Vatican anahusika vipi na hii vita?!
Umuulize Putin maana ana missiles zimelekezwa huko kama tu zilivyoelekezwa Ulaya na Marekani. Sasa sijui anahusika vipi, kiongozi.
Historia iko wazi kama nuru ya adhuhuri.
Hakuna tofali kwenye jengo la kisiasa linaloweza kuanguka au hata kumeguka, bila kuhusika mkono wa Mvatikano.
Vatikani inaweza kuchochea vita vya Ukreni kwa upande mmoja, wakati huohuo ikahamasisha juhudi za amani kwa upande mwingine.
Inaweza kuwa na marafiki wa Magharibi na Mashariki kwa wakati mmoja, ambao huwagonganisha wachapane.
Vatikani ndiyo dola pekee duniani inayoweza kufanya mbina (antics) za kucheka na kununa kwa wakati uleule mmoja.
Vatikani inaamini kwamba yenyewe ndiyo utawala maalum wa dini, siasa, uchumi na masuala ya kijamii ambao umevikwa mamlaka na Mungu ili kutenda kwa niaba ya mbingu -- ikiwa na maana kwamba yenyewe inategemea kwamba watu, jamii, nchi na serikali zote zipate kwanza shauri na idhini kwake kuhusu mambo yao.
Vatikani inaamini kwamba kuna mungu-mtu duniani ambaye ndiye papa mwenyewe, anastahili kuabudiwa na kufuatwa anachosema.
Marekani kwa sasa ni taifa la Kikatoliki kwa asilimia kubwa, tofauti na ilivyokuwa 1776 (Uprotestanti).
Kwa nini Marekani na Russia hawajawahi kuwa marafiki? Jibu liko hapo.
Ukatoliki pamoja na ukatili na ujahili wake uliokuwepo katika zama za giza, ndio huuhuu uliopo leo -- haujabadilika hata jino moja.
Kama umebadilika, basi ni kwa kuimarika zaidi kuelekea upande uleule wa kinyama -- kwa nje anaonekana ni mwanakondoo lakini ndani ni mbwamwitu si wa sayari hii.
Taifa lolote linaweza kutenda vyovyote (hata kuendesha mauaji ya kimbari kama Rwanda & Burudi au mauaji ya Wayahudi chini ya Hitler), ilimradi maslahi ya Vatikani yamewekwa kipaumbele.
Huamini? Soma historia, ambayo iko wazi kama jua la adhuhuri msimu wa kiangazi.