Part 2
Baada ya urusi kutangaza operation hapo Ukraine, marekani na west wakakimbilia kuweka vikwazo lukuki halafu wakakaa kutulia kusubiria matokeo ya vikwazo walivyoweka, wanakuja kushtuka ni pale walipoanza kuhisi maumivu ya vikwazo badala yasikike Kwa raia wa urusi wakaanza kusikia Kwenye mitaa ya New York, London, Paris na kwingineko, ndipo wakaja kujua vikwazo vinawaumiza wao zaidi kuliko mlengwa ambaye ni urusi, na kipindi hiki cha matazamio ndipo urusi alichukua maeneo ya kimkakati na kiuchumi ya Ukraine na kujikuta west wameingizwa chaka tena na Urusi
Mimi siamini kama ilitokea bahati mbaya Ila ninachojua ulikuwa mkakati wa urusi na China kuprovoke na kutengeneza hali ya wasiwasi ya Taiwan ili kupata sababu ya kuanzishwa Kwa Vita ya pili na marekani, ni akili kubwa Sana alitumia uchina kurudi nyuma kipindi pelosi anatua Taiwan lakini lile tukio lilivuta hisia za watu Wote duniani wakiamini Vita ipo njiani Kati ya China na marekani, mpaka mwisho wa mchezo mchina akaondoka na ushindi wa point tatu kwenye mioyo ya watu wengi duniani maana kupitia tukio lile mmarekani akaonekana ni mbabe na mgomvi na mpenda Vita, yaani kiufupi ni mtu wa shari huku uchina akichukua Kura za huruma kote duniani, sasa kuanzia hapo ikaanzishwa Vita ya pili rasmi ambayo ni uchina na marekani kwenye suala la uchumi
Jana pentagon wamekubali hadharani kuwa USA anapigani Vita ya kiuchumi na mchina na pia Vita ya kijeshi na Urusi, kiufupi hapa kila mtu anacheza mechi zake kwenye uchumi mpaka sasa mchina anapiga kumbe za chembe za kufa mtu,
Kwanza ulaya ambao wangeshirikiana na marekani kwenye Vita ya kiuchumi wameshachoka hawajiwezi Kwa kukosa gas ya bei rahisi ya urusi
Pili mchina anapiga bao Kwa kuwa anapata gas ya bei ya chini, ana walipa wafanyakazi pesa ndogo na anatengeneza bidhaa za quality kubwa kama za marekani lakini anauza Kwa bei ndogo kuliko marekani, sasa ukijumlisha na anguko la uchumi na mfumuko wa bei utajijibu mwenyewe Nani anaenda kuteka soko la dunia
Huku Kwa mrusi kama west na marekani ndiyo wanakuja kugundua lengo la urusi kuingia Ukraine Siyo kuwaangamiza manazi na kuzuia Ukraine isijiunge na NATO tu bali pia URUSI IMEPANGA KUZIANGUSHA NCHI ZOTE ZA WEST PAMOJA NA USA KIUCHUMI NA KIUSHAWISHI DUNIANI
Inaendelea...........
Part 3
Hapa ndipo tunakuja kuona kwanini mrusi anataka hii Vita isiishe mapema, yaani mrusi anataka pawe hivyo hivyo yaani Ukraine hawasongi mbele na wala yeye hamalizi Vita haraka yaani inakuwa 50/50, faida ya hii Vita kukaa muda mrefu ni pamoja na
La Kwanza kabisa ni kuzimaliza silaha zilikuwa kwenye maghala kwenye mataifa hasa ya ulaya maana haya anaishi nayo pua na mdomo,
La pili ni kupunguza gas na hii imesababisha hali kuwa mbaya kiuchumi maana viwanda vinafungwa watu wanakosa kazi, baridi linakuja na sasa hivi wanatumia gasi ya akiba ambayo urusi anataka iishe kabisa ili machafuko hapo ulaya yatamalaki kama walivyokuwa wanasubiria yatokee urusi, ndiyo maana IMF ( kama nimekosea kuhusu hilo shirika kusema naomba kusahihishwa) wamesema kuwa ulaya watakutana na mfumuko mkubwa wa bill za umeme ifikapo march 2023, Kwa kuwa wanajua kipindi hicho ulaya watakuwa wamemaliza gas yoke kipindi cha baridi na hawana akiba
La tatu la kuchelewesha hii Vita ni hata kama Leo hii Vita inatokea Kati ya NATO na urusi huku silaha zao nyingi walikwisha maliza kwenye maghala maana yake wanatakiwa waingie kiwandani watengeneze zingine swali litakuwa nishati unapata wapi ya kuendeshea hivyo viwanda vya silaha???? Yaani wanunue gas ambayo ni angalia mara nne kutoka USA ili watengeneze silaha za kwenda kupigana Ukraine ππππ hata zezeta hakubali na hata wakifanya hivyo kufika salama gasi kutoka USA hadi ulaya itakuwa ngumu kutokana na usalama maana urusi hataruhusu hizo meli zifike ulaya atazilipua huko huko baharini
La nne kwenye kuchelewesha hii Vita ni kuwa mpaka sasa uchumi wa ulaya unapumulia mipira ICU Kwa hiyo mfadhiri mkuu wa Vita Kwa sasa ni USA yaani kiufupi marekani sasa hivi kaanza kuchapisha makaratasi yake Yale anayoyaita dollar ili aendelee kudhadhiri Vita Ukraine, na pia nadhani kutokana na uchumi wa ulaya kuwa vibaya nadhani kuna mataifa mengi wanakopa USA Kwa sasa Kwa hiyo kuongeza Kasi ya kutengeneza dollar
Lakini kuna kitu mrusi kakitegea vizuri tu wakati USA anaongeza uchapishaji wa pesa mrusi na washirika wake wanapunguza matumizi ya dollar, urusi wamepunguza uzalishaji wa mafuta hapa kinachoenda kutokea ni kuwa dollar tano ulikuwa unapata Lita tano mafuta basi Hali itabadilika itakuwa dollar tano unapata Lita tatu mafuta hii itasababisha kupanda Kwa bei ya bidhaa, hii pia itapelekea ili upate mafuta mengi itakubidi uwe na dollar nyingi hii itasababisha kuongezeka Kwa Kasi kutengeneza dollar, naona pigo litakalifata Kwa urusi na washirika wake kwenda wa Kwa west na marekani ni kusema kuanzia sasa mafuta hatuuzi Kwa dollar Ila Kwa yuan, au Kwa pesa za nchi husika ukija kuangalia kwenye mzunguko kuna trillion ya makaratasi ya dollar kwenye mzunguko lakini demand imepungua hapa ndipo natajionea mwenyewe marekani akipiga goti Kwa waarabu kuomba wasifanye hicho kitu
Kiufupi jinsi muda unavyokwenda ndivyo uchumi na ushawishi wa west na marekani unavyopotea duniani, TUNAMUOMBEA MWAMBA PUTIN ASIMAMIE SHOW MPAKA MWISHO SISI WENGINE TUTAKESHA KWENYE MAOMBI IWE KWA MUNGU AU MIZIMU LAKINI ADUI YETU NI MMOJA
Samahani maana imekuwa ndefu mtanisamehe WAKUU ππΎππΎππΎππΎ