Mkuu vita ya Ukraine imetufunulia mengi tulivyokua tunadanganywa.
Urusi peke yake inapigana na silaha dhidi ya jeshi linalopewa silaha Bora kabisa kutoka nchi tulizoambiwa ni nchi zenye tech ya Hali ya juu sana ya silaha,yaani nchi zote za west.
Achilia mbali silaha pia Ukraine imekua ikipewa mafunzo Bora kabisa kutoka nchi tulizokua tuliambiwa ni nchi Bora kijeshi hapa duniani,yaani nchi ya USA na NATO yake.
Sio TU silaha Bora na mafunzo Bora,Bali Ukraine imekua ikipata ushauri kutoka Kwa makammanda Bora kabisa wa USA,UK,FR, German NATO wengine.
Lakini muhimu zaidi ambacho Ukraine amekua akipata ni huduma za satellite za kijeshi na za kiraia kutoka nchi zote za west kwa ajili ya kuonesha mienendo ya jeshi la Urusi.
Na zaidi kuliko yote ni huduma za kiintelijensia.
Ukraine imepata faida kubwa sana ya misaada ya intelijensia kutoka mashirika ya kijasusi ya kijeshi na kiraia kutoka nchi zinazosifika katika tasnia hiyo ambazo ni USA,UK, German,fr, na NATO wengine.
Lakini Cha ajabu Urusi peke yake imeweza kuwadhibiti kabisa licha ya misaada yote hiyo.
Dunia inashihudia Yale iliyokua haiyajui.
Hii ni vita ya kihistoria itakayobadili mengi.
Hii ni vita itakayopelekea nchi za NATO kudharaulika, ni vita itakayopelekea Russia kufanikiwa zaidi katika uuzaji wake wa silaha.
NATO hadi sasa wanatafakari kuchukua maamuzi magumu sana lakini bado wana mvutano, huu mvutano kuna ambao wanakataa aibu na fedheha inayokwenda kutokea na wengine wakiogopa matokeo watakapofanya maamuzi magumu.
Kikubwa nachokiona baada ya vita kuisha ni kutumia billions za dola kutengeneza documentary za uongo na kupotosha watu kuhusu vita hii, kuandika vitabu na kutengeneza filamu za uongo na kweli, utakuja kusikia Russia alikuwa na vifaa vya kizamani vyenye kutu na kila aina porojo.
Hawa jamaa ni kawaida yao kupindisha ukweli, Russia ni jitu la kutisha, WWII kuna mengi yalifichwa, ukisoma Russia wanavyoelezea WWII ilivyokuwa ni tofauti na hao jamaa.
Ikumbukwe WWII kutoka mashariki Russia pekee ilikuwa nchi ya kwanza kuingia Germany, huku US , France na UK zikitoka magharibi wakamkuta Russia amepiga kambi tayari Berlin. Hivyo West kutengeneza NATO wanaifahamu siri na nguvu ya Russia kijeshi toka WWII.
Ngoja tusubiri Hollywood movies, NetFlix documentaries za mchongo kutoka West...
Novels za mchongo, internet itachafuliwa kwa habari za kupotosha.
All in all vitendo vinaongea kuliko maneno.