LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Kama kweli Ukraine kaua wanajeshi zaidi ya 1,000 wa Russia (nawe waamini!) si ndio raha kwa Ukraine na Wamarekani wa JF, sasa sio muendelee kulialia. Tulieni kazi iendeleee...

Russia anaendelea kuingia zaidi Kyiv kwa mujibu wa taarifa toka Uingereza.

 
Daaah jamani😪😪😪 , hii video inatisha, wakae mezani amani ipatikane jamani.
Ukisikia vita hata iwe ya mapanga, ni mbaya sana. Nawashangaa humu ambao huwa wanabishana kana kwamba vita ni soka.

Labda kwa sababu hatujawahi kuonja machungu yake. Mungu awasaidie hawa watu kumaliza hili suala. Tuendelee kuwaombea
 
Raisi wa Urususi Vladimir Putin leo katika hotuba yake iliyokuwa mubashara katika vyombo vya habari ameliambia jeshi la Ukraine itakuwa rahisi kuanza mazungumzo nao tofauti hicho kikundi Cha majambazi (Nazis) na wasikubari kuwaruhusu waasi kuja kuwatumia vibaya na watoto wao wazee na raia wa UKRAINE Kama ngao yao
 
Hivi vyombo vya habari wa kimagharibi mara zote zimekuwa na kazi ya kiwatoa bongolala kwenye attention.

Acheni propaganda, tupeni taarifa za kinachoendelea kwenye battle field. Russia hajavamia Ukraine akitegemea msaada wa China, ninachojua ametoa angalizo kwa kiherehere yoyote atakaejaribu kumuingilia na ndiomaana huoni mjinga yoyote akijipendekeza.
 
Tuzidishe tu maombi sana ili pasitokee WWIII ili tuweze kula kwa urefu wa kamba zetu tukinenepeana mashavu kama chempazee.
 
Hapa anataka kudivide and rule
 
Nasikia korea kaskazini wamesema watamuung mkono urusi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli Urusi ina Nguvu kubwa Sana za Kijeshi Tena Sana. Lakini hawezi hata siku moja kuthubutu kutumia kombola la Nyuklia kwenye Vita. Kombola la Nyuklia ni kwa ajili ya Duterrence(Kutishia). Kinachosababisha mpaka Sasa NATO washindwe Kuingia vitani kuisaidia Ukraine ni kwasababu Russia ana Nyuklia Waepons ambazo zikitumika Basi NO WINNER,All are LOSSERS.

Urusi ina Makombora 7500 ya Nyuklia kwa takwimu za NIT. Makombora 2500 yako tayari kufyatuliwa kuelekea Endeo lolote Lile Duniani litakapotumwa. Marekani ina Miji mikubwa 358 na Majimbo 54. Kombora Moja linaugeuza mji kuwa Majivu kabisa. Kama Mrusi akituma Makombora yote 2500 kuelekea Marekani,Basi ndani ya dakika 30 hakutakuwa na USA Duniani.

Kwa Upande Mwingine,Marekani ina Makombora ya Nyuklia 6800. Kati ya hayo, 3500 yako tayari kufyatuliwa ndani ya Dakika 5 wakipokea Order na Direction ya kuyafurumusha. Urusi ina Miji mikubwa 43. Endapo USA akiona Russia kashatuma Makombora Yake kuelekea Marekani na hakuna jinsi Basi ndani ya Dakika 5, Makombora 3500 ya Marekani yatakuwa njiani kuelekea Urusi kuteketeza Miji 43,Ndani ya Nusu saa hakutakuwa na Urusi Tena. Hiyo inaitwa MUTUAL ASSURED DESTRUCTION(MAD).

Haya Sasa,Tuseme wewe ni Raisi wa Russia,utarusha hayo Makombora kuelekea Marekani au utafanya juhudi za majadiliano?

Mwishoni mwa Vita baridi kabisa (1988) Nchi za Marekani na Urusi Zilikuwa na Akiba ya Makombora 127,000 (Laki moja na elfu ishirini na Saba). Kati ya hayo, 58,000 ya Urusi na 69,000 ya USA. Embu fikilia. Kombora Moja linafuta mji mmoja wa Dar. Je,Dunia ina Miji 127,000? Jibu ni Hapana.

Kwahiyo ndugu yangu usiwe na tempa unapokuwa unachangia hizi maada,tumia Logic utaelewa tu.

Urusi na Marekani wanajuana,wakikutana Anga Furani Kila mmoja anaangalia Nani anamaslahi makubwa na anamwachia ili kuepusha Vita.

Georgia Mwaka 2008 Marekani hakuingiza mguu kusaidia Nchi hiyo dhidi ya Uvamizi wa Russia kwasababu Marekani anajua hapo Russia ana maslahi Makubwa.

Iraq mwaka 2003 Russia hakutia Mguu kwasababu Marekani alikuwa na Maslahi Makubwa.

Libya mwaka 2011 Russia hakutia Mguu kwasababu USA alikuwa na Maslahi Makubwa.

Venezuera Marekani aliogopa Msululu wa wakimbizi kumiminika nchini Marekani hata Kama angeliamua Vita Urusi angelipisha Coz pale ni Maslahi Makubwa ya kiusalama kwa USA.

Syria pale Wote Urusi na USA wanamaslahi na ndio maana mpaka Sasa wameigawana kijanja. Urusi inamhitaji Assad kwasababu Anamdai pesa ndefu. Marekani anahitaji Mafuta ndio maana mpaka leo Majeshi ya Marekani yapo Syria kulinda Visima vya Mafuta.

Kuhusu Ukraine,hata Marekani anajua kabisa Maslahi ya Urusi ni Makubwa kwahiyo lazima akae pembeni. Atashiriki tu kijanja lakini sio moja kwa moja.

Kuhusu NORTH KOREA,Yeye Ana Mabomu 10 TU ya Nyuklia kwahiyo hata akiacha atupe Mabomu yake Marekani atateketeza Miji 10 ya Marekani Kati ya 358. Kwa upande mwingine,NORTH KOREA ana miji 7 Mikubwa. Marekani akituma Makombora Yake ya Nyuklia 3500 nadhani unaona kabisa Makombora Mengine hayana pa Kupiga kabisa.

MTz 255Dar.
 
Haya sasa NATO hao wanaingia Astonia (NATO's member country) nchi inayopakana na Urusi. Mkuu wa NATO amesema Urusi ikiishambulia tu mwanachama yeyote basi wao hawatasita kuingia rasmi kwenye vita maana vikosi vyote viko standyby
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…