Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Leo niliona mwandishi mmoja wa habari Aljazeera akiwa Bakhmut alikuwa anawahoji baadhi ya wanajeshi wa Ukraine.

Aka-organize maelezo ya wanajeshi na kutoa analysis yake.

Kwamba, Wanajeshi wa Ukraine kwasasa wameingiwa na hofu kubwa kwny uwanja wa mapambano kutokana na hali ya Jeshi la Urusi kutengeneza mazingira ya kuwazunguka na kuwaweka kati.

[emoji3]yani propaganda za uongo wanazisambaza mpaka wanaamua kuyasema yenye uhalisia.

Ila kiukweli Ukraine hali sio shwari kwasasa, kashikwa mtu Kengele huko, ni mwendo wa kuchuchumia tuu.[emoji23]
Upo sahihi mkuu hata Mimi nimeona
 
Asante Mkuu Kwa kuniita. Nimeipitia hii habari yote ambayo ukumbuke habari hii imeandikwa December 16, 2022 at 1:00 a.m. EST. Toka tarehe hiyo Kuna mabadiliko kadhaa kwenye uwanja wa mapambano huko Ukraine.

Habari uliyotuletea Ina Tatizo ya kuwa na magepu mengi. Kwa ujumla imeandikwa kimkakati wa kihisia zaidi kuliko ukweli halisi ndiyo maana wameweka ushahidi ulio na mashaka ukiangalia mtiririko wa matukio na muda. Pia sehemu nyingine wanakwepa kuweka details muhimu za kuthibitisha tukio linalozumgumzwa.

Nitatoa mifano michache.


1. A Russian military medical file indicates that the 200th's commander, Col. Denis Kurilo, sustained head injuries on April 22. He was treated in July at a military hospital in Moscow.

(Juu ya maneno haya hapa chini huko kwenye link Kuna picha inayoonyesha gari lililolipuliwa na huyu Ndugu Kurilo kupata majeraha ya kitisha kiasi cha kupoteza kumbukumbu)

The aftermath of a strike that Ukrainian military officials said targeted the 200th around the time its commander was injured. Col. Denis Kurilo was eventually hospitalized. (Ukrainian government)

Wording at the top of the document indicates that it was to be approved on May 28 by Kurilo, suggesting that he was still with the unit despite his recent injury. A medical file in the trove, however, indicates that he was suffering severe symptoms from a “craniocerebral injury,” including nausea, vomiting, memory loss and “short-term disorientation.” It says he left the unit on July 11 to be treated at Burdenko military hospital in Moscow and was released in late August. The medical file also says his duties were temporarily assigned to another officer( Yaani Kamanda apate majeraha Yale bado aendelee kukaa field huku akiongoza kikosi kwa karibu miezi mitatu? Hivi mnatuonaje lakini?).

2. May-July
Withdraws from Ukraine to regroup in Valyuki. A “mixed volunteer” force is formed in Pechenga and sent to replenish brigade after heavy losses.
===
Ngoja niishie hapa kwanza.
 
Leo niliona mwandishi mmoja wa habari Aljazeera akiwa Bakhmut alikuwa anawahoji baadhi ya wanajeshi wa Ukraine.

Aka-organize maelezo ya wanajeshi na kutoa analysis yake.

Kwamba, Wanajeshi wa Ukraine kwasasa wameingiwa na hofu kubwa kwny uwanja wa mapambano kutokana na hali ya Jeshi la Urusi kutengeneza mazingira ya kuwazunguka na kuwaweka kati.

[emoji3]yani propaganda za uongo wanazisambaza mpaka wanaamua kuyasema yenye uhalisia.

Ila kiukweli Ukraine hali sio shwari kwasasa, kashikwa mtu Kengele huko, ni mwendo wa kuchuchumia tuu.[emoji23]
Nimekuelewa boss, umeleta habari source ikiwa aljazeera na ww ni Pro Russia ss umekwepa mtego fulani hivi kuhusu kuziamini western media.
 
Leo niliona mwandishi mmoja wa habari Aljazeera akiwa Bakhmut alikuwa anawahoji baadhi ya wanajeshi wa Ukraine.

Aka-organize maelezo ya wanajeshi na kutoa analysis yake.

Kwamba, Wanajeshi wa Ukraine kwasasa wameingiwa na hofu kubwa kwny uwanja wa mapambano kutokana na hali ya Jeshi la Urusi kutengeneza mazingira ya kuwazunguka na kuwaweka kati.

[emoji3]yani propaganda za uongo wanazisambaza mpaka wanaamua kuyasema yenye uhalisia.

Ila kiukweli Ukraine hali sio shwari kwasasa, kashikwa mtu Kengele huko, ni mwendo wa kuchuchumia tuu.[emoji23]
Bora wewe naona unajaribu kuleta habari njema kwa warusi wa buza japo kwa kubumbabumba[emoji23]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Nimepitwa na mengi kwa hii wiki ila ngoja nirudi nyuma miaka kadhaa. Sianzishi uzi, tunaishi humu humu naleta gazeti.

Vladimir Putin ni somehow autocrat na kawaida yao huwa hawataki mtu popular zaidi yao. Si jambo la ajabu kwao kuvumilia kiongozi mwandamizi mwenye uwezo wa kawaida na makosa madogo madogo lakini mtiifu kuliko maelezo. Wanakuwa wagumu kuendana na mtu mwenye uwezo mkubwa, msimamo, mkweli na bold, akiwa hivyo atakuwa popular na ni kosa kwenye medani kwa vile authoritarians hutaka kukaa muda mrefu madarakani na kuwa undisputed. Never outshine your master.

Viongozi wa wa wastani wanajitahidi kuwa watiifu kuliko kuwa watendaji wazuri. Na wanadumu katika nyadhifa zao, wanalindana wale wababaishaji na hawapendi kuona kiongozi smart sana au mnyoofu baina yao, hawezi vumilia ujinga wao na atawazidi kupendwa.

Putin hakuwa best candidate kuwa Rais wa Urusi, kipindi Yeltsin anataka kuachia madaraka alimtaka bold leader asiyebabaisha maana nchi ilimshinda kwa namna fulani. Aliondoka kizalendo angeweza kung'ang'ania kwani alishapitia Black October akalishinda Bunge kwa kutumia jeshi kisha akabadilisha katiba. Hata hivyo alitaka mtu wa kulinda maslahi yake na oligarchies, watu bold waliokuwepo hawakupendwa na oligarchies na hawakuwa na strong 'connection' serikalini. Kwao ilikuwa ni hatari kukabidhi nchi kwa asiyejua taratibu za kihuni za wanaonufaika.

Valentin Yumashev alikuwa mshauri mwaminifu kwa Yeltsin na alimuoa Tatyana, binti wa YeltsinView attachment 2485041
Anatoly Chubais (pichani) mchumi aliyemshauri Yeltsin afanye privatisation iliyowatoa oligarchies ndio alimpendekeza Putin kwa Yumanshev wakati anamuachia ngazi cheo cha Chief of Staff. Hapo maafisa wengi wa KGB/FSB waliondoka taasisi ilipopungua umaarufu na majukumu, ndio kama akina Putin wakaenda kwenye siasa kuwa naibu meya St. Petersburg. Putin akawa anakubalika na Katibu Mkuu mstaafu na aliyepo, na akawa na background nzuri ya KGB. Picha ni Yeltsin na PutinView attachment 2485044
Chubais ni kiongozi mzuri ana reputation duniani, amekuwa kwenye bodi nyingi za makampuni na ametumwa na Urusi kwenye majukumu kadhaa ya kimataifa, alikuja kukimbia nchi mwaka jana Russia ilivyovamia Ukraine. Yuko kinyume na vita kwa mtazamo wa kiuchumi, anajua umafia wa serikali hivyo aliamua kutoroka na aliweza kwa namna gani, hatujui.
Yumanshev ni mkimya.

Yeltsin alikuwa na possible candidates wake ni Boris Nemtsov, Sergei Stepashin na Nikolai Aksenenko.

Nemtsvov aliwahi kuwa Makamu Waziri Mkuu cheo alichopitia Chubais kabla ya kuwa Chief of Staff (Russia hakuna makamu wa Rais tangu jaribio la 1991, Waziri Mkuu alikuwa na makamu wake).
Nemtsvov aliuwawa 2015 kwa risasi akiwa darajani, alikuwa anapanga maandamano kupinga Russia kuivamia Ukraine na uchumi mbovu. Ndio alikuwa mpinzani mkuu wa Putin. Huyu hakupendwa na oligarchies kabisa kuwa mrithi wa Yeltsin, alikuwa mkali na amenyooka.

Sergei Stepashin ndio alikuwa Waziri Mkuu kabla ya Putin, huyu alikuwa mwaminifu kwa Yeltsin ila sio mtu sahihi wa kuokoa jahazi. Yupo ametulia hana headlines. Nikolai Aksenenko alikuwa Waziri ila Putin akamfuta kazi baadae kidogo. Nadhani performance yake haikuwa nzuri.

Yumanshev ndio alimpendekeza Putin awe mrithi na Yeltsin akakubali baada ya kujadiliana na watu wake wa karibu na wao kushawishika. Hapo kumbuka 1997-98 Putin alikuwa mkuu wa FSB then 99 akawa Waziri Mkuu na Yeltsin akamuachia madaraka.

Fast forward, 2008 Russia ikavamia Georgia jirani yake na former Soviet Union kama yeyeView attachment 2485045
Utaratibu ni uleule kama wa kupanga misururu ya magari na kulipua miji, ndio uleule utaratibu wa Syria. Ndio maana General Armageddon anapolaumiwa kufanya vile Ukraine nikasema ndio utaratibu wao hata awe mwingine atafanya hivyo. Performance ya Russia ikawa mbaya vitani na Georgia kanchi kadogo.

Mwaka kabla ya Georgia, Putin alishagundua jeshi lake lina matatizo makubwa akamuamisha Anatoly Serdyukov kutoka Waziri wa Kodi kuwa Waziri wa Ulinzi alimuelekeza apambane tu na rushwa na innefiency ya jeshi. Jeshi halikupenda kabisa lilimjua alivyo, mkuu wa General Staff wa jeshi wakati ule akasema Serdyukov anabidi akae ofisini mwezi mmoja wamfundishe kazi, Serdyukov akaandika barua ya kujiuzulu ila Putin akaikataa, kabla hajakataa mkuu wa General Staff alishatoa na maoni kama ni hivi Waziri ajaye hata akiwa mwanamke.

Serdyukov alianzisha audit kali baada ya kuwachukua watu kadhaa Wizara ya Kodi na kuwaleta afanye nao kazi, akakuta maofisa wameiba fedha za bajeti, tenda wanatoa hovyo, makampuni ya silaha yanadanganya specifications, wakaguzi wanahongwa na mambo mengine. Akaenda mbali akaweka mazoezi ya mwili kila mwanajeshi apite na asiwe na kitambi, maofisa kibao wakafeli ikawa gumzo kwenye media. Akaanzisha utaratibu bajeti haiguswi na ofisa, inajadiliwa na kitengo kipya cha bajeti ambacho sio wanajeshi maana alikuta fedha zilizotolewa ni nyingi miaka mfululizo ila kilichofanyika hakiendani (early 2000s mafuta yalipanda na Russia ikapata hela nyingi, bajeti ya ulinzi ikapanda). Baadae 2012 Putin akamtoa Serdyukov akamleta Sergei Shoigu kutoka Wizara ya Dharula. Serdyukov alifanya kazi yake ila asingeweza kubaki pale juu ya popularity, kuchukiwa na maofisa wa jeshi, ila kupendwa na wanajeshi wa kawaida. Na hapo akapatikana General Valery Gerasimov kama Chief of Staff wa jeshi, huyu alipata umaarufu vita ya Chechnia miaka ya 90s.

Sasa vita hii, Sergei Shoigu kadumu kwenye teuzi za Putin tangu late 1990s mpaka leo, huyu anajua fika nini Putin anataka. Sio popular, hapendi siasa, sio asili superior ya Warusi (kila nchi ina kaubaguzi ndani kiasi chake). Gerasimov kakaa tangu 2012 mpaka sasa, anajua Putin anataka nini na hasumbui, haijalishi anafanya vizuri au sio. Gerasimov ana miaka 67 anastaafu lini sijuiView attachment 2485046

Putin anawaamini hawa watu wawili, mwanzo operation ilianza vibaya (in military view ile ni blunder). Media ziko controlled ila social media Gerasimov na Shoigu wanalaumiwa sana kwa incompetency yao. Kwangu naona Gerasimov sio mbaya ila Shoigu ndio sio mzuri kivile. Baadae October 2022 akachaguliwa S.V Surovikin, huyu ndio the best kwa majenerali wao, nilisema siku amechaguliwa na nitaendelea kuamini hivyo. Ghafla wakati mambo yanaenda sawa, akaondolewa kusimamia operation. Normally, you don't change a General when everything is going accordingly, nakataa theory wanayoshika pro Russians wengi kwamba Surovikin kamaliza task yake hivyo anakuja mwingine. Task ipi imemalizika?

Na kitendo cha Shoigu na Gerasimov kupendekeza Surovikin atoke kisha Gerasimov aongoze operation mwenyewe nakitafsiri kama hawa wawili hatua hii wanajua plans zao na wanaamini operation inaenda kufanikiwa hivyo wanaiba mafanikio kwa Surovikin, technical wivu. Hata hivyo naona ni hatari kama matarajio yao yatakuwa kinyume watabeba lawama.
Surovikin anakubalika na kila mtu kuanzia wanajeshi wadogo, media, social media, veterans, Kadyrov wa Chechnia na Prigozhin wa Wagner PMC.

Nimeanzia story mbali ili kuunganisha matukio. Putin anapenda mbishane ukouko chini yeye yuko juu anajua atakachofanya. Hapendi kukaa na watu wanaelewana wote, na hapendi kukaa na mtu maarufu (viongozi wa Russia na USSR wote walikuwa hivi). Na pengine anampima Surovikin uvumilivu wake ashajua uwezo wake, amemshusha. Naamini atamteua kuwa mrithi wa Gerasimov kama atataka mtu smart, akitaka ndio mzee Surovikin sijamuona kama yuko vile sana kwanza ni competent na pia ni mkweli. Reports kadhaa alizofanya live alionyesha kuadmit baadhi ya vitu wenzake walikuwa na kigugumizi kukubali.

Sergei Prigozhin naye ana matatizo yake na Wagner yake. Hayuko chini ya MoD ila anapewa silaha nao, offensive ya Soledar wamefanya Wagner ila MoD inataja jeshi kwenye mafanikio, Wagner wamechukia. Prigozhin haziivi sana na General Gerasimov na Shoigu. Natafsiri kwamba utaratibu wa Putin unaendelea, pambaneni ukouko msiungane dhidi yangu.

NB: Haya ni maoni yangu. Ni very honest kama una utimu shauri yako
Gen Gerasimov ni kama CDF kwa huku kwetu.

Watafiti wa mambo wanasema kwamba, kitendo cha Putin kumteua Gen Gerasimov kinaonyesha kwamba hii inaenda kuwa vita kamili ambayo inahitaji coordination ya Joint Chief of Staff, ambayo huyo Gen Gerasimov ndiye mwenyekiti wake.

Kuhusu huyu Gen Armageddon yeye hajashushwa cheo, ila amepandishwa kama maana sasa hivi amekuwa ni Deputy wa Gerasimov.

Special Military Ops inakuwa na limitations nyingi na inamlazimu mara kwa mara huyo Gen Armageddon awe anaomba ruhusa kutoka huko Joint Chief of staff, sasa hii inapelekea kuwe na slippage kwenye operations.
 
Nikiwatakia wakati mwema, naomba niwaache na hasara aliyolamba super pawer wa kuchonga mpaka Sasa
1673981652130.jpg


Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Anapenda kujifanya anajua vitu vya ndani ya serikali za watu wakati yeye ni kapuku mmoja ambaye ana mbele wala nyuma[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Yani kandika sijui ujumbe,insha au barua ya kuomba kazi.yani akieleweki alichoandika.[emoji23][emoji23][emoji23]
Ukipunguza kutumia emoji za kuchekacheka itakufanya uonekane wa maana sana. Kama najifanya najua na wewe ni kilaza hamna shida kila mtu kachagua fungu lake
 
Kwa hiyo Kh ikitumwa ikapige kwa mkapa inaenda 'kuangukia' temeke. Yaani Missile ikikosa shabaha inaenda kuanguka sehemu nyingine na sio 'kupiga' sehemu nyingine!?

Maajabu sio maajabu!

Hakuna namna watu achilia mbali hao wa ulaya hata sisi watz tunaweza kumistake missile iliyopiga sehemu isiyotakiwa kupiga (miss due to bad accuracy) na missile iliyokuwa intercepted. Unaposema kh haina shabaha hivyo ikitua pengine sio pale ilipolengwa iende kutua watu wanasema imekuwa intercepted ni uongo wa mchana kweupe!!!

Kombora likitumwa likapige uwanja wa taifa lenyewe likakosea shabaha likaenda kupiga hospital ya temeke huwezi kusema limekuwa intercepted. Not in a million years.

Taarifa ya mwanzo kwamba Ukr waliwahi kudungua/kuintercept makombora hayo jamii ya Kh ilikuwa ni taarifa ya kumbumba kama ilivyo taarifa nyingi zinazotoka Ukraine. Leo wenyewe wamejiumbua kumbe hawana AD inayoweza kuintercept makombora aina hiyo.

Unageuka kituko unapotaka kutetea taarifa hiyo. Ndio maana unaforce kombora lililokosa terget kuwa mistaken na kombora lolilokuwa intercepted. Huko ni kujifucha kwenye shamba la karanga
Ukiambiwa hata wewe mwenyewe usome hapa huwezi jielewa. Umeandika:

"Kwa hiyo Kh ikitumwa ikapige kwa mkapa inaenda 'kuangukia' temeke. Yaani Missile ikikosa shabaha inaenda kuanguka sehemu nyingine na sio 'kupiga' sehemu nyingine!?"

Ndio umeuliza nini hivyo?

Ukraine hawajajiumbua, wametoa taarifa sahihi na clarification. Haya mambo huwezi yaelewa kama unaamini kwenye nguvu za superpower ambaye last week alitangaza kuharibu silaha ambazo hazijafika hata Ukraine.

Hizo missiles zilizokuwa zinapiga playground ndio walizielekeza hivyo. Hata kama hujui, si utumie common sense?
Unataka kusema Russia ni ngumbaru kupiga uwanja wa kuchezea watoto? Yani superpower ana makombora ya kupigia viwanja vya watoto vikiwa na majani pekee ila anaacha military facilities?
IMG_20230117_220706.jpg
 
Sawa ni Maoni yako lakini hayana mtiririko unaotizamia kufikisha ujumbe mmoja. Hata kama ni maoni yako ndio utupangilie shagalabagala namna hii!? What is your point!?

"Vladimir Putin ni somehow autocrat na kawaida yao huwa hawataki mtu popular zaidi yao

Putin hakuwa best candidate kuwa Rais wa Urusi

Chubais ni kiongozi mzuri ana reputation duniani

Yumanshev ndio alimpendekeza Putin awe mrithi na Yeltsin akakubali baada ya kujadiliana na watu wake wa karibu na wao kushawishika

Yeltsin alikuwa na possible candidates wake ni Boris Nemtsov, sergei Stepashin na Nikolai Aksenenko.

Jeshi halikupenda kabisa lilimjua alivyo

Putin anawaamini hawa watu wawili

Na kitendo cha Shoigu na Gerasimov kupendekeza Surovikin atoke kisha Gerasimov aongoze operation mwenyewe

Wagner wamechukia.

Prigozhin haziivi sana na General Gerasimov na Shoigu"

- Haya sio maoni ni madai. Una ushahidi!? Mafano, Unaweza kututhibitishia kwamba Prigozin na Shoigu na Gerasimov haziivi!?
Umejuaje nataka kufikisha ujumbe mmoja?
Una uhakika nimepanga shaghala baghala. What if hujaelewa au umekaza kichwa. Na mbona umejua kutoa summary tena kwa mtiririko, hata kuficha unafiki umeshindwa. Shaghala baghala ila umejua ku-summarize.

Unauliza what's my point na umesoma mwanzo mwisho. Si ungeachia njiani sasa, umesoma na hujaelewa unauliza nikueleweshe kwa voice note au video?

Kama hujui hiyo ndiyo taarifa yako sasa. Tena sio Prigozhin, hata Kadyrov haziivi. Hata pro-Russian channels zinasema, hata bloggers wenu maarufu wanasema. Telegram channels kibao hizo taarifa zipo. Unataka ushahidi tafuta
 
Kama kweli ni mshabiki muelewa huwezi kuipuuza uingereza kwenye uwezo wa medani kiasi cha kutoa field martial sio mchezo. Historically, british ndio ya kwanza kutumia tanks kwenye uwanja wa medani, mifumo na miundo ya majeshi include tz ni copy ya uingereza. Kuja kwenye point, hapa mkuu wa majeshi anatoa rai kwa serikari kuboresha jeshi katika kipindi hiki cha uvamizi wa russia ukraine
Ndio maana mnapotea
Historically Uingereza hio hio iliwahi kua taifa kubwa kabisa DUNIANI kwenye angle zote KISIASA KIJAMII KIUCHUMI nk
Leo hana sifa hata moja kwenye hizo nilizokutajia kabakia na epl tu
Maisha na mambo yanabadilika achaneni na mambo za historically
Hao UK leo wanalia lia msaada tu wanasema jeshi litakua dhaifu
RUSSIA anakaribia mwaka sasa ila silaha zake zinaisha CNN BBC FOX nk
Kwasasa UK nitaifa lakulipuuza tu nabila yakua kwenye NATO lisingesikika mpaka kwa epl

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom