VITA VYA LIBYA NA NATO!
Nashindwa kupata majibu kwa nini Uongozi wa Urusi ulikubali kupinduliw a Serikari za Libya, Iraq, wakati WALIKUWA friendly countries na Urusi?
Maana Sasa nashuhudia Urusi akiwadhibiti hawa Wanafiki ambao walituhaminisha kuwa West ndio kila kitu.
Tena namshukuru Mungu nimeona ubabe wa Urusi kabla sijafa, maana propaganda zilituhaminisha uongo.
Kwanza Urusi walikua bado hawajashitukia ujanja wa wamarekani wa kupindua serikali za Marais waliokua wakiwachukia.
Ilikua ni kama vuguvugu TU la raia kumbe kulikua na nguvu ya west ndani yake.
Warusi walikuja kugundua janja ya west muda umeshapita na Ghadafi alishatolewa na kuuwawa siku nyingi.
Hata hivyo wakati huo Rais wa Urusi alikua Medvedev na Putin waziri Mkuu,ingawa hii sio sababu muhimu.
Sababu muhimu ni kuwa hakuna aliejua kua huo ulikua ni mpango wa west kuwatoa Viongozi wasiowapenda.
Urusi walikuja kushituka kwa Bashar Al Assad wa Syria pale wamarekani waingereaza na wafaransa walipowafadhiri waasi wa Syria na wale jamaa wa ISIS ili wamtoe Assad ndipo Urusi waliposhitukia mbinu hii na kupeleka jeshi kibabe na kwenda kumuokoa Assad Hadi Leo yupo.
Urusi pia walimuokoa Rais Edogan wa Uturuki ambae pia alifanyiwa njama za kupinduliwa kwa mipango ya Marekani.
Urusi pia walimuokoa Nikolas Maduro alipotakaiwa kupinduliwa kwa maandamano kwa Hila za Marekani.
Urusi pia walimuokoa Rais wa Beralus aliponea chupuchupu kupinduliwa kwa Hila za Marekani.
Urusi pia hivi juzi walionekana kujiingiza kwenda kumuokoa kama nchi yake na za washirika wake kama zingevamiwa ili kuwaondoa Rais wa Niger na Marais wa nchi rafiki akina Bukina Faso dhidi ya vitisho vya ECOWAS waliotaka kuwavamia Viongozi wa kijeshi walikataa kua vibaraka wa wafaransa na west badala yake wakawa upande wa wananchi wa Niger.
Hapa Urusi pia aliwatuma Wagner tayari Kwa mtanange na ECOWAS pamoja na west.
Sasa naona Urusi kaamua kutibua Hila za mabeberu kote duniani