LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mkuu, Putin anatafuta pa kujificha. Hivi unapoanzisha ugovi na mwezako ni budi ufahamu kuwa adui yako ana marafiki zake ambao watamsaidia pindi atakapo zidiwa kivita, na kwa bahati mzuri Putin alilijua hilo ndio maana akatoa onyo kwa Nchi yeyote ile itakayo msaidia Ukraine, ataipiga kipigo cha mbwakoko. Leo ndio anatambua kuwa kuna wanao msaidia Ukraine, sasa kwa nini asiwachape? Mbona yeye ana saidiwa lakini wenzake wapo kimia tu. Apambane na hali yake.
 
Nasisistiza Tena NATO wanapigana na Urusi Kwa kificho hivyo Urusi inakosa uhalali wa kisheria kuzishambulia nchi zinazoisaida Ukraine.
Unajifanya mjuaji kumbe unajikanyaga tu,nani kakuambia urusi anafuata Sheria.,tuambie alipovamia Ukraine alifata Sheria ipi ya kimataifa.,hivi una habari umoja wa mataifa uliiamuru urusi iondoe majeshi yake na kukomesha uvamizi wake Ukraine?! Vip alitii?

Pumba tupu!
 
Ukrainian forces attempt to take the village of Vesela and move west and appear behind the Russian troops in that part of the battlefield. Towards the north there is a natural border, the River Seym which prevents the Russians from bringing in reinforcements. the Plan remains brilliant.
 
😂😂😂😂 ivyo vijiji vyote unavyonyesha hapo visharudi zamani sana nashangaa sijui unapata taarifa kwenye google acount baada ya google search
 
Kursk direction. The Armed Forces of Ukraine are approximately 700 meters from the Tyotkino village municipality building and continue to advance. Russian soldiers who don't flee will be eliminated.View attachment 3095086
🤣🤣🤣🤣 ivi ujachoka tu kuokoteza habari kwenye vijiwe vya kahawa.yani wenzako wanaikimbia Kurks, wewe unaleta taarifa ya kwamba wanasonga mbele.we kweli unachekesha😂😂😂😂
 
Kama mimi sijaelewa vibaya, Ukraine Yuko mbele, warusi wapo nyuma wanakuja na mto uko mbele ya Ukraine, nadhani Ukraine ndio inabidi wavuke mtu Ili waendelee na offensive
Always mwenye ugumu ni yule anatakiwa kuvuka mto
 
Russia ni nchi pekee yenye makombora ya kutungua satelite.Walizindua miaka miwili nyuma na yana indefinite flight time,nikimaanisha chanzo chake cha nguvu ya kuyasukuma ni endelevu.
Hizo missile ambazo wanaziita burevestinik bado ziko kwenye experimental phase huo uwezo wa unlimited flying distance maana yake inaweza kwenda kokote bado ni in theory. Na umesemwa kwasababu hizo missile zitakuwa ziko powered na nuclear reactor..

So yes its a new technology kwa upande wa missile ila kutumia nuclear reactor ku power machines and other things sio teknolojia mpya kwa sasa napata wakat mgumu wa kuamin kuwa after two years bado Russia ndio iwe pekee yenye uwezo wa kutungua satelite... dunia ya sasa unaweza ukadumu na ugunduz wako hardly a year . Utak unataka watu watafanya kama ww..

Baada ya computer hakuna ugunduz mpya dunia .. ni maboresho tu
 

Tupate wadhamini kidogo...​

Bomu la nyuklia la USSR lililoishangaza dunia​


fano wa bomu lililopewa jina Tsar Bomba


Mapema asubuhi, mnamo 30 Oktoba 1961, ndege ya kuangusha mabomu ya Muungano wa Usovieti aina ya Tu-95 ilipaa kutoka uwanja wa kambi ya ndege za kivita ya Olenya katika rasi ya Kola kaskazini mwa Urusi.
Tu-95 ilikuwa ndege kubwa sana yenye injini nne ambayo iliundwa mahsusi kubeba mabomu.
Katika mwongo mmoja uliotangulia, Muungano wa Usovieti ulikuwa umepiga hatua sana katika utafiti kuhusu nyuklia.
Marekani na USSR zilikuwa zimejipata upande mmoja wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia lakini baada ya vita, kukatokea Vita Baridi.

Wasovieti baada ya kujipata wanakabiliwa na taifa pekee lililokuwa na silaha za nyuklia, iliona njia pekee ya kushindana vyema na Marekani ilikuwa ni kuwa na silaha zake za aina hiyo.
Tarehe 29 Agosti 1949, Wasovieti walikuwa wamefanyia majaribio silaha yake ya kwanza ya nyuklia kwa jina 'Joe-1' katika eneo ambalo sasa linapatikana Kazakhstan.
Walitumia ujuzi uliopatikana kwa kuingia kisiri na kupata taarifa kuhusu mpango wa atomiki wa Marekani.
Katika miaka iliyofuata walikuwa wamepiga hatia sana. Walikuwa wamelipua silaha zaidi ya 80 za atomiki kipindi hicho. Mwaka 1958 pekee, Wasovieti walikuwa wamefanyia majaribio mabomu 36 ya nyuklia.
Lakini hakuna bomu hata moja walilokuwa wamefanyia majaribio awali ambalo lilikaribia bomu lililokuwa limebebewa na ndege hiyo aina ya Tu-95.
Lilikuwa bomu kubwa sana, bomu ambalo halingetoshea sehemu ya kubebea mabomu ya ndege.
Bomu hilo lilikuwa na urefu wa 8m (26ft), kipenyo cha karibu 2.6m (7ft) na lilikuwa na uzali wa tani 27

Muonekano wake ulikuwa sawa na mabomu yaliyopewa majina 'Little Boy' na 'Fat Man' ambayo yalikuwa yameangushwa na Marekani katika miji ya Hiroshima na Nagasaki miaka kumi na mitano awali.
Bomu hilo lilifahamika kwa majina mengi sana kiufundi - kuna walioliita Project 27000, Product Code 202, RDS-220, na Kuzinka Mat (Mamake Kuzka).
Lakini sasa hufahamika zaidi kama Tsar Bomba - 'Bomu la Tsar'.
Tsar Bomba halikuwa bomu la kawaida la nyuklia.

Bomu hilo lilifanyiwa majaribio katika kundi la visiwa vya Novaya Zemlya
Lilikuwa matunda ya jaribio la wanasayansi wa USSR la kuunda silaha ya nyuklia yenye nguvu zaidi duniani wakati huo.
Aidha, walitiwa hamasa na hamu ya waziri Mkuu Nikita Khruschchev ya kutaka kuwa na silaha ambayo ingeufanya ulimwengu kutikiswa na 'kunyenyekea' kutokana na teknolojia ya silaya ya Muungano wa Usovieti.
Ilikuwa zaidi ya kifaa cha chuma ambacho hakingetoshea ndani ya sehemu ya kubebea mabomu ya ndege kubwa zaidi ya kivita - ilikuwa ni silaha ya maangamizi makubwa, silaha ya kutumiwa wakati wa mwisho kabisa.
Ndege hiyo ya Tupolev (Tu) ilikuwa imepangwa rangi nyeupe kupunguza madhara ya mwanga ambao ungezalishwa na mlipuko wa bomu hilo.
Ndege hiyo ilifika eneo la kuangushwa bomu Novya Zemlya, eneo ambalo halikuwa na watu katika visiwa vya Bahari ya Barents juu katika kaskazini maeneo yenye barafu ya USSR.
Rubani wa ndege hiyo ya Tupolev Meja, alifikisha ndege hiyo Ghuba ya Mityushikha Bay, eneo la kufanyia majaribio silaha la muungano wa Usovieti na kufika karibu 34,000ft (10km) juu angani. Ndege nyingine ya kuangusha mabomu aina ya Tu-16 ilipaa karibu na ndege yake, lengo lake likiwa kupiga video mlipuko wa bomu hiyo na kuchunguzaathari za mlipuko huo hewani ikipitia eneo la mlipuko.
Ili kuhakikisha ndege hizo mbili haziharibiwi - na uwezekano wa kutodhurika ulikuwa asilimia 50 - ilipangwa kwamba Tsar Bomba iangushwe kwa parachute ya uzani wa karibu tani moja.
Bomu hiyo lingeshuka hadi kiwango kilichotakikana- 13,000ft (3,940m) - na kisha kulipuka.
Wakati wa mlipuko, ndege hizo za kuangusha mabomu zingekuwa karibu 50km (30 miles) mbali na eneo hilo. Umbali huo ungetosha kuzuia ndege hizo kuathirika.
Tsar Bomba ililipuliwa saa 11:32, saa za Moscow. Ghafla, bomu hilo lililipuka na kusababisha moto mkubwa wa upana wa karibu maili tano. Moto huo ulipaa angani kutoka eneo la mlipuko kutokana na nguvu za mlipuko wenyewe. Mwanga wa mlipuko huo ungeonekana na watu waliokuwa umbali wa 1,000km (maili 630).
Wingu la mlipuko lililofanana na uyoga lilipaa juu hadi 64km (40 miles), sehemu ya juu ikiwa imepanuka kwa karibu 100km (maili 63) kuanzia sehemu moja hadi nyingine. Kilikuwa kitu cha kushangaza sana bila shaka.
Katika eneo la Novaya Zemlya, madhara ya bomu hilo yalikuwa ya kuogofya.
Katika kijiji cha Severny, 55km (maili 34) kutoka eneo la mlipuko, nyumba zote ziliharibiwa kabisa.
Hii ni sawa na nyumba zote zilizo katika uwanja wa ndege wa Gatwick nchini Uingereza zikiharibiwa na mlipuko uliotokea katikati mwa London.
Katika wilaya za Muungano wa Usovieti zilizokuwa mamia ya maili mbali na eneo la mlipuko, uharibifu wa kila aina ulitokea. Nyumba ziliporomoka, mapaa ya nyumba yakaanguka, vioo kwenye madirisha vikavunjika na milango ikaharibika pia.
Mawasiliano ya redio yalitatizika kwa zaidi ya saa moja.
Durovtsev na ndege yake ya Tupolev walikuwa na bahati kunusurika - mlipuko wa bomu hilo ulisababisha ndege hiyo kushuka ghafla zaidi ya 1,000m (3,300ft) kabla ya rubani huyo kuweza kuidhibiti tena.

dege aina ya Tu-95 ilitumiwa kuangusha bomu hilo
Mpiga picha wa Usovieti aliyeshuhudia mlipuko huo alisema baadaye:
"Mawingu chini ya ndege na maeneo ya mbali yalitiwa mwanga na nuru ya ghafla yenye nguvu. Mwanga huo ulienea na kuwaka hivi kwamba ungeweza kuona ndani ya mawingu. Wakati huo, ndege yetu ilitokea kutoka katikati ya mawingu mawili na chini kitu kilichofanana na mpira cha rangi iliyokolea ya machungwa kilikuwa kinajitokeza. Kilikuwa cha kuogofya na kilifanana na sayari ya Jupiter. Aste aste, kilianza kupaa juu. Kilionekana kana kwamba kilikuwa kinaimeza Dunia. Lilikuwa tukio la kushangaza sana, sijawahi kuliona.
Tsar Bomba ilizalisha nishati ambayo nguvu zake zilikuwa haziwezi kufikirika.
Kwa sasa, inasadikiwa kwamba bomu hilo lilizalisha nishati ya megatani 57 au sawa na tani milioni 57 za TNT. Hiyo ni mara 1,500 zaidi ya mlipuko wa mabomu ya Hiroshima na Nagasaki kwa pamoja

Aidha, ni mara kumi zaidi ya nguvu za mabomu yote ambayo yalilipuliwa wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Mlipuko kama huo haungewekwa siri.
Ndege ya kijasusi ya Marekani iliyokuwa kilomita elfu kadha kutoka eneo hilo, ilikuwa na kifaa cha kupima milipuko ya nyuklia kwa mbali.
Takwimu kutoka kwa ndege hiyo zilitumiwa na wataalamu wa jopo la kufuatilia silaha za nchi za nje la Marekani kukadiria uwezo wa bomu hilo.
Muda si muda, mataifa yalianza kushutumu kitendo hicho cha USSR.
Marekani na Uingereza, na hata nchi za Ulaya majirani wa muungano huo mfano Sweden.
Bahati pekee ni kwamba wingu la mlipuko huo halikuwa limefika ardhini, jambo lililosababisha kiwango cha miali nururishi iliyotokana na bomu hilo kuwa chini sana.
Hali ingekuwa tofauti sana kama hilo lingetokea.
Ni bahati kwani bomu hilo lilikuwa limefanyiwa mabadiliko kidogo kupunguza uwezo wake. Tsar Bomba ilikuwa imeundwa kuwa na uwezo mara mbili ya uliokuwa kwenye bomu hilo lilipolipuliwa.
Mmoja wa waliohusika zaidi kuunda bomu hilo alikuwa mwanafizikia Andrei Sakharov ambaye baadaye alipata umaarufu sana kwa kuongoza juhudi za kumaliza silaha za nyuklia - ambazo alikuwa mwenyewe amechangia kuziunda na kuzistawisha.

akharov aliunga mkono kupigwa marufuku kwa majaribio ya silaha za nyuklia. Alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1975.
 
Kutupa makombora ya Storm Shadow ndani ya Russia ni lazima wahandisi wa UK (ambao ndo wenye ujuzi nayo) watumie mitambo ya Satelite ambayo pia ni ya UK, hivyo moja ya majibu ya Russia yaweza kushambulia satelites za UK na kuharibu kila kitu kinotegemea mitambo hiyo huko UK.

Ndo maana NATO na US wapo Washington kujadili waaamue Zelensky aruhusiwe (au wenyewe wajiruhusu) watupe makombora hayo ndani ya Russia au vipi.

Putin katupa mpira ulingoni mwa NATO/US kazi ni kwao yasubiriwa nani aanze.

Ndo maana kucheza Chess na Putin ni kazi ngumu.
 
Ndiyo, makombora ya kutungua satelaiti yalishatumika katika mazingira halisi, ingawa matukio haya yalikuwa machache na kwa kiasi kikubwa yalikuwa majaribio ya kijeshi.

Hapa kuna mifano michache:

• Marekani (1985): Marekani iliharibu satelaiti yake mwenyewe ya upelelezi (Solwind P/N) kwa kutumia kombora la ASAT. Hii ilikuwa jaribio la kuonyesha uwezo wa Marekani wa kukabiliana na vitisho vya satelaiti za adui.

• China (2007): China iliharibu satelaiti yake mwenyewe ya hali ya hewa kwa kutumia kombora la ASAT. Hii ilikuwa jaribio ambalo liliunda kiasi kikubwa cha uchafu wa anga, na kuzua wasiwasi kuhusu hatari ya matumizi ya silaha hizi.

• India (2019): India iliharibu satelaiti yake mwenyewe ya upelelezi kwa kutumia kombora la ASAT. Hii ilikuwa jaribio la kuonyesha uwezo wa India wa kukabiliana na vitisho vya satelaiti za adui.

• Urusi (2022): Urusi ilishambulia satelaiti ya Kosmos-1408, ambayo ilikuwa imetumika kwa muda mrefu, kwa kutumia kombora la ASAT. Huu ulikuwa tukio la kwanza la nchi moja kuharibu satelaiti ya nchi nyingine tangu 1985.


Ni muhimu kutambua kuwa matumizi ya makombora ya ASAT ni nadra sana, na yanaweza kuwa na madhara makubwa. Kuna juhudi za kimataifa za kupunguza hatari ya matumizi ya silaha hizi, ikijumuisha mikataba na kanuni mbalimbali.


Licha ya matumizi machache yaliyorekodiwa, uwepo wa makombora haya na uwezo wao wa kuangamiza satelaiti ni jambo linaloendelea kuzua wasiwasi kuhusu usalama wa anga na amani ya kimataifa.

...........................................................................
. Makombora haya yanajulikana kama Anti-satellite weapons (ASAT) au makombora ya kupambana na satelaiti.

Jinsi yanavyofanya kazi:

Makombora haya yanaweza kutungua satelaiti kwa njia mbalimbali, ikijumuisha:

• Kugongana kimwili: Kombora linaweza kugongana na satelaiti, na kuivunja vipande vipande.

• Kulipua karibu: Kombora linaweza kulipuka karibu na satelaiti, na kuzalisha wimbi la mshtuko linaloweza kuivunja au kuidhuru.

• Kupeleka silaha za elektroniki: Kombora linaweza kupeleka silaha za elektroniki ambazo zinaweza kuingilia mfumo wa uendeshaji wa satelaiti, na kuifanya iwe isiyoweza kutumika.

Nchi zinazozalisha:

Nchi kadhaa zimeendeleza na kujaribu makombora ya ASAT, ikijumuisha:

• Marekani

• Urusi

• China

• India

• Israeli

Athari za matumizi:

Matumizi ya makombora ya ASAT yanaweza kuwa na athari mbaya sana, ikijumuisha:

• Kuvuruga mawasiliano: Kuangamiza satelaiti kunaweza kuvuruga mawasiliano ya simu, televisheni, na internet.

• Kuvuruga urambazaji: Satelaiti hutumika kwa urambazaji wa GPS, na kuzivuruga kunaweza kusababisha matatizo makubwa kwa usafiri na shughuli zingine.

• Kuunda uchafu wa anga: Vipande vya satelaiti vilivyovunjika vinaweza kubaki katika anga kwa miaka mingi, na kuhatarisha satelaiti zingine.

• Kuongeza mzozo: Matumizi ya makombora ya ASAT yanaweza kuongeza mzozo kati ya nchi, na kuhatarisha amani ya kimataifa.


Muhimu kutambua:

• Utumiaji wa makombora ya ASAT ni hatari sana na unaweza kuwa na madhara makubwa.

• Kuna juhudi za kimataifa za kupunguza hatari ya matumizi ya silaha hizi.


Natumaini majibu haya yanakusaidia kuelewa zaidi kuhusu makombora ya kutungua satelaiti.
 
The Ukrainian Armed Forces gained a foothold in Novy Put and transferred Obukhovka to the gray zone, there is a battle in the Vesely area;
Kursk region.
 
Wewe muite, Russia walishadungua setilate
Atazifikiaje hizo satellite. Ni vema mkajua umbali uliopo huko juu zilipo satellite. Labda afanikiwe kuharibu vituo vinavyoendesha hizo satellite
Wewe muite elimu yako ni chekechea kabisa IQ yako ni ndogo sana, sijui darasa la Saba D, sijui form four failure. Russia Wana hiyo technology toka zamani ya kufungua satellite.
 
Wewe muite, Russia walishadungua setilate

Wewe muite elimu yako ni chekechea kabisa IQ yako ni ndogo sana, sijui darasa la Saba D, sijui form four failure. Russia Wana hiyo technology toka zamani ya kufungua satellite.
Nyie ndio hamjui kitu. Na hamuangalii nje ya box. Ipo siku mtanikumbuka. Halafu IQ sio kuamini kila taarifa unayoiona mitandaoni.
 
The Ukrainian Armed Forces gained a foothold in Novy Put and transferred Obukhovka to the gray zone, there is a battle in the Vesely area;
Kursk region.
 
Wewe muite, Russia walishadungua setilate
 
Kauli ya kiume ya Putin imewachanganya wamagharibi wote.
Boden (babu) amemuita chawa wake - Starmer - wajadiliane kuruhusu mashambulizi au la.
Siku za nyuma walikuwa West wote wanajazana kwenye ukumbi wakipiga 'kelele'; baada yapanho wa Kursk kushindwa; wameitana wawili; na hali ikiendelea hivi yawezekana hata hao wawili wakasambaratika.
Nakuona comedian- Zelensky - akisistiza kuwa anataka apige launch ground zilizopo Rusia, sio civilian - nomemuonea huruma.
Na kwa muonekano wa kawaida, Zelensky amechoka kuliko hata wakulima wa kule Tanganyika - Katavi.
 
Yani we jamaa ndio huwa sikuelewi kabisa unachoandika make huwa unajichanganya kwenye maandiko Yako, yani mara useme Urusi inapigana na NATO, mara NATO Bado haijatangaza vita na Urusi, mara NATO inapigana vita na Urusi kwa kivuli/kinyonge, sasa sijui point Yako ni ipi hasa, mimi nimefuatilia vita hii toka ilipoanza hakuna popote unapoweza kunidanganya, nivile tu huwa naheshimu mawazo ya kila mtu humu, ila wewe una ushabiki uliopindukia, hakuna vita ya urusi na NATO hapo na siku ikitokea wewe mwenyewe utaona utofauti na vita inayopiganwa sasa, siungi mkono vita hivi, kiukweli Ukraine inaonekana kuelemewa lakini sio kwa mahaba haya yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…