Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sio uzushi. Kh-22 Kitchen haina accuracy nzuri kwenye land attack. Primary ni anti ship missile na carrier killer design ya miaka ya 1960s, that time iko very advanced na ahead of its time. Ila sasa ziko store nyingi na kwa kuwa secondary attack capability ni land ambapo inapiga stationary targets basi Russia wakaitumia. Makombora mengine Kh family hasa yaliyotengenezwa na Raduga hayako supersonic kwa vile ni land attack. Meli inabidi uipige na kombora lenye uwezo mkubwa zaidi hivyo anti ship missiles ziko vizuri na hazizuiliki kirahisi na land based air defence systems.

Mkuu wa Air Defense wa Ukraine kasema hawajadondosha Kh-22 hata moja tangu zirushwe mamia vita hii yote. S-300 zote haziwezi idungua, ni air launched inapaa juu inakuwa supersonic kisha inakuja kwa kudondoka, tofauti na zile Kalibr zinazoenda horizontal unaweza detect iko Mbagala ukaipimia Kisarawe. Mpaka Patriot au SAMP/T ndio unaweza engage Kh-22.

Kinachofanya kuwe na makosa kuamini zimedondosha ni accuracy yake mbovu ardhini, inatumwa ipige kwa Mkapa inadondoka barabarani Temeke basi watu wanarekodi imekuwa intercepted ila jeshi baadae likipima debries wanakuta haikuwa intercepted. Taarifa yake inaeleweka kabisa
 
Kaongea mcha mbuzi kutoka buza.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Haya ndo mafunzo waliyopewa wanajeshi wa Ukraine kutoka kwa NATO na washirika wake.hakika ni moja ya mafunzo mazuri kuwahi kutokea katika uwanja wa vita.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]



Himars, T-24Armata, kipanya44, Axel [emoji1787][emoji1787][emoji1787] macho yenu yanaona kama mimi
 
Hiyo Bakhmut tangu mwezi May wanapigana kuichukua lakini mpaka Leo hawajaichukua,yaani karibu mwaka mzima wanapigana kuteka kamji kamoja.
Huko nyuma nilikupa credits sana kuwa unajibu huja kwa facts, kumbe nawe ni wale wale. Au ndio kipigo kimeingia kwenye mishipa??

Ni hivi hapo Ukraine iliweka nguvu kubwa sana, wanajeshi waliwekwa wa kutosha. Russia baada ya kuijua supply route ya hapo ndio maana umeona wameenda kwanza kuizika Soledar ili huo mji usipate supply yoyote ya vifaa vita pamoja na wanajeshi..
 
Hiyo mifereji warusi si ndo wabobezi,walichimba mifereji Kherson ila walichezea kichapo mpaka wakaacha mifereji yao wakakimbilia kando ya pili ya mto[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sawa ni Maoni yako lakini hayana mtiririko unaotizamia kufikisha ujumbe mmoja. Hata kama ni maoni yako ndio utupangilie shagalabagala namna hii!? What is your point!?

"Vladimir Putin ni somehow autocrat na kawaida yao huwa hawataki mtu popular zaidi yao

Putin hakuwa best candidate kuwa Rais wa Urusi

Chubais ni kiongozi mzuri ana reputation duniani

Yumanshev ndio alimpendekeza Putin awe mrithi na Yeltsin akakubali baada ya kujadiliana na watu wake wa karibu na wao kushawishika

Yeltsin alikuwa na possible candidates wake ni Boris Nemtsov, sergei Stepashin na Nikolai Aksenenko.

Jeshi halikupenda kabisa lilimjua alivyo

Putin anawaamini hawa watu wawili

Na kitendo cha Shoigu na Gerasimov kupendekeza Surovikin atoke kisha Gerasimov aongoze operation mwenyewe

Wagner wamechukia.

Prigozhin haziivi sana na General Gerasimov na Shoigu"

- Haya sio maoni ni madai. Una ushahidi!? Mafano, Unaweza kututhibitishia kwamba Prigozin na Shoigu na Gerasimov haziivi!?
 
Anapenda kujifanya anajua vitu vya ndani ya serikali za watu wakati yeye ni kapuku mmoja ambaye ana mbele wala nyuma[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Yani kandika sijui ujumbe,insha au barua ya kuomba kazi.yani akieleweki alichoandika.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hiyo Kh ikitumwa ikapige kwa mkapa inaenda 'kuangukia' temeke. Yaani Missile ikikosa shabaha inaenda kuanguka sehemu nyingine na sio 'kupiga' sehemu nyingine!?

Maajabu sio maajabu!

Hakuna namna watu achilia mbali hao wa ulaya hata sisi watz tunaweza kumistake missile iliyopiga sehemu isiyotakiwa kupiga (miss due to bad accuracy) na missile iliyokuwa intercepted. Unaposema kh haina shabaha hivyo ikitua pengine sio pale ilipolengwa iende kutua watu wanasema imekuwa intercepted ni uongo wa mchana kweupe!!!

Kombora likitumwa likapige uwanja wa taifa lenyewe likakosea shabaha likaenda kupiga hospital ya temeke huwezi kusema limekuwa intercepted. Not in a million years.

Taarifa ya mwanzo kwamba Ukr waliwahi kudungua/kuintercept makombora hayo jamii ya Kh ilikuwa ni taarifa ya kumbumba kama ilivyo taarifa nyingi zinazotoka Ukraine. Leo wenyewe wamejiumbua kumbe hawana AD inayoweza kuintercept makombora aina hiyo.

Unageuka kituko unapotaka kutetea taarifa hiyo. Ndio maana unaforce kombora lililokosa terget kuwa mistaken na kombora lolilokuwa intercepted. Huko ni kujifucha kwenye shamba la karanga
 
All over the map

Unasoma hadi katikati alaf unajiuliza anazungumzia nini!? Unarudi unaanza upya tena na tena

Mtu anaandika kbs Putin hampendi fulani anampenda fulani. How do you know that!?
 
Mpaka Sasa wapo zero kilometer kuingia Bakhmut.

Na Bakhmut yenye inazingirwa 75%

Kama kweli America ni super power basi aingie mwenyewe front
Leo niliona mwandishi mmoja wa habari Aljazeera akiwa Bakhmut alikuwa anawahoji baadhi ya wanajeshi wa Ukraine.

Aka-organize maelezo ya wanajeshi na kutoa analysis yake.

Kwamba, Wanajeshi wa Ukraine kwasasa wameingiwa na hofu kubwa kwny uwanja wa mapambano kutokana na hali ya Jeshi la Urusi kutengeneza mazingira ya kuwazunguka na kuwaweka kati.

[emoji3]yani propaganda za uongo wanazisambaza mpaka wanaamua kuyasema yenye uhalisia.

Ila kiukweli Ukraine hali sio shwari kwasasa, kashikwa mtu Kengele huko, ni mwendo wa kuchuchumia tuu.[emoji23]
 
Kwanza umeandika kwenye mtirirko mzuri sana big up ila Napingana nawe kwenye kutolewa sarovikin kwanza kama ulivyosema ni mtu makin na mkweli maana kama angekuwa general mwingine angeacha askari wake wapambane na kufa ili tu kufurahisha mamlaka ila kwa uwezo wake aliwatoa wanajeshi na kuachia eneo hadi upande wa pili wa MTo aya ni maamuzi magumu na makubwa sana hakujali kuusu media wala lawama.
Ila kushushwa kwake chini ya mtu naisi ni kujipanga kwa matuko ya mbeleni naona Russia amejitoa kwenye kucheza mziki wa ukrein maana toka mwezi wa 9 hadi wa 11 Russia walikuwa wanachezeshwa segere na kuachia maeneo mengi waliyonyakua ila kidogo mwezi wa 12 nimeona progress kubwa upande wa Russia naisi kumtoa ni kuweka akiba ya watu wao wa kuongoza hii vita maana ata wao wameipa hii vita kuendelea kwa kipindi kirefu na ukrein hayupo tayri kwa mazungumzo kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…