Meli tatu za kivita na nyambizi ya kivita zilobeba silaha za kinyukilia za Russia zimetia nanga kwenye bandari ya Havana, Cuba.
Picha na Reuters.
Meli hizo zikiongozwa na meli iitwayo Gorshkov na nyambizi hiyo ya kivita iitwayo Kazan zilipokelewa jana na meli ndogo ya kuongozea meli bandarini mjini Havana.
Bendera za Cuba na Russia zikionekana kuning'inia katika nyambizi hiyo.
Nyambizi hiyo ya Kazan imebeba makombora ya aina tatu Zircon, Kalibr na Onyx na wizara ya ulini ya Russia imesema vifaa hivyo vitakuwa hapo kwa mazoezi maalum.
View attachment 3016001
Wananchi wakiangalia na kuchukua picha meli ya kivita ya Gorshkov ikiwasili mjini Havana. Picha na Reuters.
Vifaa hivyo vya kivita vilipita pembeni katika pwani ya Florida kuelekea Cuba huku maofisa wa Marekani akiwemo Jack Sulivan akisema kuwa hali hiyo ni ya kawaida na hutokea mara kwa mara akimaanisha kwamba ni "routine".
View attachment 3016016
Nyambizi ya kivita ya Russia aikitia nanga katika ufukwe wa mjini Havana nchini Cuba. Picha na AFP.
Pwani ya Cuba ipo umbali wa maili 100 au kilomita 160 kutoka pwani ya Keay east mjini Florida ilipo kambi ya jeshi la majini la Marekani.