Mkuu asante kwa hoja na sababu za maana unazotaja!
Bila shaka Ulaya magharibi inaona matatizo ya kiuchumi shauri la kukosa nishati kutoka Urusi. Si vile kwamba Ulaya yote inategemea nishati hiyo lakini kufungwa kwa mabomba yalipandisha bei juu mno kwenye masoko hayo ya kibepari.
Ila, wakifaulu kuvuka nusu mwaka unaokuja (hadi mwisho wa winter kule) matatizo yao yatapungua. Maana nchi hizo zote ziliamua tayari kuondoka kwenye nishati ya kabohidrati yaani mafuta na gesi kwenda nishati mbadala katika miaka ijayo. Vita hii inaharakisha mwendo huo. Mfano Ujerumani ni uchumi mkubwa uliotegemea hasa gesi ya Urusi lakini hapa wananchi waliamua kwenye uchaguzi uliopita kuimarisha vyama vinavyotaka kuondoka haraka zaidi kwenye uchumi wa gesi na mafuta.
Tatizo walizo nazo sasa na kwa miaka michache ijayo hawana miundombinu wa kutosha (yaani mabandari ya pekee) kupata gesi miminika kwa meli (jinsi ilivyo Hispania na Ureno ambao hawatumii kabisa gesi ya Urusi) ila sasa wanajenga kwa mbio. Kuanzia mwaka ujao watakuwa na vifaa vya kutosha kupokea gesi miminika kutoka Marekani, Qatar na penginepo duniani. Tayari sasa bei ya gesi imeanza kushuka kwenye soko la dunia, maana vurugu ya kwanza sokoni )kawaida baada ya mabadiliko ya ghafla) imeshakwisha. BAdo ghali, bado hali ngumu, lakini kuna mtazamo ni hali nafuu.
Tuone jinsi gani jamii hizo za Ulaya magharibi zitavumilia matokeo hasa katika miezi ijayo. Hadi sasa idadi kubwa ya wananchi huko inakubali msaada kwa Ukraine na hatua dhidi ya Urusi, hata kama asilimia 30-40 wana wasiwasi au kupinga. Hivyo marafiki wa Putin wa hapa wanaweza kuleta kila siku mifano ya maandamano na upinzani dhidi ya siasa rasmi. Ila kwa sasa ingekuwa mwisho kwa kila serikali katika Ulaya magharibi kama ingehamia upande wa Urusi. Asilima 60 ni wengi zaidi kuliko asilimia 40 (hata kama hao si wachache).
Tuone jinsi gani mambo yatakavyoendelea.