Mkuu asante kwa kueleza. BAsi hapo juu uliandika "So sad CIA kill him." (yaani Hugo Chavez). Nilifikiri unarudia madai ya Maduro aliyetangaza Chavez alikufa kutokana na kansa na matatizo ya moyo, akishtaki CIA walimambukiza kwa virusi za kansa. Ilhali hakuongeza virusi ipi (maana virusi vya kansa viko aina tofauti) mimi naona alitangaza tu madai bila msingi - ambayo mimi naita propaganda, tena si propaganda nzuri.
Kama hujamaanisha madai hayo ya maduro, naomba radhi. Lakini sasa wewe unatakiwa kuthibitisha madai yako "CIA kill him!"
Karibu!
Mkuu, unataka kunambia maduro ni mjinga kwa kile alichokiongea cndio ety propaganda, bado inaonekana jinsi gany ulivyomweupe. Usichokijua nikwamba hugo chaves alijua kabisa lazma atakuja kuawa, na mauaji yake hayakuwa kwa bahati mbaya hata kidogo, kwasababu ulikua ni mpango wa marekani kupitia (CIA) kuwaua wanamapinduzi na wapigania uhuru duniani.
Nisiende mbali sana mfano ni kupitia lijasusi la marekani bill oxley aliyekiri kuhusika moja kwa moja na kifo cha marehemu Bob Marley, ambapo alimpa Bob Marley viatu aina ya raba kama zawadi, ambapo ndani yake kulikuwa na sindano ndogo sana yenye ncha kali ikiwa na vimelea vya ugonjwa wa kansa ambao ulipelekea kifo cha Bob Marley.
Usichokijua nikwamba CIA wanamiliki maabara nyingi sana za siri duniani ambazo wanatengeneza dangerous microbes kwa mashambulizi ya kijasusi ikiwemo assasination kwa watu na viongozi mbali mbali duniani wanaoweka obstacles kwenye interests za USA, wew hujiulizi ile maabara ya siri ya marekani iliyokua Ukraine, unadhani ilikua kwa bahati mbaya.
Au unadhani raisi wa urusi (Putin) na majasusi wake wa FSB walikua wajinga kupambana haraka na kitisho hicho kilichokua mbele yao tena cha hatari kwa raia wake na taifa kiujumla.
Kama unasubiria evidence yakuwa cia ndio waliomua basi hunatofauti na ambaye anakataa wanasayansi wa nuclear wa irani kuawa na mossad lengo akidhani kwamba ushahidi mpaka wakili hadharani kuwa wanahusika na mauaji hayo. Hivyo jitahidi sana mkuu kukonect doti nasio kusubiria kuletewa ushahidi, sababu siku zote penye ukweli uongo hujitenga.