Una ushabiki wa kitoto sana., unadhani vita ni kuwa na uwezo wa kupata silaha tu.., unafikiri hayo madini yanachimbwa tu kama unavyochimba muhogo?
Umeshajiuliza ghalama zinazotumika kuwatibu majeruhi wanaojeruhiwa huko front line Kwa mamia na maelf kila kukicha??
Umeshajiuliza vifaa vinavyoharibiwa (unrepairable) kila kukicha vina thamani kiasi gani?
Umeshajiuliza ghalama zinazotumika kufanya matengenezo ya zana za kivita zinazopata damage huko front line? Au unafikiri ni sawa na jinsi unavyofanya service ya IST?
Umeshajiuliza ghalama zinazotumika kwenye mapishi ya askari zaidi ya laki 5 walioko kwenye uwanja wa vita? Fikiria unavyoangaika kuihudumia hiyo familia yako ya watu wanne kisha ulinganishe kuwahudumia askari zaidi ya laki 5 walioko front line mchana na usiku kwa chakula Bora malazi, na vifaa vingine muhimu.., kumbuka asikari huwezi kumpikia kama unawapikia wafungwa gerezani..
Umeshajiuliza ghalama za pensheni zinazotumika kuwalipa wajane na yatima walioachwa na askari waliolambishwa mchanga kwenye uwanja wa vita?..,au unafikiri Hawa wanaachwa tu?
Wewe upo hapa kama shabiki tu lakini vita ni zaidi ya unavyoijua.., inashangaza unatuletea picha ya kiwanda Cha silaha kama udhibitisho kwamba urusi anaiweza vita..,
Sent from my Infinix X660B using
JamiiForums mobile app