Ndugu, nikusaidie tu. Ile miezi miwili baada a kuanza kwa SMO jeshi la Ukraine lilikuwa limevurugwa kwa zaidi ya 85%. Kwa maana ya miundo mbinu ya kijeshi kuharibiwa, hii ni pamoja na zana za kivita kama vifaru, ndege, magari nk.
Ndio zikaanza zile packege za misaada toka west na marekani. Wamechagishana weee mzigo ukiisha, inatumwa packege nyingi. Mchezo ndio huo mpaka sasa.
Upande wa wanajeshi. Mpaka sasa wanajeshi waliopo front 70% sio waUkraine. Ni mamluki toka nchi mbali mbali. Kwa mazingira haya ulitegemea Russia amalize hii SMO?
Mkuu umezingatia uongo na visingizio badala ya sababu kuu. Kinachoifanya Urusi ishindwe ni uwezo mdogo wa kujipanga wa maofisa wake wa kijeshi, kuna mijizi kule na mishibisha tumbo ilikuwa imekaa tu. Manaibu mawaziri wawili wa wizara ya ulinzi ya Urusi wamekamatwa kwa makosa ya ubadhirifu na rushwa. Ngoja nikutajie majizi:
1. Jenerali Dmitry Bulgakov, naibu waziri.
2. Timur Ivanov, naibu waziri.
3. Lt. Gen. Yury Kuznetsov, mkuu wa kitengo cha utumishi jeshini.
4. Maj. Gen. Ivan Popov, huyu mwanzoni mwa vita Ukraine alikuwa na nafasi kubwa.
5. Lt. Gen. Vadim Shamarin huyu alikuwa msaidizi wa Chief of Staff.
6. Vladimir Verteletsky, mkuu wa ugavi jeshini.
Sasa hata kama mnasema naichukia Urusi (in fact naikubali Urusi kuliko mashabiki walioipenda vita ilipoanza). Ina maana Putin anawaonea hawa wote sita?
Unajua siku 3 za mwanzo Ukraine ilizuia mashambulizi ya Urusi. Oleksandr Syrsky alipanga vikosi vyake vya ardhini kipindi kile ni mkuu wa jeshi la ardhi vikailinda Kyiv isianguke. Msaada wa silaha ulikuja baadae watu wamejitetea tiyari. Battle of Hostomel pale Urusi ilishindwa, hapo Ukraine haina silaha hata moja ya msaada.
Urusi ikikutana na China vitani ndio mnaweza jua kumbe ina uozo mwingi jeshini. Ukraine ilivyokuwa hata Misri ingeipiga.