Kwa NATO na USA hiyo itakuwa ni "nightmare" kwani ikiwa hivyo maana yake ni kwamba hawatakuwa na uhakika hatua zinofuata za Russia juu yao wote pamoja na nchi jirani na Russia.
Marekani na NATO daima wanapenda kuzua vimbwanga kweli.
Hivi Ukreni ingebaki nyutro kama yalivyokuwa makubaliano yao ya awali, hivi vita leo vingekuwepo?
Kama NATO isingediriki kusogeza pua zao karibu na Urusi, maelfu ya watu wasio na hatia wangeuawa?
Mwaka 2022 Februari wakati wa kuanza SMO, Zelensky na washauri wake (hasa Uingereza), wangeridhia kumsikiliza Putin, leo hii majanga haya yangekuwepo?
Marekani hataki kabisa Urusi ajisogeze karibu naye (mfano mzuri ni ule mtikasi wa Cuba na hata Venezuela); kwa nini adhani Urusi atafanya tofauti?
Ni wazi kwamba mchonganishi ni nani; na anafanya hivyo kwa manufaa yake mwenyewe.
Marekani bila vita vya nje, ndani mwao hutokea fukuto lisilokalika.
Mabepari wakubwa ndio wamiliki wa makampuni ya viwanda vya silaha na zana za kijeshi. Bila vita, miradi yao inakufa.
Marekani huvuruga amani katika mataifa kwa lengo la kujichotea rasilimali na kupanua himaya yake.
Kwa hiyo, hofu ya Marekani kuhusu kuipoteza Ukreni inatokana na ukweli kwamba maslahi na ushawishi wake vinadorora duniani.
Marekani anatumia mataifa mengine kama ngao yake mwenyewe.