Si rahisi kwa Russia hata kidogo kuibeba Ukraine yote yenye kupewa msaada na nchi kubwa duniani.
Inaweza kuchukua miaka 8 hadi 10 ya mapigano, sidhani kama ana nguvu kazi hiyo.
Kumbuka upande wa pili nao wanachoka.
Urusi ana nafasi nzuri kwa sababu rasilimali zote zinazohitajika kuendesha vita muda mrefu anazo...upande wa pili hadi wachangishane alafu kuzifikisha Ukraine ni kazi nyingine sababu inabidi wazigawanye vikundi vidogovidogo Jambo ambalo ni risk pia kwa sababu, humo kwenye vikundi vidogovidogo ndimo Urusi alimoficha majasusi wake.
Wakisema wasafirishe kwa kutumia meli kubwa au train/kuweka mayai yote kapu moja ili kuokoa gharama za usafirishaji wanajikuta wanapata hasara kubwa sababu satellite za Urusi zitakuwa zinawafuatilia toka hukohuko America na ulaya na atatumia wale malaika wake pendwa kina Kinzhal, Dagger, Islanders nk kuzamisha meli na treni zenye kubeba silaha hizo pamoja na vibebeo vyake.
Mimi nawaambia watu siku zote kwamba, kuingia vitani na Urusi ni sawa na kudumbukia kwenye karai la kukaangia maandazi.
Urusi inatisha sana sema haiwekwi wazi na hawa wamagharibi waliowekeza sana kwenye vyombo vya habari!
Ukiichunguza Urusi vizuri utagundua ipo kwaajili ya kurejesha utaratibu wa kibinadamu duniani alafu ikisharudisha utaratibu wa kawaida inakaa kimya bila kujitangaza wala kuonesha makucha yake.
Kama Mungu anayatumia mataifa, basi utagundua Urusi imekuwa ikitumika pale tu inapoonekana kusudi la Mungu duniani linakiukwa!
Tuwe tu watazamaji huku tukishuhudia mifumo salama ya dunia ikirejeshwa japo ni kwa taratibu ili wapumbavu wasijue kipi ni kipi.
Kama tukienda kwa mwendo huu mdogo, basi tutafika ule wakati wa maarifa kuongezeka sana duniani pande zote kwa kuwango cha kutisha kitu kitakachopelekea mapatano ya upendo na kuheshimiana/amani iliyo kuu.
Tukienda kwa mwendo mkali tutafikia mapatano ambayo tutatangaziana amani huku wengine wakiwa wameficha mapanga 😁