa upande wa pro..NAto ambao huwa nawaheshimu...sitarajii uanze kuzungumzia eti HIMMARS sijui nini
 
We'we dada, huwa nakuheshimu Sana ujue...wewe ni miongoni mwa wachache wa upande wa pro..NAto ambao huwa nawaheshimu...sitarajii uanze kuzungumzia eti HIMMARS sijui nini
Asante sana kwa heshima yako Mkuu nami naipokea,lakini uhalisia wa mambo ndiyo huo.Naondoa neno HIMARS kwakuwa linakuletea ukakasi ili uweze kunijibu maswali yangu.Kwenye malengo ya mwanzo kabisa ya hii operation yalikuwa ni yapi?.Labda nisaidie kujibu hili swali pia,ile nia ya Russian troops kuelekea Kyiv ilikuwa na lengo gani? Ni kweli haya yanayotokea sasa ndiyo yalikuwa malengo ya awali ya hii 'Special Operation'?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…