Marekani haihitaji fedha ya mtu. Kiuchumi ni dubwana kubwa sana
Umesahau kwamba Marekani ndiye kinara wa kupoka mafuta na madini na rasilimali watu kutoka mataifa mbalimbali?
Majaribio ya kisayansi na fani ya tiba umesahau jinsi yanavyoiathiri dunia kisiasa, kiafya, kiuchumi na kijamii kwa sababu tu Marekani anatafuta ukiranja wa dunia?
Nani asiyejua kwamba mizuko mingi ya magonjwa kama vile ebola na bakteria na virusi vingine ni miradi ya watu yenye nembo na muhuri wa taifa hilo?
Kwa nini Ukraine kuna janga kubwa sasa la kuchuuza viungo vya mwanadamu?
Marekani ana haki gani ya kuyaamulia mataifa mengine uongozi na mfumo wa uongozi, kama si hofu ya kiuchumi?
Kwa nini China ni tishio kubwa zaidi kwa Marekani kama si suala la uchumi? (Tiktok, Huawei, etc. zimeikosea nini Marekani?)
Kwa nini nchi tajiri kama Venezuela, Iraki, Afghanistani, Libya, Irani, Korea Kaskazini, nk. zinaishi katika ufukara unaoendelea kubarikiwa na Marekani?
Kwa nini Marekani inaweza kuivamia nchi yoyote bila kuwajibishwa, lakini nchi zingine zisifanye hivyo?
Hizi kambi za jeshi za Marekani zilizotapakaa dunia nzima zina makusudio yepi hasa?
Nalala kidogo; nikiamka ntaendelea kukuuliza maswali mengine.