mkuu F-16 ni mojawapo ya ndege nzuri za kivita ingawa ukweli utabaki pale pale kwamba F-16s hazitakua na uwezo wa kubadilisha balance of power kwenye vita hii, ni kama ambavyo western weapons nyingine zilizopita lakini zinaweza kusababisha uharibifu kwa Russia.
Kwa mda sasa Ukraine imekua inapokea makombora ya AGM-88 kutoka US, mengi yakiwa ni version B (AGM-88B), na baadhi ya version E (AGM-88E).
View attachment 2855929
Wakasaidiwa na mainjinia wa Poland kuweza kuya intergrate yaweze kutumika kwenye Mig-29s na SU 27s za Ukraine ingawa kombora hizi hazikuwa na performance nzuri sana sababu ya limitations kwenye modifications za Mig-29s na SU-27s ili ziweze kuyatumia makombora hayo ukilinganisha na yatakavyotumika kwenye F-16s.
View attachment 2855923
Nadhani ni program ya NATO kufanya modification ya ndege vita za Ukraine ili ziweze kutumia silaha za west, mfano Mig-29 pia waloifanyia michakato iweze kubeba JDAMS.
View attachment 2855955
Recently US ameunda version nyingine ya kombora hizi, version G (AGM-88G) ambazo zina range mpaka ya 300km na ziko faster zaidi.
Sasa kombora hizi zitakua na performance nzuri zikitumika kwenye F-16s kuliko jinsi ambavyo zimetumika kwenye Mig-29s na SU-27s, na zinaweza kuleta uharibifu kwa Russia.
Kama nilivyosema mwanzo kwamba ndege hizi hazitaweza kubadilisha upepo wa vita kwa kiasi kikubwa sababu Russia yuko more superior kwa vitu vingi ukilinganisha na Ukraine, ila uwepo wa F-16s unaweza kuwasababishia hasara kwa baadhi ya vifaa vyao vya kijeshi vya Russia.
Ni wazi kwamba Russia atareplace hizo losses zitakapotokea ila ni vyema zaidi kwa Russia kujipanga kiulinzi ili kuzuia losses kwa sababu kureplace pia ni gharama.
Haya ni mawazo ya sisi tulioko huku mabondeni, think-tanks wa Kremlin wanajua zaidi na wamejipanga zaidi kudeal na tishio hilo la F-16s na pengine wameshazitafutia muarobaini wa jinsi ya kudeal nazo.
Russia amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye SMO yake, maana alikua na malengo ya demilitarization na denazification na sio ku occupy Ukraine. Ameendesha SMO yake kwa utaratibu wake tofauti na mawazo ya wengi walivyokua wanafikiria/wanataka iwe.
Demilitarization imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuivunja vunja nguvu ya ukraine kijeshi, ripoti mbali mbali zimeonyesha kwa sasa Ukraine kuna shortage ya wanajeshi na silaha, ukraine imepoteza namba kubwa ya wanajeshi wake na vifaa vya kijeshi na sasa inategemea zaidi misaada ya kijeshi kutoka western.
View attachment 2855951
View attachment 2855943
Odds ziko against Ukraine, hakuna muujiza kwamba Ukraine ataishinda Russia kivita.
View attachment 2855944
Ingawa pia Russia anapaswa kukaa "kitaalamu" maana Ukraine anajitahidi kusababisha losses ili kuwapa morali na kuwapa moyo wapiganaji wake kwamba inawezekana kuharibu military assets za Russia.