LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hataweza kiuchumi.

Next week Iran na Venezuela wanaondolewa vikwazo vya kiuchumi na kuanza kuuza mafuta kwenye nchi za Ulaya.

Kama Iran watakubali basi Vikwazo vya Nishati kwa Urusi vitakuwa vikali kabisa,lakini kama wakikataa basi ni wazi Ulaya hawana mbadala wa mafuta ya Urusi kwa mda huu. Ndio maana wanaharakisha kuondoa vikwazo kwa Iran na Venezuela.

Kama Iran na Venezuela watakubali basi watakuwa wameisariti Urusi ambayo ilikuwa nao bega kwa bega pindi walipobanwa na vikwazo.
 
Gesi baba tatizo ni Gesi.....
Afu winter is Coming.
 
Wewe unaongea nadharia wakati mimi naongea ambacho kilifanyika juzi. Juzi shirika la International Atomic Energy Agency (IAEA) imefungua ofisi zake rasmi Tehran kwa ajili ya ukaguzi wa vinu vya nyuklia vya Iran kwa Masharti ya Iran kuondolewa vikwazo vyote vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani.

Mpaka sasa kilichobaki ni Marekani kwenda kusaini Mkataba. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ANTONY LINKEN amesema Next Week wanasaini mkataba mpya na Irani Joint Comprehensive Plan of Action (JCPOA).
 
Gesi baba tatizo ni Gesi.....
Afu winter is Coming.
Ni kweli,ndio maana wameanza mafuta. Leo Marekani imeweka vikwazo vya Mafuta kwa Urusi. Pia baada ya Iran na Venezuela kuingia Sokoni,EU wataweka vikwazo vya mafuta kwa Urusi. Marekani imetangaza nchi yoyote itakayonunua mafuta ya Urusi baada ya siku 90 itakutana na vikwazo vikali vya kiuchumi kutoka Marekani.

Pia,Marekani imeyatahadharisha Makampuni ambayo yanafanya biashara ya dhahabu na Russia kwani yatakutana na vikwazo vikali vya kiuchumi.
 
Irani ishaachia mlango wazi , waombeeni Russia , na bado resistance ya waukraine inazidi kuwa kubwa zaidi ..!!!
 
Hapa Russia tupumzishe kidogo kutudanganya,hii wape taarifa Warusi ambao hawana access ya kuona kinachoendela Duniani 🙂
Huyo jamaa hajadanganya kabisa labda haujamwelewa.

Jana Urusi na Ukraine waliweka Cease fire ili kuwaondoa raia wa Ukraine kwenye mji wa Maliopor ambao ni mji wa bandari unaoshambuliwa na Meli za kivita za Urusi zilizoko Black Sea. Baada ya raia kuambiwa kuwa wanapelekwa Russia wakagoma na CEASE FIRE ikaisha na mapigano yakaendelea.

Ukraine iliishambulia Meli ya Urusi Black sea kwa kutumia Drone ya Uturuki na kusababisha MAJOR DAMAGE. Hapo ndipo Urusi ikaanza kushusha mamia ya CRUISE MISSILES za Kutosha na kuisambaratisha AIRPORT YOTE.
 
Nipe hii clip nione
 
Rais WA Marekani Joe Biden amepiga marufuku ununuzi WA mafuta ya Urusi kuanzia Leo.

Today, I’m announcing that the United States is targeting a main artery of Russia’s economy.

We are banning all imports of Russian oil and gas.
 
Ndio maana wengine tunaiunga mkono Urusi sababu ya huu ubabe na uonevu wa Marekani.

Haya mnaosema Urussi kavamia nchi huru vipi na huyu Mmarekani anaezuia nchi huru kufanya biashara na Urussi

Tuombee Urussi afanikiwe hii operation ili dunia i balansi..

La sivyo Marekani atatushika tako sana tu.
Marekani amegundua anaenda kupoteza ushawishi duniani ameanza mikwara mapema tu.
 
BREAKING NEWS

Majeshi ya Ardhini ya Urusi yanakaribia kuuteka mji wa IRPIN. Raia waanza kuuhama mji huo. Jeshi la Ukraine limepeleka wanajeshi 200 kuzuia jeshi hilo la Urusi.
 
Kelele zimekuwa nyingi kwa utawala wa Biden hatimae leo ame sain excutive order kuweka vikwazo vipya na kuzuia ununuzi wa nishatj zoote hizo, Biden anasema wametoa mapipa m60 kwa ajili ya ku maintain soko la dunia. Naona kila kukicha mambo yanaumana tuu
 
Maduro atafaidi sana huu msimu... Siwaoni EU na Uk wakiban hii rasilimali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…