Unajua hawa vijana, kama wangeacha tu kukurupuka na kusoma comments kwa utulivu wangegundua matatu kuhusu
Mag3!
- Mag3 ni mtu anayechukia utawala wa kiimla haijalishi mhusika ni mweusi, mwekundu au mweupe!
- Mag3 ni mtu anayeunga mkono utawala wa sheria unaozingatia na kuheshimu Katiba ya nchi.
- Mag3, hana unafiki...koleo ataliita kwa jina lake na nyani giledi atamkoma bila ya kumtazama uso.
Humu JF, ID yangu ni ile ile na sijawahi kutumia nyingine kwa sababu siamini nina cha kuogopa kama nasema ukweli, katika hilo sina unafiki!
Ni wachache sana humu wanaoijua historia ya
Jamii Forums baada ya mtangulizi wake
Jambo Forums kupewa msukosuko na serikali ya CCM.
Kwa bahati mbaya kuna kundi limekuja kuivamia JF kwa lengo la kuidhoofisha na sasa kauli mbiu ya
nguvu ya hoja imebadilishwa kuwa
hoja za nguvu.
Udikteta haujawahi kufanikiwa popote pale na kama walivyoondoka Hitler, Sadam, Emporer Bokasa, Idi Amin Dada na wengineo, hivyo hivyo ataondoka Putin.