Kwanza Algeria haihitaji msaada wa Urusi wala Iran kufanya intervention hapo Niger. Hakuna jeshi la kuizuia Algeria hapo ECOWAS hata wakijumlisha uwezo wao wote na Nigeria ikiwemo. Algeria ina jeshi kubwa la kisasa, mpinzani wake wanayechukiana sana kwa majirani hapo ni Morocco naye yuko vizuri na makini.
Pili, Algeria sijaona popote ambapo imeunga mkono serikali ya kijeshi ya Niger, mara ya mwisho nimeona FM wao anatoa kauli ya kutaka peaceful and civilian means na hakuna dalili wanatetea mapinduzi. Hiyo statement ya kwamba wataunga mkono utawala wa kijeshi inazushwa na Waafrika wanaodhani ama Urusi, Ufaransa ama Marekani inahangaika kwa ajili ya maslahi ya Afrika. Na hao wazushi ndio walewale walisema Burkina Faso imezuia uuzwaji wa Uranium kwa Ufaransa wakati B. Faso haina hata ores na haijawahi uza U kwa Ufaransa.
Kilichopo hapa ni kwamba Russia kupitia Wagner inataka kuondoa influence ya France kwa Afrika. Since 2020 kuna mapinduzi mara 9 yamefanyika. ECOWAS wameona mapinduzi ni mengi na wale maraisi wameamua kutishia majeshi yao kwamba mkifanya mapinduzi ECOWAS itawajia. Wanamapinduzi wanaijua ECOWAS ilivyo effective wameamua waungane mkono kuteteana sababu wote hao B. Faso, Niger na Mali hakuna majeshi ya maana pale, so kama ECOWAS ingeanzia Niger ingeweza kufuata hao wengine.
Wagner inaongezewa majukumu Afrika kuifanya busy na sababu huku ni kwepesi. Russia ina control kubwa ya fuel rods za nuclear reactors duniani hivyo inataka kubana hapo Niger flow inayoenda Ufaransa isiende. Hata hivyo Niger inauza 5% ya Uranium duniani, na mteja wake mkubwa ni Ufaransa. Na wakati huo Russia inajitosheleza kwa U hivyo haitokuwa mbadala wa Ufaransa kwenye ununuzi. Anayenufaika hapa ni Russia, wanaoumia ni France na zaidi zaidi Niger.
Ikitokea confrontation kweli, ECOWAS inaweza wadhibiti wote hao kama itakuwa na dedication ila it seems hata Nigerian officers hawapendi hiyo mission na ndio jeshi lao linategemewa. Uamuzi wa kisiasa wa Tinubu kuzima mgogoro wa uchaguzi kwake ndio unamtuma atake kupeleka jeshi Niger sababu hawatoweza mbadilisha akiwa vitani.
Wagner ya Afrika haina silaha za kutosha na wapiganaji, hapo Libya ndio wana silaha nyingi zaidi ila napo huwa wanapigwa na majeshi yanayoungwa mkono na UAE na Uturuki. Uko kwingine wanaishia kumlinda Rais, ofisi mbalimbali na kufundisha, wakitoa silaha kubwa basi ni MANPADS. Unless Wagner wakiongeza nguvu, sioni wataletaje upinzani dhidi ya ECOWAS armed with French & US intelligence.
Huu mgogoro utaiumiza zaidi Afrika, umalaya wa kisiasa haiwezekani wenzetu wanapigana sisi kiherehere kujihusisha na ugomvi wao. Afrika tunapigana miaka mingi ila Ulaya pale wanaishi maisha yao.
Ikiwepo vita hii na wahusika wote hapa wakawepo, itajirudia kama vita ya Biafra, USSR na Uingereza zote ziliiunga mkono Nigeria ila hasara waliyopata Nigeria hawatokaa wasahau hata kama walishinda kwa mbinde. Na mikataba ya chuma na mafuta waliyosaini wapewe silaha, na mikopo waliyopata vita ile. Afrika akili zimelala