T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Prigozhin alikuwa sahihi kukasirika. Alafu hakuwa na lengo la kufanya mapinduzi ndio maana hakufanya recruitment wala hakumshirikisha kiongozi yeyote wa kijeshi au usalama.Waliepusha mapigano yaso muhimn kati ya friendly forces yaani Wagner na Russian army . Shida ilikua kubwa inayotatulika. Hivyo suluhisho likawa ni mazungumzo. Putin ni mtu wa visasi alichomfanyia Kwa msela ake wa zamani wote tulishangaa
Prigozhin alitaka Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi waondolewe. Yeye aliwaona ni dhaifu na wanaochelewesha vita kuisha. Sijajua alitumia vigezo gani, ila ukizingatia yeye ni mpishi kwa taaluma wala sio mwanajeshi ila aliweza iongoza Wagner vizuri na kila ilichokifanya kinaonekana. Lazima tu alikuwa anajua kwa uwezo wa jeshi la Urusi, kwa resources na ukubwa ni performance ipi ilitakiwa na matokeo gani yapatikane. Nani asiyejua kazi nzuri ya Wagner kule Syria kupambana na ISIS? Nani asiyejua kazi ya Wagner kule Bakhmut?
Kiasili Prighozin ni mhuni, mhalifu, jambazi, fighter wa kuzaliwa. Pale jeshini kuna wale majamaa waliajiriwa ili wapate mishahara, jeshi ni ajira sio asili yao. Maofisa ni kamlete, zamani wengine walikuwa wanahonga kupanda vyeo, mwenye utii na unyenyekevu "chawa" ndio anapanda.
Mwisho wa siku jeshi linajikuta na watu wa kawaida wengi juu. Akitokea aliyenyooka kama Surovikin anaonekana mnoko, anajipendekeza au anatafuta vyeo, na kawaida mtu kama huyo sio ndio mzee hivyo hapendelewi kivile na serikali.
Akitokea kama boss wa Wagner alivyokuwa basi maofisa wanaogopa anaonyesha udhaifu wao, wanamcheleweshea supplies na ammunition wanampa kwa kumpimia. Wanafanya apate vifo na majeruhi wengi makusudi.