Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 13,481
- 26,392
Haya maswali yako yote jibu ni moja tu.Hio movie naisubiri kwa hamu sana.
Je, Zelensky atakaa pale Kyiv akubali akutwe na majeshi ya Russia kama sehemu ya kuonyesha uzalendo na kutokata tamaa?
Kwa sababu akikimbia itakuwa aibu na fedheha,askari walioko vitani watamuona msaliti, kama wengine wamefariki vitani kwa nini yeye akimbie?
Je kutatokea nini Russia wakifika Kyiv? Je NATO itapeleka majeshi, kwa maana tunaona sasa NATO wakiongozwa na France wanapiga mikwara kupeleka askari Ukraine sasa sifahamu wanamtishia Russia ama wanamaanisha naona maji yanazidi unga.
Je NATO watakubali Zelensky waliyemshawishi apambane na Russia akamatwe kama kuku huku wao wakishuhudia, hii nayo ni aibu kwao NATO.
Maswali ni mengi sana nakosa majibu.
Ngoja tusubiri
Marekani haitokaa kamwe iruhusu Urusi ajitwalie ushindi na heshima dhidi yake. Urusi nayo vilevile.
Umoja wa NATO uko tayari kuwatoa kafara watu wote ulimwenguni, ikiwezekana, ilimradi ijaribu kujisitiri aibu.
Kauli za Putin nazo haziko mbali na ukweli huo mchungu.
Maana yake ni nini? Tunaelekea kushuhudia mtukuso wa kijeshi (military showdown) wa namna yake ambao haujawahi kutokea kamwe katika historia ya ulimwengu.
Matokeo? Muda wenyewe utazungumza. Lakini ukweli tuujuao yakini ni kwamba kamwe katu hatakuwepo mshindi--si Marekani wala Urusi!