Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Three Soldiers Who Destroyed 32 Ukrainian Tanks Awarded Hero of Russia & Gold Star Medals​




Several Russian army officers received prestigious awards from Russian Defense Minister Sergei Shoigu on Friday after units under their command recently destroyed nearly three dozen pieces of Ukrainian armor.
“The exploits of many of you were seen not only by the whole country, but also by almost half the world. I congratulate you on these high awards. I wish you that in the future, firstly, your awards will not be the last,” Shoigu said. “Secondly, you continued to defend our Fatherland with dignity, no matter where you were, on what fronts and in what positions
 
Ukraine wanachekesha sana. Mkuu wa majeshi anadai vita imekwama hawawezi kusonga mbele na counter offensive haijafanikiwa chochote cha maana ila Zelenskyy anakataa na kudai wanaendelea vizuri. Jackal hapa tumuamini Zaluzhn mwanajeshi au Zelensky mwanasiasa?
 
Hii Vita haiwezi kutoa mshindi wa kijeshi moja kwa moja.

Mazungumzo hayaepukiki
Ha ha haa.
Naona unapata taabu kuukubali ukweli ndugu.
Ukweli usiopingika Ukraine ilishashindwa siku nyingi TU.
Ni USA na vijinato vyake ndivyo vilivyojidai kurefusha vita.
Sasa USA na vijinato vimeona Ukraine inazidi kupoteza watu na mwisho wa siku haitakua na manpower ya kutosha kuendelea kukabiliana na might Russia.
Vimejaribu kuingiza silaha weee huko Ukraine lkn zote zinaishia kuteketezwa.
Vimepeleka Hela weee Hadi wabunge wa USA wamekasirika.
Hivyo basi njia iliyobki ni kumuamuru mtu wao zelensky arudi kwenye meza ya mazungumzo na might Russia.
Mazungumzo na Russia maana yake zelensky aombe kurudishiwa maeneo yake kwa njia ya mazungumzo,maana kwa mtutu imeshashindikana.
Je mpaka hapo wewe huoni kama Urusi ndio mshindi?
Kwa hiyo rafiki yangu Proved Russia ndio mshindi wa vita hii.
Ukraine yeye anapambana kumuondoa Urusi katika maeneo yake.

US and Europe in Talks With Ukraine on Possible 'Peace Deal' With Russia - Report​

2 hours ago



As Kiev flounders with its counteroffensive, political support for propping up the Volodymyr Zelensky regime gradually wanes in some US political circles; meanwhile, Israel’s war on Hamas takes center stage, prompting speculation as to how swiftly Ukraine fatigue will gather momentum, and what it may spill out into.
Quiet conversations are already reportedly taking place between US and European officials on the one hand, and the Ukrainian government on the other, about possible peace negotiations with Russia.
 
Marekani na Ulaya Ziko katika Mazungumzo na Ukreni kuhusu Uwezekano wa ^Makubaliano ya Amani^ na Urusi

Wakati Kiev ikiyumba kwenye harakati zake za mashambulizi-pinzani, uungwaji mkono wa kisiasa ili kuutegemeza utawala wa Volodymyr Zelensky unapungua polepole katika baadhi ya makundi ya kisiasa Marekani; wakati huohuo, vita vya Israeli dhidi ya Hamas vinachukua hatua kuu, vikizua uvumi kuhusu haraka kiasi gani uchovu wa Ukreni utashika kasi, na nini ambacho kinaweza kuwa matokeo yake.

Mazungumzo ya kimya-kimya tayari yanaripotiwa kufanyika kati ya maafisa wa Marekani na Ulaya kwa upande mmoja, na serikali ya Ukreni kwa upande mwingine, kuhusu uwezekano wa mazungumzo ya amani na Urusi.

Majadiliano hayo yamegusia maafikiano ambayo pengine Ukreni ikahitaji kukubaliana nayo iwapo makubaliano yoyote hayana budi kuwezekana, kwa mujibu wa maafisa wakuu wa sasa na wa zamani wa Washington waliotajwa katika ripoti fulani ya Marekani.

Mkutano wa wawakilishi kutoka mataifa zaidi ya 50, wakiwemo wanachama wa NATO wanaounga mkono utawala wa Kiev, wajulikanao kama Kikundi Washirika wa Kuihami Ukreni, uliofanyika mwezi Oktoba, unadaiwa kwamba ndio ulitumika kama mahali pa baadhi ya mazungumzo haya ^makini,^ kulingana na ripoti hiyo.

^...Kuna hisia inayoshamiri kwamba mambo yamechelewa sana, na huu ndio wakati wa kufanya makubaliano,^ afisa mkuu mmoja wa zamani wa Washington alinukuliwa akisema hayo.

Kuhusu kwa nini mazungumzo haya yamekuwa yakishika kasi, vyanzo vya habari vya chombo hiki vilikiri kwamba yamechochewa na mienendo ya kijeshi kwenye uwanja wa vita, ambapo Ukreni inakabiliwa na mparaganyiko wa mashambulizi-pinzani, na hali ya kisiasa Marekani na Ulaya.

Mparaganyiko wa Mashambulizi-pinzani
Kwanza kabisa, kuna ongezeko la watu wanaokiri kwamba hakuna kiasi chochote cha msaada wa kijeshi kwa Ukreni ambao umesaidia juhudi zake za kupenya safu za ulinzi za Urusi. Hata jenerali mkuu wa Ukreni, Valery Zaluzhny, alikiri kwamba licha ya ^vitabu vya kiada^ na ^mahesabu ya NATO,^ Kiev ilihitaji kupiga hatua kubwa sana ya kiteknolojia ili kuvunja ^mkwamo^ wa sasa katika mashambulizi yake pinzani dhidi ya askari wa Urusi. ^Kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba hayatakuwepo mafanikio mazuri na ya kina,^ alisisitiza katika mahojiano na jarida la Economist la Uingereza.

Moscow, hata hivyo, kwa namna inayoeleweka haikuliafiki neno ^mkwamo,^ ikikataa kwamba haukuwepo mkwamo wowote kwenye uwanja wa vita, na kuthibitisha ukweli kwamba Urusi inaendelea kithabiti kufanya operesheni maalum za kijeshi ili kufikia malengo yake iliyojiwekea.

Ukreni ilipoteza wapambanaji zaidi ya 90,000 waliouawa na kujeruhiwa tangu kuanza kwa mashambulizi-pinzani kunako Juni 4, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alisema Oktoba 30. Iliongezwa kwamba mashambulizi-pinzani ya Ukreni yalikuwa yameshindwa kupata mafanikio makubwa katika uwanja wa vita, huku wanajeshi wa Ukreni wakipoteza takriban vifaru 600 na magari ya kivita yapatayo 1,900. Jeshi la Urusi litaendelea ^kiutaratibu na kiujasiri^ kutekeleza majukumu waliyopewa katika eneo la operesheni maalum ya kijeshi, iliongeza wizara hiyo.

Uchovu wa Ukreni
Pia kuna ongezeko la mashaka kuhusu uwezo wa kuendeleza mtiririko wa msaada kwa Ukreni, maafisa wanaripotiwa kusema hayo. Hivi karibuni tu, Baraza la Wawakilishi la Marekani lilipiga kura kuidhinisha mgao mkubwa wa msaada wa mabilioni ya dola kwa Israeli usiojumuisha mabilioni ya dola kama hayo ya ufadhili wa ziada kwa Kiev. Baada ya kutumia dola bilioni 43.9 kwa ajili ya msaada wa usalama wa Ukreni tangu Februari 2022, kwa mujibu wa Pentagon, utawala wa Biden inasemekana sasa una takriban dola bilioni 5 zilizosalia ili kupelekwa Kiev kabla ya pesa kuisha.

Hata hivyo, Idara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza mgao mpya wa msaada wa kijeshi wa dola milioni 300 kwa Ukreni siku ya Ijumaa pamoja na akiba ya dola milioni 125.

Mnamo Novemba 2, Bunge la Marekani liliidhinisha mgao wa msaada wa usalama wa dola bilioni 14.3 kwa Israeli sana sana kwa kuzingatia mirengo ya vyama, huku Seneti ya Marekani ikionesha tangu wakati huo kwamba itaainisha mgao wake wenyewe unaounganisha fedha kwa ajili ya Ukreni na Israeli.

Mswada huo unakabiliwa na mvutano mkubwa katika Seneti, na tishio la kura ya turufu kutoka Ikulu.

^Kuishiwa Nguvukazi^
Kadhalika, maafisa wa utawala wa Biden wanasemekana wana wasiwasi kwamba Vikosi vya Jeshi la Ukreni vinaishiwa nguvukazi. Ukreni imekuwa chini ya sheria ya kijeshi tangu Februari 24, 2022, huku Rais Volodymyr Zelensky akisaini amri ya uandikishaji wa wanajeshi katika nchi nzima. Huku wanaume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 60 wakiwa wamekatazwa kuondoka nchini humo, waandikishwaji mara nyingi hupewa notisi katika maeneo mbalimbali ya umma, pamoja na mitaani, kwenye vituo vya mafuta, na mighahawani. Mara nyingi utumiaji wa nguvu unahitajika kutoka kwa vikosi vya usalama na wanajeshi waendeshao uvamizi kwa watu wanaotazamiwa kuandikishwa.

Hivi karibuni sana, yamekuwepo maandamano mengi katika miji ya Ukreni, huku watu wakidai kiwango cha juu cha miezi 18 kwenye utumishi wa sasa wa lazima jeshini usio na mipaka kwa waandikishwa. Vikosi vya jeshi la Ukreni vinavyopungua kwa kasi vimekuwa vikizidi kumtia wasiwasi Rais wa Marekani Joe Biden, wandani walikiambia chombo hiki cha habari.

^Nguvukazi ni kipaumbele cha wasiwasi wa utawala huu hivi sasa,^ chanzo kimoja kilinukuliwa kusema hayo, na kuongeza kuwa wakati ambapo msaada wa kijeshi unawasilishwa Ukreni, ^iwapo hawana vikosi mahiri vya kuitumia misaada hayo, basi haitaweza kufanikisha kazi kubwa.^

Katika badiliko lingine lisilotarajiwa kwa utawala wa Zelensky, ongezeko kubwa la hivi karibuni la mzozo wa Palestina na Israeli kuanzia lile shambulio la kushtukiza lililoanzishwa na Hamas tarehe 7 Oktoba limefunika mgogoro wa Ukreni. Sambamba na uchovu wa Ukraine ambao umekua kwa kipindi kirefu, hii imezua hofu huko Washington kiasi kwamba kupata msaada wa ziada kwenda Kiev kunaweza kuwa changamoto zaidi.

Wakichambua mafanikio duni ya Ukreni kwenye uwanja wa vita, baadhi ya maafisa wa Marekani inaripotiwa walisema faraghani kwamba Kiev ina muda fulani hadi mwisho wa mwaka huu au zaidi kidogo kabla suala shinikizi la mazungumzo ya amani halijaanza. Maafisa wa Marekani wamedaiwa kuweka wazi maoni yao juu ya ^muda^ huo kwa washirika wao wa Ulaya.

Kushindwa kupiga hatua kwa Ukreni kwenye uwanja wa vita kumesababisha pia kupungua kwa uungwaji mkono wa umma ili kupeleka misaada zaidi kwenye jengo hilo tupu, walisema maafisa hao. Kura ya maoni ya hivi karibuni kwenye taasisi ya Gallup ilidhihirisha kwamba asilimia 41 ya Wamarekani wanaamini kuwa nchi yao inafanya kupita kiasi katika kuisaidia Kiev -- kutoka asilimia 24 miezi mitatu tu iliyopita.

Hata hivyo, afisa mkuu wa utawala wa Marekani aliyenukuliwa katika ripoti hiyo alikanusha uvumi kwamba Washington ilikuwa ikijaribu kuishawishi Kiev kuelekea kwenye mazungumzo, akiongeza kwamba Waukreni, ^wako kwenye shinikizo kwa mantiki ya hali ya hewa, lakini hawako kwenye shinikizo kwa mantiki ya athari za siasa kijiografia.^

Marekani imeshiriki pamoja na Ukreni katika majadiliano ya muundo wake wa ^mkutano wa amani,^ afisa wa utawala wa Biden alitajwa kusema hayo akijibu ripoti hiyo, akiongeza kwamba Ikulu ^haijui mazungumzo yoyote na Ukreni kuhusu maafikiano kwa sasa.^

Kuhusu mazungumzo ya ^amani^ na Ukreni, Moscow imeonesha mara kwa mara kwamba iko tayari kwa maafikiano, lakini Kiev imepiga marufuku mazungumzo hayo katika ngazi ya bunge. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov alisisitiza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba kwamba Moscow haingezingatia mapendekezo yoyote ya kusitisha mapigano, ^kwa sababu wakati fulani tulipozingatia hilo, Kiev ilitudanganya.^

Akizungumzia ^Kanuni ya Amani^ ya Rais wa Ukreni Volodymyr Zelensky yenye dondoo 10, Sergey Lavrov alibainisha kwamba si jambo lisilokuwa na chembe za uhalisia, ingawa nchi za Magharibi hulichukulia kama msingi pekee wa amani nchini Ukreni.

^Tunaongozwa na uhalisia mbaya, na huo ndio ambao Zelensky na kila mtu anayemwongoza kutoka Washington, London na Brussels wanasema kwa dhati kwa sauti moja, Hakuna msingi mwingine wa amani isipokuwa ile kanuni ya Zelensky.^
 
Umefanya jambo jema kuitafsir kabisa
 
Hii Vita ipo kwenye 'Stalemate'.... mazungumzo hayaepukiki.

 
"Stalemate" maana yake nin???
Kwa hisani ya Chatgpt.....


Stalemate ni hali katika mchezo, hasa michezo ya ubao kama vile mchezo wa chess, ambapo hakuna mchezaji anayeweza kufanya hatua yoyote inayofuata, na hivyo mchezo unakwama.

Katika lugha ya kawaida, stalemate inaweza kutumika kumaanisha hali ambapo watu au pande mbili zinakwama na hakuna hatua inayoweza kuchukuliwa ili kufikia suluhisho au mabadiliko.
 
Ahsante kwa tafsir


Nadhan hiyo stalemate inachagizwa kutokana na mchoko wa masponsa+vurugu za Israel dhidi ya Hamas
 
Watu wanachukulia "stalemate" kama ni ushindi kwa upande flani.,Wanashindwa kuelewa kwamba vita yeyote lazima iwe na Hali ya stalemate, ukisikia kwamba vita ya dunia ilipiganwa kwa miaka 4 Haina maana kwamba moto ulikuwa unapelekwa mwanzomwisho kila siku kwa muda wa miaka 4,

Kuna nchi hazikusaini mikataba ya usitishaji vita tangu vita ya pili ya dunia,hizi nchi inahesabika kwamba ziko vitani mpaka Leo,



Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Unamaanisha hao ambao hawajasain makubaliano ya kusitisha mapigano nao wapo kwenye stalemate mpaka leo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…